Ilani ya Chama Cha Wananchi CUF, katika kujenga Uchumi imara unaotoa ajira na tija kwa wote

Zanzibar bado ina uchumi wa zao moja, unaotegemea karafuu kwa wastani wa asilimia 76 ya mapato yake ya mauzo ya bidhaa zake nchi za nje. Kilimo (yaani ukulima, misitu na uvuvi) bado ndiyo sekta kuu inayoajiri kiasi cha asilimia 80 ya wananchi. Zaidi ya asilimia 25 ya mazao ya kilimo ni kwa ajili ya chakula cha mkulima mwenyewe (subsistence farming). Hali ya maisha ya Mzanzibari kwa wastani imeendelea kuwa mbaya kutokana na umasikini wa kipato. Ukuaji wa uchumi wa Zanzibar bado haujamnufaisha mwananchi wa kawaida.

Kupanda kwa kasi ya kutisha kwa gharama za maisha hakuendani na ongezeko la mapato ya wananchi walio wengi. Muundo wa uchumi unaonekana kuzorotesha uzalishaji, uwekezaji, biashara na ubunifu. Kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kunatoa fursa pekee na adhimu ya kihistoria ya kutumia vipaji na uwezo wa Wazanzibari wote walio ndani na nje ya nchi katika kuujenga upya uchumi wa Zanzibar kwa lengo la kumnufaisha Mzanzibari.

4.1. FURSA NA UWEZO WA KIUCHUMI
Zanzibar imekaa pazuri kijiografia. Uzuri wa maeneo yake na utamaduni wake unaosifika peke yake ni vivutio vikubwa kwa wawekezaji. Ina ardhi yenye rutuba nzuri inayoweza kustawisha mazao muhimu ya biashara. Bahari ya Zanzibar ina utajiri mkubwa wa viumbe vya bahari na inayo rasilimali ya mafuta na gesi asilia iliyoko katika ardhi yake na mipaka yake ya bahari ambayo pia bado haijaguswa.

Kuna maelfu ya Wazanzibari wanaoishi Tanzania Bara na nchi za nje. Wengi wao wamefanikiwa sana kiuchumi na wamekusanya rasilimali ya elimu na fedha. Hivi sasa maelfu ya Wazanzibari walio nyumbani wanatunzwa na Wazanzibari walioko nje.

Vianzio hivi vya maendeleo havijatumiwa ipasavyo kumnufaisha Mzanzibari na kuinua hali ya maisha yake. Hatujatambua umuhimu wa kuhifadhi ardhi finyu tuliyo nayo wala kupanga matumizi yake baina ya ardhi ya ukulima, makaazi ya watu, viwanda na uwekezaji, na ile ya biashara hasa biashara ya utalii.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itachukua hatua zifuatazo:
Itahakikisha mgawanyo wa rasilimali unakuwa wa uwiano baina ya visiwa vyote na mjini na mashamba.

Itahakikisha tafiti mbali mbali za kiuchumi zinafanyika na kuzifanyia kazi ili kutoa maamuzi yanayofaa kwa wakati muwafaka.

Itahakikisha kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi unajali maslahi ya wananchi wanyonge hususan katika haki zao za umiliki wa ardhi, upatikanaji wa maji safi, miundombinu na pembejeo za kilimo, mifugo, ufikiwaji wa barabara bora, nishati, huduma za elimu na afya, na mawasiliano.

Itatumia sera za kibenki (monetary policy) kupunguza mfumuko wa bei ili kujenga ukuaji wa uchumi unaoenda sambamba na maisha mazuri kwa wananchi.

Itatumia sera za kodi (fiscal policy) kukuza uzalishaji wa ndani na kukuza viwanda vidogo vidogo.

4.2. UONDOSHAJI WA UMASKINI
Wastani wa kipato cha Mzanzibari ni dola za kimarekani 650 kwa mwaka. Hivyo Wazanzibari wengi wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku. Kiasi ya asilimia 51 ya wananchi ni maskini wa kupindukia. Maeneo ya mashamba umaskini umekuwa ndio mfumo wa maisha, ndio utamaduni wa nchi na wananchi wanalazimishwa kuukubali na kukaa bure, bila ya kazi, huku maisha yao yakiyoyoma. Wazanzibari wamekuwa hawana vishawishi wala njia za kutumia rasilimali walizo nazo kujiletea maendeleo.

