Manifesto ya CUF kwa uchaguzi wa 2015
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015 si uchaguzi wa kawaida kwa Zanzibar. Ni uchaguzi wa kihistoria. Utatupa Wazanzibari fursa ya kihistoria kufanya mabadiliko ya msingi ya jinsi tunavyoongozwa. Ni uchaguzi utakaoamua mwelekeo wa Zanzibar yetu.