Karibu CUF Bi Rurida – Maalim Seif

Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi kutoka mkoa wa Lindi, Riziki Said Rurida amekihama chama hicho na kuhamia Chama cha Wananchi CUF. Rurida alitangaza kukihama chama hicho na kukabidhiwa kadi ya CUF na Katibu Mkuu wa chama hicho, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika jana Mchinga, Lindi…

Safari ya CUF, UKAWA inaendelea – Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amewahakikishia wanachama wa chama hicho kuwa uamuzi wa Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kujiuzulu wadhifa wake hautausambaratisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na CUF kimeendelea kubaki katika mikono salama.

Kwaheri Profesa, lakini kwa nini leo?

Hadi asubuhi hii imeshasemwa ama kuandikwa na wengi kuwa CUF ni taasisi na inafanya kazi zake ki taasisi. Mimi nasema ni Taasisi Imara iliyojengwa kwa misingi imara ya kitaasisi. Nilipokuwa University miaka ya mwanzoni mwa 1990 nilisoma somo la Organizational Behavior. Kitu kimoja nilichojifunza humo, na hupenda kukitumia mara kwa mara, ni kuwa Office (Cheo)…

Usilolijuwa usiku wa kiza

Wahenga wa Kiswahili husema “usilolijua usiku wa kiza”. Ni kawaida ya mwanaadamu ya kutojua jambo analolifanya kuwa mwisho wake litaleta athari gani, kwake au kwa jamii iliyomzunguka. Binadamu hufanya matendo mbali mbali duniani lakini baadhi yao hujikuta wakijutia yale waliyoyafanya baada ya kuona athari zake.

CCM wamezowea vya kunyonga, vya kuchinja hawaviwezi

Mtu ambaye katika maisha yake yote anapenda dhuluma, basi ni vigumu kuibadili tabia hiyo. Tabia hiyo ndio waliyonayo wanachama na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao sisi Waswahili husema wamezoea vya kunyonga, vya kuchinja hawaviwezi. Dhuluma, wizi, rushwa na ubabe ndiyo itikadi ya chama chao. CCM kimehitimisha kwa sehemu kubwa mchakato wa kupiga kura…

Mjuwe Prof. Lipumba

Ibrahim Lipumba ni mchumi wa kimataifa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF). Alizaliwa Juni 6, 1952 katika Kijiji cha Ilolangulu mkoani Tabora. Alipata elimu ya msingi mkoani Tabora mwaka 1959 katika Shule ya Wamisionari wa Sweden waliokuwa Tanzania wakati huo, shule hiyo iliitwa “Swedish Free Mission Primary School”, alimaliza mwaka 1962 na akasoma Shule…

CUF yaichukuwa wilaya ya Chemba

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya, na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Abdul Kambaya, wanaogoza ujumbe wa kampeni ya kujiandikisha wapiga kura kwenye wilaya ya Chemba ambako umla ya wananchi 700 wamejiunga na CUF kwa siku moja tu kwenye kata ya Mrijo.

Haya hapa madudu ya ZEC

Niwakumbushe tu wenzangu kwamba wimbi la mabadiliko linapofikia wakati wake huwa halizuiliki tena. CCM isitarajie kuendelea kubakia madarakani kwa kutumia njia za hadaa, udanganyifu, hujuma, nguvu, ubabe na vitisho. Hii ni nchi yetu sote na kama alivyowahi kusema Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, CCM haina hatimiliki ya nchi hii. Hatuna budi kulitambua hilo na tushirikiane…