Kutokana na hali hii, tofauti kubwa ya viwango vya maisha ya wananchi kati ya walionacho na wasionacho imezidi kuongezeka katika visiwa vyote viwili, mijini na mashamba. Kisiwa cha Pemba kiko nyuma kwa maendeleo pamoja na kubarikiwa uwezo mkubwa zaidi wa rasilimali ya kilimo na maliasili na kutoa robo tatu ya zao la karafuu.

Kwa muda mrefu huduma muhimu za umma kama maji na umeme zimekuwa zikitolewa kwa mgao hata katika miji mikuu ya Zanzibar. Haishangazi basi kuwa watu wengi wamehama katika maeneo yao ya asili yenye utajiri na rasilimali kwenda Tanzania Bara na kwengineko duniani kutafuta maisha bora. Ni wazi kwamba hii ni hatari kwa uchumi wa nchi yetu.

Maeneo ya mashamba ya Zanzibar yamejikuta yakishindwa kuunganishwa kiuchumi na miji ya Zanzibar na kuwafanya wananchi wake kushindwa kujiendeleza kimaisha na kiuchumi. Fursa ya mikopo ya Benki kwa mwananchi wa kawaida bado ni changamoto kubwa. Mwananchi wa kawaida anashindwa kumudu mikopo ambayo ingetumika kama mtaji wa kuanzisha miradi ya kumuinua kimaisha pamoja na familia yake.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itachukua hatua zifuatazo:
Itatengeneza mpango mpya wa maendeleo endelevu (Zanzibar Sustainable Development Strategy) utakaojali vipaumbele vya maendeleo na huduma za jamii vinavyotokana na mahitaji ya wananchi wenyewe.

Itautilia mkazo mpango mpya wa maendeleo unaojali programu za uzalishaji na uendeshaji zenye ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yaani Public-Private Partnership (PPP).

Itaongoza uwekezaji pamoja na ujenzi wa miundombinu mbalimbali madhubuti na endeleveu ya huduma zote muhimu za kiuchumi na kijamii, kama vile kilimo, mifugo, viwanda, uvuvi, nishati bora na endelevu, maji, mawasiliano, barabara, nakupeleka vitega uchumi sehemu zote za visiwa hivi ndani ya kipindi cha miaka mitano ya uongozi.

Itahakikisha upanuzi wa huduma za jamii na masuala yanayogusa kila mtu kama vile usalama wa chakula, lishe bora, elimu bora inayojali usawa na kutoa fursa kwa wote, Tiba bora na afya ya jamii, makaazi ya kisasa na endelevu, na masoko.

Itasimamia fursa mpya za maendeleo ya sekta ya bahari kuu ikiwemo mashirikiano ya kikanda ya uvuvi wa bahari kuu na uchimbaji wa mafuta na gesi katika bahari.

Itatoa motisha unaohitajika kwa Wazanzibari walioko nje ili walete nyumbani akiba zao pamoja na kuwahakikishia usalama wa mali zao.

Itahakikisha inatoa misaada ya kuwawezesha wavuvi wetu wadogo wadogo kujiongezea uwezo wa kuvua na kuhifadhi samaki ili kuwaongezea kipato.

Itatekeleza ipasavyo sheria iliyopo inayozuia mgeni yeyote kumiliki ardhi humu nchini. Ardhi itabaki rasilimali kuu ya Wazanzibari na itaweza kutumika kama hisa ya mzalendo katika kuingia ubia wa uwekezaji na mtu yeyote. Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itawasaidia Wazanzibari kuhakikisha hawadhulumiwi wala hawaonewi.

4.3. USIMAMIZI WA MAPATO
Kwa muda mrefu, hususan katika kipindi cha miaka ya karibuni, bajeti ya Serikali imeathirika kwa kuwepo nakisi kubwa. Hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi baada ya usawazishaji wa kodi wa 1999. Katika kipindi chote hicho, nakisi imekuwa ikipanda na kushuka bila ya faida yeyote kwa Pato la Taifa (GDP) la Zanzibar.

