Lowassa mguu kwa mguu hadi Ikulu

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ameanza hatua nyengine kwenye kile kilichopewa jina la “Safari ya Matumaini” katika azma yake ya kuwania nafasi ya juu ya uongozi wa nchi kwa kuchukua rasmi fomu ya kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hapo jana.

Mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa, akikaribishwa na mashabiki wake kwenda kuchukuwa fomu.

Mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa, akikaribishwa na mashabiki wake kwenda kuchukuwa fomu.

Akizugumza mara baada ya kupokea fomu ya kuwania kiti hicho katika makao makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, Lowassa amesema kamwe hatoyumbishwa na wale wanaokosoa uamuzi wake wa kujiunga na chama hicho.

“Wachambuzi wa mambo wanaonishambulia kwa kuwa nimejiunga na Chadema, ni mlafi wa madaraka, wanapoteza muda na hawatoniyumbisha. Mimi ningependa kuwaambia natekeleza maelekezo ya Baba wa Taifa, Marehemu Julius Nyerere aliposema kuwa Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Mimi nimeridhika kuwa ndani ya CCM mabadiliko hayo hayawezi kupatikana.”

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alisema kuwa tarehe 3 au 4 Agosti, mkutano mkuu na ule wa Baraza Kuu utaitishwa ili kupata jina la mgombea urais na mgombea mwenza watakaopeperusha bendera ya chama hicho.

Aidha amesema mkutano mkuu huo utapitisha ilani ya Chama itakayotumiwa na CHADEMA na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Naye Mwanasheria mkuu wa chama hicho Tundu Lissu  amesema utaratibu uliotumika kumpata Lowassa uliwashirikisha mwenyekiti wa taifa, katibu mkuu, makamu wenyeviti wote wawili wa chama, manaibu makatibu wakuu wote wawili, na wajumbe wote wa kamati kuu ya chama.

Lowassa amejiunga na chadema hapo juzi kufuatia hatua ya kuenguliwa jina lake katika kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwanzoni mwa mwezi Julai kwenye hatua ya awali jijini Dodoma.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s