CUF Manifesto 2010

A Vision for Change

“Watanzania wameweka matumaini yao kwa Chama cha CUF na misingi yake ya sera ya kuleta “Haki sawa kwa wananchi wote” na “Kujenga uchumi imara unaoongeza ajira na utakaoleta neema na tija kwa wote.” Chama chetu kimekuwa ni Chama kikuu cha upinzani nchini kwa muda mrefu sasa na wananchi wanaendelea kuteseka kwa kuona matatizo yao yakizidi kuongezeka bila kuchukuliwa kwa hatua za msingi kushughulikia matatizo yao. Hali hii inawafanya wananchi wengi hasa vijana na wanawake kuwa katika shauku kubwa ya kuona utawala wa nchi yetu unabadilishwa kwa amani kupitia karatasi za kura. CUF kwa kutambua nafasi yake katika kuyaongoza Mabadiliko yanayohitajika, kikiwa siyo tu chama kikuu cha upinzani hapa nchini bali pia kutokana na mjengeko wake wa kuwa kweli ni chama cha kitaifa chenye kukubalika na chenye mtandao mpana katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano, imezindua DIRA YA MABADILIKO – VISION FOR CHANGE. Dira ya Mabadiliko ndiyo msingi wa ILANI yetu ya uchaguzi. Vision for Change chini ya Serikali ya CUF itatujengea Tanzania Mpya inayojali haki sawa kwa wananchi wote na itakayojenga uchumi imara unaoongeza ajira na utakaoleta neema na tija kwa wote.” Endelea kusoma waraka wa Prof. Ibrahim Lipumba kwa Watanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010

Kwa kuisoma Manifesto yetu ya Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa mwaka 2010, bonyeza hapa.

NAFASI PEKEE YA KULETA MABADILIKO ZANZIBAR

“Mtazamo wetu ni kwamba Wazanzibari tutakuwa na nguvu na sauti licha ya udogo wetu ikiwa tutakuwa na mfumo shirikishi baada ya tenganishi na kwamba tunaweza kuyafikia, kwa umoja wetu, mengi ambayo hatukuweza kuyafikia kwa kugawanyika kwetu. Ni CUF pekee kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoweza kuyaleta haya. Maridhiano yetu na mafahamiano yetu juu ya malengo na dhamira zetu ni kuamini kwamba tunaweza kuingiza shauku na hamu mpya katika utungaji wa sera bora zenye nia ya kuleta mabadiliko ya haraka na ya maana yenye tija na neema kwa wananchi wote. Changamoto pekee itakayobaki itakuwa ni kusimamia na kufuatilia utekelezaji wake. Ni CUF kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa pekee inayoweza kuyaleta haya.” Endelea kusoma waraka wa Maalim Seif kwa Wazanzibari kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.Kuisoma Manifesto yetu kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa 2010, tafadhali bonyeza hapa

Kutembelea mtandao wa mgombea wetu wa Urais wa Zanzibar na kuchangia kampeni zetu, tafadhali bonyeza hapa

PROF. IBRAHIM HARUNA LIPUMBA

PROF. IBRAHIM HARUNA LIPUMBA

‘TUNAKUOMBA UTUPE MAMLAKA YA KUKUTUMIKIA, NASI TUNACHUKUA DHAMANA YA KUTUMIKA’

“Kwa mara nyingine tena ifikapo Oktoba 2005 wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tutapiga Kura kuchagua Rais, Wabunge, na Madiwani wa nchi yetu. Huu utakuwa ni Uchaguzi Mkuu wa tatu chini ya mfumo wa vyama vingi ambapo kila Mtanzania mwenye sifa ya Kupiga Kura, na aliyejiandikisha atakuwa na wajibu wa kumchagua yule anayedhani anamfaa. Chaguzi kuu mbili zilizotangulia, yaani ule wa kwanza uliofanyika Oktoba 1995 na wa pili uliofanyika Oktoba 2000 zimetupa uzoefu wa kutosha juu ya nini cha kutarajia kutoka kwa viongozi, makada, wanachama, washabiki, na mawakala wa CCM waliopandikizwa katika vyombo mbalimbali vya umma. Kwa kifupi chaguzi hizi zimetufunza kutarajia wizi wa Kura, Rushwa, Vitisho, Ghilba na Ulaghai wa kila aina kutoka kwa CCM na mapandikizi wake ndani ya vyombo vya dola.“ Endelea kusoma waraka wa Prof. Ibrahim Lipumba kwa wapiga kura wa Tanzania kwa uchaguzi mkuu wa 2005

Bonyeza hapa kusoma Ajenda ya CUF kwa maendeleo ya Tanzania 2005

AJENDA YA CUF KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR

AJENDA YA CUF KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR

‘HII NDIYO NAFASI PEKEE YA KUILETEA MABADILIKO ZANZIBAR’

“Jumapili ya Oktoba 30, 2005 tutapiga kura kwa mara nyengine tena kuchagua Serikali itakayotuongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Wengi wenu mtakao kuwa mnapiga kura siku hiyo, hamkuwahi kushuhudia kitu kingine zaidi ya serikali ya CCM. Nyote mmeshuhudia kibri cha utawala ambao umekulia huku ukiamini kuwa kutawala ni haki yao tu na kwamba maslahi ya umma maana yake ni maslahi yao wao. CCM imepoteza uhalali wa kuongoza. Kuichagua CUF ni nafasi pekee ya mabadiliko ya kweli. CCM imajiweka mbali na dhana ya uongozi wa heshima uadilifu na kusahau kwamba uongozi ni dhamana. Kwa miongo na miaka kadhaa sasa imekuwa ikisaliti imani na kudharau heshima iliyopewa na wananchi wa Zanzibar.” Endelea kusoma waraka wa Maalim Seif kwa wapiga kura wa Zanzibar kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005

Bonyeza hapa kusoma Ajenda ya CUF kwa maendeleo ya Zanzibar 2005

Tafadhali tutumie maoni yako. Usisahau kuandika mada ya kile unachokitolea maoni.

(c) 2008, Kurugenzi ya Haki za Binaadamu na Mahusiano ya Umma, CUF

Advertisements