Nakisi hii kubwa ya kifedha imesababishwa na mfumo dhaifu wa kodi, ubovu wa ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi, misamaha mingi ya kodi na kutojua taratibu za ushuru.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itachukua hatua zifuatazo kurekebisha kasoro hizi:

Katika kurejesha imani katika utaratibu wa bajeti, itaziba mianya yote ya rushwa inayopelekea kupungua kwa ukusanyaji wa mapato wa kiuchumi na huduma za kijamii.

Itaoanisha muundo wa serikali na majukumu yake katika kupunguza gharama kubwa zinazoitia Serikali hasara na kuinyima mapato kwa kupunguza ukubwa wa serikali.

Itajitoa katika shughuli za moja kwa moja za uzalishaji na kuunga mkono programu za Public Private Partnership (PPP).

Itabinafsisha biashara ya karafuu na kuuangalia upya muundo na dhamana za Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC).

Itaweka uwiano mzuri katika mahusiano ya kifedha hasa katika kushawishi mgawanyo mzuri wa gharama na maslahi ya Muungano, ikiwemo thamani ya mapato yanayokosekana Zanzibar kutokana na kusawazishwa kodi ya bidhaa ziingiazo nchini.

Itarekebisha utaratibu wa misamaha ya kodi ili kuepuka utumiaji wake mbaya.

Itapanua mtandao wa kodi na itaimarisha ukusanyaji wa mapato bila ya kuwaathiri wananchi wanyonge wenye kipato cha chini au wafanyabiashara wadogo.

Itadai Zanzibar iongezewe kasma katika mikopo na misaada.

Itazijengea uwezo mamlaka za serikali za mitaa kukusanya kodi katika maeneo yao pamoja na kukasimu madaraka ya matumizi ya maendeleo yao.

4.4. MPANGILIO WA BAJETI
Mwanya mkubwa uliopo baina ya bajeti na mgawanyo halisi wa rasilimali umekuwa ukivuruga mipango ya Wizara na Idara mbali mbali Serikalini. Hii imeathiri sana ufanisi wa shughuli zao. Miradi mingi ya Serikali imekuwa haina matokeo mazuri (positive impact) wala mafanikio kwa jamii yenyewe. Hii inadumaza sana mipango ya muda mrefu ya Serikali.

Usimamizi wa nidhamu ya utekelezaji wa bajeti haupo. Hatupangi bajeti kwa kuzingatia uhalisia wa mapato yetu. Wakuu wa Wizara ya Fedha wanajipa madaraka na mamlaka ya kuamua kiasi gani kiende wapi bila ya kuzingatia bajeti iliyopitishwa. Kitendo cha watawala wa Wizara ya Fedha kujifanya wafalme katika muundo mzima wa matumizi ya fedha katika nchi ni mfano wa matumizi mabaya ya madaraka.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na CUF itahakikisha yafuatayo:
Itautizama upya muundo mzima wa usimamizi, madaraka, na mipango ya bajeti ya Wizara ya Fedha na kuondoa “ufalme” wa madaraka wanaojipa watawala wa Wizara ya Fedha.

Itaangalia upya vipaumbele vya utekelezaji wa bajeti za Serikali kwa mujibu wa malengo ya maendeleo endelevu na vipaumbele vya Zanzibar.

Itadhibiti matumizi holela ya rasilmali na kuhakikisha kuwa kila senti inayopatikana inaelekezwa kunako harakati za ujenzi wa uchumi na maendeleo ya miundombinu pamoja na huduma na usalama wa jamii.

Itatafuta mufaka wa kutafuta njia bora ya mashirikiano na wafadhili (Consultative Group Meetings for Zanzibar) katika misaada ya bajeti kwa malengo makhsusi ya Zanzibar.

4.5. MISHAHARA NA UAJIRI UTUMISHI
Orodha ya malipo ya mishahara na mafao ya wastaafu imejaa wafanyakazi na wastaafu hewa. Pamoja na ufinyu wa mafao yenyewe kumesababisha watu waliofikia umri wa kustaafu kujilazimisha kuendelea na kazi pasina kuwa na uwezo wa uzalishaji na hivyo kukosekana tija.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itachukua hatua zifuatazo kurekebisha kasoro hizi:
Itaondoa wafanyakazi na wastaafu hewa katika orodha ya malipo ya mishahara na mafao.

