Maalim Seif: Nitasambaza huduma ya Umeme Kwenye Vitongoji Vyote Vya Unguja na Pemba

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema endapo atachaguliwa kuiongoza Zanzibar, atasambaza huduma ya umeme katika vitongoji vyote vya Unguja na Pemba.

Akihutubia kwenye mkutano wa Kampeni kwa Jimbo la Kijini, uliofanyika katika Uwanja wa Kijiwe Mtu uliopo Matemwe nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Maalim Seif amesema kwamba kwa muda wa miaka 50 Zanzibar imekuwa na tatizo kubwa la upungufu wa nishati ikiwemo mafuta na umeme, hivyo ameahidi kulishughulikia tatizo hilo pindi tu atakapoingia madarakani.

“Nitaakikisha huduma ya uememe inafika kila pahala Unguja na Pemba, na huu umeme wa kukatakata sitaki kusikia” Alisisitiza.

Wananchi 2

Maalim Seif ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alirejea kauli yake ya kuifanya Elimu kuwa bure kwa wazanzibari wote , ili kutoa fursa kwa wananchi wenye kipato cha Chini kupata huduma hiyo.

“Mzee Karume alitangaza elimu bure kwa kila Mzanzibari, jee waliyomfuata Mzee Karume waliendelea na sera hiyo au waliiondoa? Alihoji Maalim Seif.

Alisema kwamba, Elimu ni muhimu sana kwa wananchi wa Zanzibar, kwani ndiyo rasilimali ya kibinaadamu na ya Taifa inayoamua juu ya sura na kasi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Pia alibainisha kwamba, umasikini mkubwa uliokithiri nchini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na kiwango duni cha elimu.

Alisema lengo la kutaka kuifanya elimu kuwa bure, ni hatua moja wapo ya kumuenzi Mzee Abeid Amani Karume sambamba na kuwawezesha wananchi wa Zanzibar kusoma kuanzia Chekechea hadi Chuo Kikuu.

Aidha Maalim Seif alifafanua kwamba lengo lake ni kutaka kuifanya Zanzibar irudishe hadhi yake ya kinchi ili itoe fursa ya kujiamulia mambo yake wenyewe na hivyo kuweza kujiletea maendeleo.

“Chini ya Serikali ya CUF, nawahakikishieni wananchi, kila kijana, kila mzee atajihisi ni raia wa nchi huru na atatembea kifua mbele bila ya manyanyaso wala bughudha” Aliongeza.

Wananchi 3
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Meneja kampeni wa Chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui, amewataka wananchi hao wasifanye makosa itakapofika tarehe 25 mwezi huu kwa kumpigia kura za ndio Maalim Seif Sharif Hamad ili aweze kuiongoza Zanzibar.

Mazrui amesema kwamba, kwa miaka yote 50 ya Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Zanzibar imepoteza hadhi yake, na hivyo kuwataka wananchi hao kutumia fursa hiyo ili waweze kuirejeshea hadhi yake kwa kuwaletea maendeleo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s