Lowassa: Wameisoma namba

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayewakilisha vyama vinavyounda Ukawa, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsindikiza wakati akienda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ni salamu kwa CCM na ‘wameisoma namba’ kwamba Watanzania wanataka mabadiliko.

UKAWA tutashinda uchaguzi – Lowassa

Mkutano Mkuu wa Chadema, kwa kauli moja, umempitisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, papo hapo mwanasiasa huyo akasema Chadema itachukua nchi asubuhi. Lowassa alipitishwa kuwania urais kwa mwavuli wa Ukawa kwa kuungwa mkono na vyama vyote katika “safari ya uhakika”. Mbunge huyo wa…

Seif: Ilikuwa kazi kumshawishi Duni Haji

Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema ilikuwa kazi kubwa kumshawishi Juma Duni Haji kukiacha chama hicho na kujiunga Chadema ili awe mgombea mwenza wa Edward Lowassa. Duni, ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF, alitangazwa kujiunga na Chadema jana, ikiwa ni makubaliano ya mkakati maalumu wa…

Juma Duni mgombea mwenza wa Chadema

Mwanasiasa machachari wa upinzani kutoka Zanzibar, Juma Duni Haji ameteuliwa kuwa mgombea mwenza wa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa kupitia Chadema. Uteuzi wa Juma Duni Haji umefanyika mara tu baada ya mwanasiasa huyo kukihama Chama cha Wananchi (CUF) ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya…

“Safari ya Mabadiliko” yaanza upya na haizuliki

Hakuna anayeweza kukanusha kuwa sasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaingia kwenye kipindi cha kisiasa ambacho haijawahi kuingiapo tangu kuasisiwa kwake mwaka 1964. Ni hapo jana tu ambapo vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa limechukua sura mpya katika nchi yetu ya Tanzania kwa kushuhudia aliyekuwa waziri mkuu na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akiteuliwa rasmi kupeperusha…

CCM yajitapikia, yajipaka, yameza

“Sitapiki nikameza” ni msemo mashuhuri sana katika jamii zetu, ambao mtu huutumia akimaanisha kuwa kamwe hatorudia jambo au kitu ambacho ameshaachana nacho. Kwa bahati mbaya sana, msemo huu ni tofauti na mtazamo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani wao sio tu hujitapikia, bali pia hujipaka matapishi hayo kabla hawajaanza tena kuyameza. Uchafu ulioje! Tukumbushane kidogo.…

Lowassa mguu kwa mguu hadi Ikulu

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ameanza hatua nyengine kwenye kile kilichopewa jina la “Safari ya Matumaini” katika azma yake ya kuwania nafasi ya juu ya uongozi wa nchi kwa kuchukua rasmi fomu ya kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hapo jana.…

Lowassa afunua ukweli wa Richmond

Hatimaye ameingia Chadema. Ilianza kama uvumi lakini jana ilikuwa dhahiri baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kutangaza rasmi kukihama chama tawala, CCM na kujiunga na Ukawa kupitia Chadema, huku akisisitiza; “Sasa basi, imetosha.” Baada ya kukabidhiwa kadi ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Lowassa alisema amejiunga na chama hicho kikuu…