CUF njiani kupata mwenyekiti mpya

BAADA ya Profesa Ibrahim Lipumba kuchukua uamuzi wa ghafla wa kujiuzulu uenyekiti wa CUF jana, vikao muhimu vya dharura vimeanza kwa lengo la kujaza nafasi hiyo. Anaandika Jabir Idrissa. Profesa Lipumba ambaye baada ya kuzongwa na Wazee wa Chama asichukue uamuzi huo sasa, jana asubuhi alikimbilia Hoteli ya Peacok, katikati ya jiji la Dar es…

Kwaheri Prof. Lipumba

Hakuna neno jingine linalofaa kuelezea hali ilivyo ndani ya Ukawa zaidi ya “mtikisiko” baada ya Profesa Ibrahim Lipumba kuamua kujivua uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) wakati mkakati wa vyama vya upinzani kushirikiana kutaka kushika dola ukiwa umeshika kasi. Uamuzi wa Profesa Lipumba, mmoja wa waasisi wanne wa Ukawa-Umoja wa Katiba ya Wananchi unaoundwa na…

“CUF iko imara, inasonga mbele”

Katika historia yake, CUF imepita katika dhoruba na misukosuko mingi lakini mara zote kimeonesha uwezo mkubwa wa kuhimili dhoruba na misukosuko hiyo na kukabiliana na athari zake. Hatuna chembe ya wasiwasi kwamba hata mtihani huu tutauvuka na tunaamini tutaibuka tukiwa Chama imara zaidi.

CUF kuigeuza Z’bar kituo kikuu cha biashara

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa visiwa vya fursa za biashara na ajira kwa wananchi. Maalim Seif ambaye tayari Chama chake kimeshamteua rasmi kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, ameeleza hayo katika viwanja vya…

Maalim Seif ‘kidedea’, kuwania urais Zanzibar

Chama cha Wananchi CUF kimempitisha katibu mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa mara ya tano. Pia, CUF imewarudisha baadhi ya wagombea wa nafasi za ubunge na uwakilishi walioanguka katika kura za maoni za majimboni. Maalim Seif amepitishwa na CUF kuwania nafasi hiyo kwa mara tano tangu kurejeshwa kwa mfumo…

CUF yapuliza kipenga urais wa Zanzibar

Chama cha Wananchi (CUF) kimepuliza kipenga cha urais kwa upande wa Zanzibar, kwa kuwataka wanachama wake wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kuteuliwa kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kuanzia leo. Kadhalika, CUF kimesema wamekubaliana na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa mgombea wa urais Zanzibar atatoka chama hicho. Aidha, pia Jimbo la Kikwajuni…

Vigogo CUF waanguka ubunge

MATOKEO ya awali ya kura za maoni kwa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaowania Ubunge na Uwakilishi yameanza kutoka huku majina mapya yakichomoza kwa kupata ushindi dhidi ya wabunge wanaotetea nafasi zao. Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyopatikana mjini Unguja jana, Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF), amebwagwa katika kura za maoni…