CUF SUK Zanzibar

Wapendwa Watembeleaji wa Weblog yetu,

Kufuatia maendeleo mapya katika siasa za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, ambayo yanahusiana na uamuzi wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi kubadilisha uamuzi wake wa kutokumtambua Mhe. Amani Karume kama rais halali wa Zanzibar, ukurasa huu mpya umeanzishwa kwa lengo la kutoa fursa kwenu kupata habari na kutoa maoni yenu. Karibuni sana!

ZANZIBAR DAIMA, YASEMA RISALA YA WANAWAKE WA CUF

Sasa, tunachokitaka sisi wanawake wa Zanzibar ni nchi yetu tu. Zanzibar hii ambayo kwa miaka 50 sasa imekuwa ikichinjwa na kukatwa vipande vipande, tuna jukumu leo hii la kuikusanyakusanya na kuileta pamoja. Na tafauti wanavyosema watu kwamba La Kuvunda Halina Ubani, Zanzibar yetu haijavunda. Bado inawezekana kuiunda tena, ikasimama kuchukua nafasi yake iliyokuwa imeshikilia kwa karne kadhaa huko nyuma, yaani kitovu cha elimu, ustaarabu na maendeleo. Na kama alivyokuwa akinadi kampeni zake Barack Obama, ambaye hata babu yake Bwana Onyango Hussein Obama, alipitia Zanzibar na kufaidika na ustaarabu wa watu wa nchi hii, YES WE CAN! Ndiyo, na sisi Wazanzibari tunaweza, na lazima tuweze. Endelea kusoma risala hii

DK. KARUME: HAKUNA MASHARTI TULIYOWEKEANA NA SEIF

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume, amesema hakuna masharti waliyowekea na Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, walipokutaka hivi karibuni, Ikulu ya Zanzibar. Amesema hakuna masharti isipokuwa sharti lao kubwa ni kusameheana na kusahau yalitopita kwa kurejesha udugu katika kudumisha utulivu na amani kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ya wananchi wa Zanzibar. Endelea kusoma

MAALIM SEIF AMSINDIKIZA KARUME KUPOKEA SHAHADA

UHUSIANO kati ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Dk Amani Karume na Chama cha Wananchi (CUF), unaonekana kuendelea kuimarika baada ya viongozi wa chama hicho jana kumsindikiza rais huyo katika hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu Maalim Seif jana walimsindikiza Karume katika kutunukiwa shahada hiyo iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki. Endelea kusoma

MAANDAMANO KUUNGA MKONO SEIF, KARUME

SIKU chache baada ya wafuasi wa Chama Cha Wananchi (CUF) kutaka kumshambulia Katibu Mkuu wao, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kukubali kumtambua Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, jumuiya za chama hicho zimetangaza kuunga mkono hatua inayoashiria muafaka mpya. Wakati Jumuiya ya Wanawake wa chama hicho (UWCUF) Zanzibar imeandaa maandamano ya kuunga mkono mazungumzo hayo, ile ya vijana imempongeza Maalim Seif kwa hatua hiyo. Endelea kusoma

RAIS KARUME, HAMAD WAMKUNA JK

Rais Jakaya Kikwete amempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ)Amani Abeid Karume, na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad kwa kukaa kuzungumza kuondoa tofauti zao. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwandishi wa habari wa rais, Msaidizi, Premi Kibanga, mbali na kufurahishwa kwa hatua hiyo, Rais Kikwete amewahakikishia viongozi hao ushirikiano wake na wa Serikali. Endelea kusoma

KIKWETE ELATED OVER SITUATION IN ZANZIBAR

President Jakaya Kikwete yesterday commended Zanzibar President Amani Abeid Karume and Civic United Front (CUF) Secretary General Seif Shariff Hamad for holding landmark talks at the Isles’ State House. A statement issued in Dar es Salaam by the Directorate of Presidential Communications said the president was impressed with the decision by the opposition party to recognize Karume as legitimate President of Zanzibar after years of bad blood between it and the ruling CCM linked to general election results. Read more

KIKWETE APPLAUDS CUF’S NEW STANCE ON KARUME

PRESIDENT Jakaya Kikwete has commended Zanzibar President Amani Abeid Karume and Civic United Front (CUF) Secretary General, Mr Seif Sharif Hamad, for their recent meeting that shed more light in resolution of protracted political tension in the Isles. The Directorate of Presidential Communication said in a statement yesterday that President Kikwete, specifically hailed CUF for recognising President Karume and his government as legitimate authorities elected into office in October 2005. Read more

