CUF Michango

Usiache kukichangia Chama

Chama kinahitaji Mchango wako kifedha ili kiweze kusonga mbele, unaweza kuchangia kwa kutumia sim yako ya kiganjani kwa njia ya ujumbe mfupi wenye neno “CHANGIA” kwenda kwenye namba 15338, na utatozwa kiasi cha TZS 300/=

Bangalore iko tayari kuisaidia Zanzibar

  • Kuharakisha maendeleo ya elimu, viwanda na ITC

    Waziri Kiongozi wa serikali ya Karnataka nchini India, DV sadananda Gowda, amesema serikali yake iko tayari kutiliana saini na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya makubaliano ya mashirikiano katika Nyanja za elimu, viwanda na teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT).   Soma zaidi hapa 

TUJIAMINI TULETE MABADILIKO

KATIBU MKUU, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD

KATIBU MKUU, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD

“Inaeleweka na sote kwamba katika kipindi kisichozidi miaka miwili kuanzia sasa, tutaingia katika harakati za uchaguzi wa Serikali za mitaa hapo 2009 na uchaguzi mkuu wa taifa hapo 2010. Tukizingatia ukubwa wa nchi yetu, hali mbaya ya barabara na miundo mbinu mengine, ukosefu wa uhuru wa vyombo vya habari unaofika kwa wananchi vijijini, mfumo usioaminika wa kuendesha uchaguzi, miaka miwili si muda mkubwa kujitayarisha kwa chaguzi hizo. Maandalizi ya chaguzi yanahusisha, pamoja na mengine, kuwatayarisha mawakala wa kusimamia uchaguzi huo, kununua vifaa vya uchaguzi pamoja na magari ya kampeni.” Ombi la Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kuichangia CUF…

KWA NINI UICHANGIE CUF

MWENYEKITI WA CUF, PROF. IBRAHIM LIPUMBA

MWENYEKITI WA CUF, PROF. IBRAHIM LIPUMBA

“Hivyo kazi ya CUF na wewe unayechangia ni kujenga chama imara kilicho bora, chenye kuwatetea watu, chenye matumaini mapya kwa ajili ya Watanzania wa leo na wa kesho. Wakati tunafahamu kwamba kuchangia ni jambo gumu, lakini tunaamini kwamba kutoa ni moyo na si utajiri. Ugumu wa kazi hii haulingani na umuhimu wa kuifanikisha. Hivi ni vita ambavyo CUF na wewe – kwa pamoja – lazima tushinde. Tusishindwe maana tukishindwa leo, tutakuwa tumeshindwa 2009, 2010 na tutakuwa, kwa hinyo, tumeshindwa milele kumkomboa Mtanzania kutoka maisha haya mabaya, magumu na ya kidhalilifu.” Hoja na haja ya kuichangia CUF…

VIPI UTAICHANGIA CUF

SALUM MANDARI, NAIBU MKURUGENZI WA FEDHA NA UCHUMI

SALUM MANDARI, NAIBU MKURUGENZI WA FEDHA NA UCHUMI

“Ili kukabiliana na matukio hayo tusiyoyategemea na kufanikisha matayarisho ya chaguzi, CUF inahitajia shilingi za Kitanzania bilioni 8.4 (sawa na dola milioni 7 za Kimarekani). Kima hiki ni kikubwa kwa chama pekee kukipata, ndio maana CUF inahitaji msaada wa kila mpenda mabadiliko ya kidemokrasia, haki na maendeleo ya nchi yetu.” Njia za kuichangia CUF…

JIKUMBUSHE USALITI WA CCM KWA WATANZANIA

UMASIKINI HUU WA WATANZANIA UNASABABISHWA NA CCM

UMASIKINI HUU WA WATANZANIA UNASABABISHWA NA CCM

“Jikumbushe kuwa mababu zetu walidai uhuru wa aina ya kwanza. Uhuru wa kuwaondoa wakoloni (wageni) wasituamulie maendeleo yetu na ya nchi yetu. Kazi hii ilifanywa na Julius Mwalimu Nyerere na Mzee Abeid Karume. Tunawapongeza. Uhuru huu ni uhuru wa kuwa huru (freedom for self-determination). Baada ya hapo tuliutafuta uhuru wa aina ya pili – uhuru wa kujikusanya na kutoa mawazo yetu (freedom of assembly and expression).” Sababu za kuikataa CCM na kuiunga mkono CUF…

Tafadhali tutumie maoni yako. Usisahau kuandika mada ya kile unachokitolea maoni.

(c) 2008, Kurugenzi ya Haki za Binaadamu na Mahusiano ya Umma, CUF

Advertisements