Wizi TTCL unatisha -Mnyaa

UOZO na ufisadi ulioigubika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) uliwekwa hadharani bungeni mjini Dodoma jana. Hayo yalielezwa katika hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia. Alisema utata katika umiliki na ukodishaji wa hisa za serikali, mikataba mibovu, madeni na baadhi ya vitu vilivyochangia kampuni hiyo kufilisika. Akisoma maoni hayo,…

CUF yaibua mapya sakata la Escrow

Kashfa ya Escrow imeibuliwa upya bungeni baada ya wabunge kudai kuna kampuni ya Simba Trust inayomiliki asilimia 50 za kampuni ya Pan Africa Power (PAP), ambayo inadaiwa kuhusika katika ufisadi wa uchotwaji wa zaidi ya Sh.bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow. Hayo yaliibuliwa jana bungeni na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa kuwasilisha…

‘Serikali ya Muungano haiheshimu Mkataba wa Muungano’

“Kamati ya Makamu wa Rais haina uhalali wa kisheria. Katiba yetu haisemi popote kwamba chombo hiki kipo na kwamba kina nguvu gani. Ni chombo cha ushauri tu ambacho ufanyaji kazi na mafanikio yake yanategemea zaidi dhamira njema. Na, kama tulivyosema kwenye hotuba yetu ya mwaka juzi, dhamira hiyo njema haionekani kuwepo, hasa hasa kwa upande…

CCM inaimasikinisha Tanzania

Kigezo kilichokubaliwa kimataifa kuwa matumizi ya chini kabisa kwa mtu mzima asihesabiwe kuwa ni maskini wa kutupwa ni dola moja kwa siku. Benki ya dunia inakadiria kwa kutumia kipimo hiki, umaskini Tanzania umeongezeka toka asilimia 73 ya Watanzania wote mwaka 1990 mpaka kufikia asilimia 89 mwaka 2000. Kwa kutumia kigezo hiki cha kimataifa na takwimu…

Upinzani waonesha njia

Kambi ya Upinzani inaona kuwa kwa ajili ya kutoa motisha zaidi kwa wafanyabiashara kusafirisha korosho ambazo tayari zimebanguliwa na hivyo kuongeza thamani ya bidhaa tunazouza nje na pia kutoa ajira kadhaa kwa wananchi ni bora wangepewa unafuu kadhaa katika kodi za ndani. Kwani ushuru wa usafirishaji wa korosho ghafi nje wa kulipa USD 160 kwa…

“Bila nishati mbadala, uhifadhi wa mazingira ni ndoto”

“Bila maji hakuna maisha na ili maji yapatikane lazima vyanzo hivyo vya maji vilindwe . Bado tafsiri ya chanzo cha maji kina utata kisheria, kwa kuangalia Sheria ya mwaka 2002 na Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004. Sheria zote hizi zina vipengele vya utunzaji au kuhifadhi vyanzo vya maji. Sheria ya maji hairuhusu kufanyika shughuli…

“Serikali ya Muungano haisikilizi”

Sisi wa Kambi ya Upinzani tunaamini kwamba ni kosa kubwa dhidi ya sheria zinazolinda mikataba ya kimataifa na, kwa hakika, ni hatua ya hatari kwa khatima njema ya Muungano huu, kwa ofisi za waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ambayo Zanzibar ni sehemu yake) na Waziri Kiongozi (ambayo ni ya Zanzibar tu kama…

MKUKUTA hautekelezeki

Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini unalenga kufanikisha kufikia malengo ya milenia. Hata hivyo utekelezaji wa MKUKUTA umesuasua kwa sababu gharama za mkakati hazikukadirwa mapema. Ukadiriaji wa gharama za MKUKUTA katika baadhi ya sekta muhimu ulikamilika mwishoni wa mwaka 2006 na gharama zake zikabainika kuwa ni kubwa mno kuliko uwezo wa serikali kwa hiyo…