OPTIMISM PERMEATES ZANZIBAR POLITICS AFTER CUF’S RECOGNITION OF KARUME

ZANZIBAR President Amani Abeid Karume has said his recent talks with the Civic United Front Secretary General, Seif Sharrif Hamad, have opened a new chapter in Zanzibar. Mr Karume said following the discussion, conflicts should not be entertained any more and must be replaced by hard work and commitment to develop the islands. “Zanzibar has a long history of observing peace and stability as inherited from our grandparents. Therefore, there is a strong need to maintain it” President Karume said in a statement released by the State House here yesterday. Read more

CUF DEFENDS DECISION TO RECOGNISE PRESIDENT KARUME

THE opposition Civic United Front (CUF) said today that there was no need for endless Muafaka talks as only positive actions and bold decisions would resolve the political impasse in Zanzibar. The party has also urged its members to support their leaders following their decision to recognise Mr Amani Abeid Karume as a legitimate President of Zanzibar, saying the move was the first major step towards finding a lasting solution to the Isles political stalemate. “It is no surprise that people reacted the way they did on Saturday. Read more

US STATEMENT ON ZANZIBAR

We welcome the news that the Zanzibar leaders of the isles ’ two major political parties have met to discuss “the need to maintain peace and harmony as well as understanding and cooperation among all Zanzibaris.” We have long called for Zanzibar’s leaders to champion peaceful, constructive and fair politics so that no Zanzibari feels permanently excluded from having a voice in government and no Zanzibari need fear political reprisal. We hope that Zanzibar’s leaders will follow up this meeting with concrete measures to establish a healthy political climate in Zanzibar that promotes good governance and economic development for all. A first step would be for leaders to instruct their supporters to desist from violence. We share the vision of the two leaders that if Zanzibar can overcome its several decades of bitter political divisions, then the creative, dynamic and entrepreneurial spirit of the Zanzibari people will be unleashed for the benefit of all Zanzibaris, their fellow Tanzanians and indeed all of East Africa and beyond. Zanzibar has made significant contributions to world culture. It is time for Zanzibaris once again to show the world what they can achieve.

CUF YAFANYA MAAMUZI MAZITO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ameponea chupuchupu kupigwa na wafuasi wa chama hicho, baada ya kutangaza rasmi kumtambua Rais Amani Abeid Karume. Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibandamaiti alisema kwamba Baraza Kuu la Uongozi limekutana na kupitisha uvamuzi wa kumtambua rasmi Rais Karume, ili kutafuta muafaka wa kumaliza mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar. Endelea kusoma

SERIKALI YA MSETO YANUKIA ZANZIBAR

MAPATANO ya ghafla kati ya Rais wa Zanzibar, Aman Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, yakihusisha kumtambua rasmi Karume, na Hamad kudai hatua hiyo inafungua makubwa zaidi, ni hatua za awali kuandaa serikali ya mseto, Raia Mwema imeelezwa. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka vyama vya CCM na CUF, serikali ya mseto itaundwa ikiwa ni moja ya mkakati wa vyombo vya usalama kujipatia fursa ya kubaini kasoro na namna ya kuzifanyia kazi kwa kipindi hiki cha miezi kadhaa kabla ya Uchaguzi Mkuu, mwakani. Endelea kusoma

PEACE MOVE ‘NOT A CCM INITIATIVE’

Chama Cha Mapinduzi (CCM) leaders, especially those from the Mainland, have been asked to keep off the reconciliation process initiated by Zanzibaris. Civic United Front (CUF) director of foreign affairs Ismail Jussa told The Citizen yesterday that CCM leaders should remain on the sidelines “because they don’t know what is going. He said the likes of CCM secretary general Yusuf Makamba, publicity secretary John Chiligati and propagandist Kingunge Ngombale-Mwiru should let Zanzibari leaders conclude the reconciliation process “without interference”. Read more

WHAT ARE KARUME AND SEIF UP TO IN ZANZIBAR?

