Manifesto ya CUF kwa uchaguzi wa 2015

Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015 si uchaguzi wa kawaida kwa Zanzibar. Ni uchaguzi wa kihistoria. Utatupa Wazanzibari fursa ya kihistoria kufanya mabadiliko ya msingi ya jinsi tunavyoongozwa. Ni uchaguzi utakaoamua mwelekeo wa Zanzibar yetu.

Screen Shot 2015-09-27 at 15.00.02Ndiyo maana tunasema huu si mwaka wa uchaguzi; bali ni mwaka wa maamuzi. Tarehe 25 Oktoba, 2015 Wazanzibari tutakuwa na chaguo la wazi la kuamua iwapo tunataka Zanzibar iendelee na mkwamo huu ulioletwa na uongozi usio na dira na sera zisizo na mwelekeo za Chama Cha Mapinduzi au tunataka mabadiliko yatayotuletea Zanzibar Mpya inayoangaza mbele kwenye maendeleo ya haraka na ukuaji wa kasi wa uchumi wetu na huduma za jamii.

Mimi naamini sote tumechoka na mkwamo huu. Wazanzibari kwa maumbile yetu kama wananchi wa nchi ya kisiwa ni watu tunaopenda kujituma na kutumia fursa
zilizopo katika mazingira ya nchi za kisiwa kujiletea maendeleo na kubadilisha maisha yetu.

Binafsi kama mtu mliyeniamini kuwa kiongozi wenu natambua uwezo huo tulio nao na naamini sasa wakati wa kuutumia kikamilifukwamanufaa ya nchi yetu na watu wake umefika.

Tunachohitaji ni uongozi makini, wenye dira na unaowajibika na sera bora zilizotungwa Zanzibar kwa ajili ya Zanzibar. CUF inakupa fursa hizo.Mwaka 2010 tulifanya maamuzi sahihi ya kuanzisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kuchoshwa na migogoro ya kisiasa iliyodumu visiwani mwetu kwa zaidi ya miaka 50 sasa.

Kinachohitajika sasa ni kuipatia Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa uongozi unaojiamini na unaojituma ili kuwaletea Wazanzibari maendeleo waliyoyatarajia. CUF tumejiandaa kuwapa Wazanzibari uongozi huo.

Katika kurasa za Ilani ya Uchaguzi hii mtaona ni kiasi gani tumejiandaa kukutimizia hayo. Tupe ridhaa yako na kwa pamoja tuijenge Zanzibar Mpya yenye Mamlaka Kamili na Neema kwa Wote.

Twende Pamoja.

Seif Sharif Hamad

Soma Manifesto ya CUF kwa Uchaguzi wa 2015

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s