Italipa mishahara inayokidhi kwa wafanyakazi wa Serikali.

Itanyanyua kiwango cha chini cha mshahara

Itatoa mishahara maalum ya kuvutia kwa wataalamu ili waweze kuja na kubakia kufanya kazi Zanzibar.

4.6. AJIRA KWA VIJANA
Mojawapo ya matatizo makubwa yanayoikabili Zanzibar ni ukosefu wa ajira kwa vijana wake. Wapo vijana wengi ambao wamefaidika na fursa za elimu ya juu kutoka vyuo vikuu vilivyopo Zanzibar na kuhitimu mafunzo ya fani mbali mbali lakini wameshindwa kupata ajira. Kwa upande mwengine, bado kuna wimbi kubwa la vijana ambao hawana elimu rasmi na ambao wamebaki kuzurura mitaani kutokana na kukosa ajira.

Hali hii haiashirii mustakbali mzuri huko tunakoelekea. Ukosefu wa ajira umefikia zaidi ya asilimia 30 ya nguvu kazi yote. Hali halisi huenda ikawa ni mbaya zaidi. Vile vile, Serikali inayoongozwa na CCM imeshindwa kuleta ajira kwa vijana wasio na ajira wanaoongezeka sambamba na kuongezeka umaskini nchini.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itachukua hatua zifuatazo:
Itahakikisha kwamba inatoa ufumbuzi wa kudumu kwa matatizo ya ukosefu wa ajira kwa vijana na wanaomaliza skuli, kuweka mazingira mazuri yatakayovutia uwekezaji katika viwanda, na pia kukuza biashara na utalii wenye tija ili kuchangia vilivyo katika uchumi na upatikanaji wa ajira.

Itaanzisha vyuo maalum vya kutoa elimu ya amali yenye tija na mustakbali mzuri ili kuwawezesha vijana wanaomaliza skuli na wasiokuwa na kazi kuingia katika soko la ajira la ndani na nje.

Itaupitia mtaala wa sekondari, vyuo na vyuo vya amali ili kuenda sambamba na mahitaji ya ajira na kujiajiri.

Itarahisisha mawasiliano kwa kuwawezesha vijana kupata habari za ajira zilizopo na ili vijana waweze kuzifikia.

Itashajiisha na kuvisaidia viwanda vidogo vidogo vidogo kukuza ajira.

Itawalinda vijana kupiga vita unyanyasaji wowote unaotokana na ajira.

Itawatayarisha vijana kitaaluma na mafunzo kuweza kushindana kwenye soka la ajira la kimataifa.

4.7. UWEKEZAJI
Kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2010 (Doing Business in Zanzibar 2010), uwekezaji Zanzibar bado unafanyika katika hali ya mashaka makubwa na vikwazo vingi mno. Kwa mfano, kampuni yeyote inayotaka kuwekeza Zanzibar inabidi ilipe malipo yapatao 48 na jumla ya wastani wa asilimia 40.8% ya faida yake kama kodi. Pamoja na hayo, mwekezaji humbidi atumie masaa 158 kwa mwaka katika taratibu za ulipwaji kodi. Isitoshe, mwekezaji anakumbana na vikwazo vingi vya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mambo ya kodi ya mapato ya mashirika na makampuni, na iliyobaki basi huja kama kodi kutoka sehemu mbali mbali za tozo mfano Bodi ya Mapato Zanzibar, Manispaa, Halmashauri, n.k. Hali hii inatisha
Mfumo wa Sheria unaosimamia vitega uchumi ni wa kukanganya, kugongana kimajukumu na unaopoteza wakati. Kumekuwa na mitafaruku ya kitaasisi katika kufanya kazi moja mfano ZIPA, Wizara za Fedha, Utalii, Uvuvi, Biashara, n.k. Lakini pia katika urasimu wa kutoa huduma kwa mwekezaji katika masuala ya vibali vya ardhi, mazingira, Tawala za Mikoa, Halmashauri, n.k. Wawekezaji wanapata usumbufu mkubwa kwa kupewa ahadi za uongo na kutembea taasisi nyingi pamoja na kutumia gharama kubwa sana katika kupitisha vitega uchumi vyao serikalini.