Leaders from across the political divide in Zanzibar have joined forces to counter what they see as Tanzania Mainland’s undue influence in the isles, sources within the ruling CCM and opposition CUF told The Citizen yesterday. The newfound camaraderie between President Amani Abeid Karume of CCM and his longtime political rival, Mr Seif Shariff Hamad of CUF, is said to be the outcome of behind-the-scenes efforts to chart a more independent future for Zanzibar. Read more

KARUME AMKUBALI MAALIM SEIF

WANANCHI wa Zanzibar wametakiwa kuyapokea kwa wema na faraja mazungumzo kati ya Rais Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, ili kuimarisha amani, utulivu na umoja. Mwito huo ulitolewa jana na Rais Karume alipokutana na kuzungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini anayemaliza muda wake, Sindiso Mfenyana, aliyekwenda kumuaga Rais Ikulu mjini hapa. Endelea kusoma

KARUME: LET`S FOCUS ON BUILDING OUR NATION

Zanzibar President Amani Abeid Karume yesterday called upon Zanzibaris to refrain from disputes and instead concentrate on nation-building activities, including initiatives aimed at promoting unity and boosting the economy. “There is no reason for people of Zanzibar to continue orchestrating conflicts instead of working on development issues and strengthening national unity,” the President said. Read more

MPIRA SASA UKO KWA JK, AK NA CCM

Nilikuwa sehemu ya historia mwishoni mwa wiki nilipokuwa katika uwanja wa Kibanda Maiti na kushuhudia Chama cha Upinzani CUF kikitangaza kuwa kimemtambua Rais wa Zanzibar Amani Karume. Ni moja ya siku ambazo uwanja huo ulijaa sana maana wananchi, wapenzi na wanachama wa CUF walikuwa wakitarajia kusikia kitu kufuatia taarifa kuwa Seif Sharif Hamad na Amani Karume wamekutana. Endelea kusoma zaidi

SEIF AENDELEA KUENEZA UJUMBE WA KUMTAMBUA RAIS KARUME

SITOFAHAMU kwa tamko la Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Seif Sharif Hamad, kuwataka wafuasi wake kuitambua serikali ya Rais wa Zanzibr na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume, kimezusha malumbano katika vikao vya ndani vinavyofanywa na Chama hicho. Hali hiyo imejitokeza baada ya baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Kamati Tendaji Wilaya na Majimbo 19 ya Mkoa wa Mjini, kumtupia lawama Katibu Mkuu wao na kueleza kwamba uamuzi huo umefanywa haraka bila ya kuwahusisha viongozi wengine. Endelea kusoma

MUWAZA YAWAUNGA MKONO SEIF, KARUME

Jumuiya wa Wazanzibari inayojihusisha na Mutakabali mwema wa Zanzibar imetoa tamko lake maalum kuunga mkono jitihada za makusudi zinazochukuliwa na Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Abeid Karume katika kujenga Zanzibar mpya. Soma hapa

ZAWA UK YAWAUNGA MKONO SEIF, KARUME

Jumuiya ya Wazanzibari waishio Uingereza (ZAWA-UK) inawapongeza
Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa kukutana na kuazimia kuwaunganisha Wazanzibari ili kuhakikisha kuwa Visiwa vya Zanzibar vinakuwa na amani, mshikamano na kufungua milango zaidi ya maendeleo. Endelea kusoma zaidi

SAY SOMETHING, KARUME ADVISED

Zanzibar President Amani Abeid Karume should end his silence and shed more light on his agreement with his longtime political rival, Mr Seif Shariff Hamad, a respected commentator said yesterday. At the same time, the US embassy commended the two leaders for putting their differences aside, and said the gesture should be followed by concrete measures to end the longstanding political stalemate in the isles. Read more

BALOZI AFRIKA KUSINI ASIFIA MAPATANO Z’BAR

AFRIKA Kusini imeeleza kuridhishwa na mazungumzo kati ya rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume na Seif Sharrif Hamad ambaye ni katibu mkuu wa CUF na kueleza kuwa hatua hiyo ni changamoto kwa bara la Afrika. Balozi wa Afrika Kusini, Sindiso Mfenyana, ambaye anamaliza muda wake nchini, alisema hayo jana wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais Karume Ikulu mjini Zanzibar. Endelea kusoma

Kipi kinamzuia Karume kuunda serekali ya pamoja hivi sasa?

