Manifesto ya CUF kwa uchaguzi wa 2015

Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015 si uchaguzi wa kawaida kwa Zanzibar. Ni uchaguzi wa kihistoria. Utatupa Wazanzibari fursa ya kihistoria kufanya mabadiliko ya msingi ya jinsi tunavyoongozwa. Ni uchaguzi utakaoamua mwelekeo wa Zanzibar yetu. Advertisements

Tuungane kuijenga Zanzibar Mpya

CCM imeshindwa kulinda uhuru, haki na usalama wetu. Kwa CCM, utawala wa sheria maana yake ni kuzivunja na kuzitumia vibaya sheria. Kwao wao, maana yake ni kutumia sheria kwa upendeleo na kwa mabavu dhidi ya raia wasio na hatia kwa sababu tu wamethubutu kuhoji utawala wao lakini wanasiasa wala rushwa, wababaishaji, waporaji na wauaji wanaendelea…

Tupe nafasi tuibadilishe Tanzania

Kuwepo kwa maendeleo au kukosekana kwake kuna uhusiano wa moja kwa moja na hali ya uchumi wa nchi. Kutokana na uhusiano huu ni dhahiri kuwa anayehitaji maendeleo hana budi kuwapa wataalamu wa uchumi nafasi kubwa kabisa katika kubuni, kupanga, kurekebisha, na kuratibu sera za kiuchumi. Pili, amani na utulivu haviwezi kushamiri katika mazingira ambayo haki…

Nafasi pekee ya kuleta mabadiliko Zanzibar

Mtazamo wetu ni kwamba Wazanzibari tutakuwa na nguvu na sauti licha ya udogo wetu ikiwa tutakuwa na mfumo shirikishi baada ya tenganishi na kwamba tunaweza kuyafikia, kwa umoja wetu, mengi ambayo hatukuweza kuyafikia kwa kugawanyika kwetu. Ni CUF pekee kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoweza kuyaleta haya. Maridhiano yetu na mafahamiano yetu juu ya…

Mtanzania zinduka, mabadiliko yanawezekana

Ufisadi na rushwa zinaendelea kuimarika nchini na CCM imegawika mapande mapande. Watanzania tutajuta ikiwa tutaruhusu wizi wa kura na kuipa fursa CCM kuendelea kutawala. CCM haina dira ya kuongoza nchi na kusimamia utawala bora. Imeshindwa kutumia utajiri mkubwa tulionao wa raslimali na maliasili ya Taifa kwa manufaa ya wananchi wote na badala yake leo Tanzania…

Tutaijenga Zanzibar Mpya – Maalim Seif

Kwa hakika, nataka kutumia fursa hii kutoa wito hasa kwa wananchi wote wa Zanzibar, walio CUF, CCM, wa vyama vyengine na wasio wafuasi wa chama chochote, wote kwa ujumla wao wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 31 Julai, na wapige kura ya NDIO ili kwa pamoja tuijenge Zanzibar Mpya; Zanzibar shirikishi na siyo Zanzibar tenganishi;…