Hakuna utaratibu wa kupata wawekezaji wenye uzoefu mkubwa watakaoleta tija katika nchi. Pia huduma za kiuchumi na kijami hazijielekezi katika uwekezaji wakati mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo imeweza kukusanya mitaji mikubwa na ya kutosha imeshindwa kufanya uwekezaji wa maana na wa miradi mikubwa itakayoleta tija, kuongeza pato la taifa na kutoa ajira kwa wananchi.

Vivutio vya uwekezaji haviridhishi kutokana na kukosekana kwa huduma muhimu kama za ujenzi wa barabara, upatikanaji wa maji, usimamizi wa mazingira, maji machafu na taka ngumu, pamoja na kasoro mbali mbali zilizopaswa kufanyiwa kazi ili kuvutia uwekezaji mkubwa zaidi. Migogoro isiyokwisha ya ardhi, ugomvi baina ya sekta za utalii baharaini na wavuvi, na mabadiliko ya kidemokrasia ni ya kujilazimisha na hayajengi imani ya wawekezaji. Halikadhalika, upungufu mkubwa wa akiba ya fedha nchini unaathiri uwekezaji wa wazalendo kwa kuwapatia nyenzo na taaluma muhimu ili kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo. Mojawapo ya matatizo makubwa yanayoikabili Zanzibar ni ukosefu wa ajira kwa vijana wake. Wapo vijana wengi ambao wamefaidika na fursa za elimu ya juu kutoka vyuo vikuu vilivyopo Zanzibar na kuhitimu mafunzo ya fani mbali mbali lakini wameshindwa kupata ajira.

Ili Zanzibar iweze kuendelea, hakuna budi kuwepo mazingira muafaka kwa kuvutia uwekezaji. Katika kutimiza lengo hilo, Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itafanya yafuatayo:
Itarekebisha sheria ya uwekezaji iwe bora zaidi na kuimarisha utekelezaji wa kweli uwavutie na kuwaridhisha wawekezaji.
Itaweka mamlaka moja tu ya uwekezaji itakayokuwa na dhamana pekee ya kukuza na kusimamia uwekezaji pamoja na kutoa huduma zote kwa wawekezaji (one stop centre) kwa uwazi na ufanisi mkubwa na isiwe kumhangaisha mwekezaji kama ilivyoelezwa katika tafiti za Benki ya Dunia kuhusu Uwekezaji Zanzibar.

Itaimarisha huduma zote za kiuchumi na kijamii na itawafuata na kuwavutia wawekezaji wazoefu na wenye uwezo mkubwa.

Itaweka vivutio vilivyo bora zaidi (competitive) kwa uwekezaji na vinavyokwenda na wakati.

Itaanzisha utaratibu endelevu wa kutathmini mafanikio na kasoro za sera nzima ya uwekezaji na vitega uchumi na kufanya marekebisho kila inapojitokeza haja ya kufanya hivyo.

Itaangalia uwezekano wa kuwa na sera maalum ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Zanzibar kuwekeza katika miradi mikubwa na endelevu kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali, ajira na tija kwa wanaohifadhi fedha katika mifuko hiyo.

Itasimamia uanzishaji wa Benki ya Uwekezaji (Zanzibar Investment Bank) ambayo itakuwa ikitoa mikopo kwa lengo la kuwainua wawekezaji wa ndani kusudi waweze kuwekeza na kutoa mchango katika pato la taifa na pia kuongeza nafasi za ajira kupitia miradi itakayoanzishwa.

4.8. NGUVU KAZI
Ufanisi na tija ya nguvu kazi ilikuwa ni vigumu kuonekana kutokana na mgogoro wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu, maslahi yasiyoridhisha na ukosefu wa fursa za kujiendeleza. Hakuna maslahi mazuri ambayo yangeivunja nguvu rushwa. Hakuna mpango kazi wa maendeleo unaotekelezwa.