Ambapo pia tunajua kuwa Hoja hiyo ni sawa na kuweka nia. Ni nia kwa sababu Hoja Binafsi hiyo iliyotolewa na Kiongozi wa Upinzani Abubakar Khamis Bakar, imewekewa masharti ya kupitia katika mtihani wa Kura ya Maoni ambayo haitofanyika isipokuwa baada ya kupitishwa Sheria ya Kura ya Maoni ambayo inaweza kupelekwa Baraza la Wawakilishi wakati wowote kuanzia hivi sasa. Endelea kusoma

Jussa Ladhu aukosoa Muswada wa Uchaguzi

Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Ismail Jusa Ladhu (CUF), jana aliingia bungeni kwa kishindo kwa kuwa mbunge wa kwanza aliyechangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi wa mwaka 2009. Ladhu ambaye alizungumza kwa umakini na kujiamini, alianza kwa kumshukuru Rais kwa kumteua na kueleza kitendo hicho kama cha kiungwana ambacho kina nia ya dhati ya kuimarisha demokrasia nchini. Endelea kusoma

Jussa alitikisa Bunge

MBUNGE wa Kuteuliwa na Rais, Ismail Jussa Ladhu (CUF), jana ameingia bungeni kwa kishindo baada ya kuzungumza kwa mara ya kwanza akionya kuwa suala la mgombea binafsi si hiari ya serikali bali ni uamuzi halali wa Mahakama Kuu hivyo serikali inatakiwa kuweka utaratibu mzuri wa kulitekeleza. Jussa alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali za uchaguzi wa mwaka 2009 uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, Philip Marmo. Alisema hivi karibuni Jaji Mkuu Augustino Ramadhan akishirikiana na jopo la majaji kutoa kauli kuwa suala la mgombea binafsi ni halali kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama Kuu. Endelea kusoma

Karume praised over ‘Muafaka’

THE National Executive Committee of CCM has commended Zanzibar President Amani Abeid Karume for his efforts to solve the political stalemate (Muafaka) in the isles. The meeting which started in the morning and stretched to late evening under the chairmanship of President Jakaya KIkwete, was impressed by the initiatives. Read more

Lipumba: Siamini kama haya ni maamuzi ya NEC

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema hakiamini kama Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) inaweza kupingana na maamuzi yaliyokwisha amuliwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu serikali ya mseto. Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na gazeti hili. “Ninaamini wajumbe wa NEC ya CCM ni makini sana, siamini kama wanaweza kutoa maamuzi yanayopingana na yale yaliyokwishaamuliwa na Baraza la Wawakilishi,” alisema huku akionyesha wasiwasi mkubwa. Endelea kusoma

Maalim Seif atunukiwa London

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad ametunukiwa nishani na Wazanzibari waishio nchini Uingereza kwa juhudi zake za kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya Zanzibar. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, nishani hiyo alikabidhiwa juzi nchini Uingereza yenye kigae na alama ya visiwa viwili vya Unguja na Pemba, ikiashiria kuzaliwa kwa kizazi kipya cha Wazanzibari. Endelea kusoma

`CCM can`t overrule Reps on referendum`

Zanzibar House of Representatives Speaker Pandu Ameir Kificho declared yesterday that the planned referendum on the formation of a coalition government in the Isles will be conducted before the October General Election as decided by the House late last month. He was reacting to media reports that the CCM National Executive Committee meeting which ended in Dodoma on Monday had recommended that the referendum be held after the General Election. Read more

Proposal for Zanzibar government gets mixed reactions

Intellectuals, politicians and ordinary citizen have differed on the decision by CCM National Executive Committee proposal to form an inclusive instead of coalition government in the Isles. In separate interviews with The Guardian yesterday, some said that the NEC recommendation interfered with the principles of good governance while others viewed it as the party’s strategy to defeat the opposition. Read more

Kificho: Kura ya maoni serikali ya mseto Z`bar kabla ya uchaguzi

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, amesema kura ya maoni itakayoamua kuundwa kwa Serikali ya Mseto Zanzibar itafanyika kabla ya uchaguzi Mkuu kama ilivyoamuliwa na Wajumbe wa Baraza hilo Januari, mwaka huu. Akizungumza na Nipashe jana Zanzibar, Spika Kificho, alisema hakuna mtu mwenye ubavu wa kubadilisha maamuzi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi zaidi ya wenyewe waliopitisha uamuzi huo. Endelea kusoma

Zanzibar unity government has full blessings – Membe

The Union government has already endorsed the formation and structure of a government of national unity for Zanzibar, Foreign Affairs and International Co-operation minister Bernard Membe said in Dar es Salaam yesterday. He said the whole thing was fully in line with the resolution by the CCM National Executive Committee at Butiama in Mara Region in 2008, which also called for a referendum on the issue. Read more

NEC: Ni chombo cha kuvunja sheria?