Mchango wa wastaafu katika maendeleo ya nchi hauheshimiwi ipasavyo.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itatekeleza hatua zifuatazo:

Itarekebisha na kutekeleza sheria na taratibu zitazopelekea utumiaji mzuri wa nguvu kazi.

Itarekebisha na kuweka mfumo mzuri wa maslahi kwa wafanyakazi.

Itaunda na kutekeleza mpango unaofaa kwa mafunzo ya kazini na katika taasisi za elimu.

Itasimamia sekta binafsi kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuhakikisha sheria zinazowekwa zinafuatwa.

Mojawapo ya matatizo makubwa yanayoikabili Zanzibar ni ukosefu wa ajira kwa vijana wake. Wapo vijana wengi ambao wamefaidika na fursa za elimu ya juu kutoka vyuo vikuu vilivyopo Zanzibar na kuhitimu mafunzo ya fani mbali mbali lakini wameshindwa kupata ajira.

Ili Zanzibar iweze kuendelea, hakuna budi kuwepo mazingira muafaka kwa kuvutia uwekezaji. Katika kutimiza lengo hilo, Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itafanya yafuatayo:

Itarekebisha sheria ya uwekezaji iwe bora zaidi na kuimarisha utekelezaji wa kweli uwavutie na kuwaridhisha wawekezaji.

Itaweka mamlaka moja tu ya uwekezaji itakayokuwa na dhamana pekee ya kukuza na kusimamia uwekezaji pamoja na kutoa huduma zote kwa wawekezaji (one stop centre) kwa uwazi na ufanisi mkubwa na isiwe kumhangaisha mwekezaji kama ilivyoelezwa katika tafiti za Benki ya Dunia kuhusu Uwekezaji Zanzibar.

Itaimarisha huduma zote za kiuchumi na kijamii na itawafuata na kuwavutia wawekezaji wazoefu na wenye uwezo mkubwa.

Itaweka vivutio vilivyo bora zaidi (competitive) kwa uwekezaji na vinavyokwenda na wakati.

Itaanzisha utaratibu endelevu wa kutathmini mafanikio na kasoro za sera nzima ya uwekezaji na vitega uchumi na kufanya marekebisho kila inapojitokeza haja ya kufanya hivyo.

Itaangalia uwezekano wa kuwa na sera maalum ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Zanzibar kuwekeza katika miradi mikubwa na endelevu kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali, ajira na tija kwa wanaohifadhi fedha katika mifuko hiyo.

Itasimamia uanzishaji wa Benki ya Uwekezaji (Zanzibar Investment Bank) ambayo itakuwa ikitoa mikopo kwa lengo la kuwainua wawekezaji wa ndani kusudi waweze kuwekeza na kutoa mchango katika pato la taifa na pia kuongeza nafasi za ajira kupitia miradi itakayoanzishwa.

4.8. NGUVU KAZI
Ufanisi na tija ya nguvu kazi ilikuwa ni vigumu kuonekana kutokana na mgogoro wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu, maslahi yasiyoridhisha na ukosefu wa fursa za kujiendeleza. Hakuna maslahi mazuri ambayo yangeivunja nguvu rushwa. Hakuna mpango kazi wa maendeleo unaotekelezwa.

Mchango wa wastaafu katika maendeleo ya nchi hauheshimiwi ipasavyo.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itatekeleza hatua zifuatazo:

Itarekebisha na kutekeleza sheria na taratibu zitazopelekea utumiaji mzuri wa nguvu kazi.

Itarekebisha na kuweka mfumo mzuri wa maslahi kwa wafanyakazi.

Itaunda na kutekeleza mpango unaofaa kwa mafunzo ya kazini na katika taasisi za elimu.

Itasimamia sekta binafsi kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuhakikisha sheria zinazowekwa zinafuatwa.

Itaruhusu vyama vya wafanyakazi kuwa huru na haitaviingilia katika utendaji wake wa kazi.

Itaweka utaratibu wa upimaji wa utendaji kazi na kuhakikisha utaratibu wa upandiswaji vyeo makazini utafuatwa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s