BARAZA la Wawakilishi la Zanzibar mwezi uliopita lilikubaliana kwa kauli moja juu ya kuundwa serikali ya mseto kumaliza mgogoro wa kisiasa uliokuwepo Visiwani kwa zaidi ya miaka 15 ili kujenga mazingira ya amani na maelewano. Wawakilishi hawa wa CCM na CUF pia walitaka ifanyike kura ya maoni kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu. Wapo walioona hapakuwepo haja hiyo kwa vile waliona si kawaida kuwauliza watu kama wanataka umoja na kusikilizana. Endelea kusoma

Barua ya Prof. Shivji kwa Karume na Seif

Madhumuni ya kusogeza uchaguzi ni kutoa muda wa kutosha wa kuchukua hatua za awali lakini za lazima kujenga mazingira yatakayowezesha uchaguzi wa amani, haki na huru. Kwa hivyo, kinachohitajika ni kipindi cha mpito (tuseme kama miaka miwili) kutekeleza hatua maalum, yaliyoainishwa na kukubaliwa kisheria. Kipindi hiki ni cha mpito (transitional period) kati ya mazingira ya uhasama tuliyonayo, na mazingira ya ushindani, tunayotaka. Barua ya Prof. Shivji

Maridhiano ya Wazanzibari: Ufafanuzi wa taarifa za magazeti

Suala la Maridhiano haya ni la Wazanzibari wote kwa ujumla wao. Lolote zuri linalohusiana nayo ni kwa maslahi ya Wazanzibari wote; na sio kwa CUF tu au CCM tu. Vile vile kama litafeli au kufelishwa kwa makusudi, basi hasara yake itakuwa ni kwa Wazanzibari wote; na sio kwa CUF tu au CCM tu. Kwa sababu hiyo, ndiyo maana CUF kama Chama, haina lolote la kusherehekea au kulilia peke yake; kwani furaha au kilio cha Maridhiano haya ni kwa Wazanzibari na Watanzania wote kwa pamoja. CUF haijapanga sherehe wala kujiundia Baraza la Mawaziri; kwani hivyo ni vitu vidogo mbele ya maslahi ya nchi, ambayo CUF inasimamia. Taarifa ya CUF kwa Vyombo vya Habari

“The Time Has Come!” wasema Wazanzibari

Bwana Mohammed Kombo akisoma risala ya wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar siku ya tarehe 16 Januari 2010 katika maandamano ya kumuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alitoa pendekezo la kusogezwa mbele kwa uchaguzi wa Zanzibar wa 2010


“Itoshe kufupisha maneno kwa kusema “The Time Has Come.” Sasa wakati umeshafika Zanzibar. Wakati wa kuinasua nchi hii kutoka nusu karne ya uhasama, ubaguzi, chuki na siasa za shaka na wasiwasi. Wakati umefika wa kuondoka hapa tulipo na kwenda mbele. Wakati umefika wa kuijenga upya Zanzibar kwa maslahi ya kila Mzanzibari na ya vizazi vyetu. Wakati huo umefika na ni sasa….. Risala

“Karume tena!” – Maamuzi ya Wazanzibari

Wazanzibari wote, bila kujali itikadi za vyama vyao, sasa wanaunganika nyuma ya Zanzibar Mpya, Zanzibar Moja!

Nawe Raisi Amani

Tunakujuwa moyoni

Kurefusha hutamani

Mudao ukiishia

Ila sisi ndio watu

Tulokupa kiti chetu

U mtumwa mbele yetu

Wapaswa tutumikia…. Utenzi


Maridhiano na Mustakbali wa Zanzibar

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akitoa mada ya Maridhiano na Mustakbali wa Zanzibar kwa washiriki wa Kongamano lililofanyika tarehe 15 Januari 2010 kwenye ukumbi wa Salama, Bwanani Hotel, Zanzibar

“Katika chaguzi hizo zote zilizowahi kufanyika Zanzibar, ukiacha uchaguzi wa mwanzo wa 1957, hakujawahi kutokea uchaguzi wowote ambao washiriki wake waliridhika kikamilifu na uendeshaji wake na wakayapokea kwa moyo mkunjufu matokeo yake. ASP ililalamikia uendeshaji na matokeo ya chaguzi za Januari 1961, Juni 1961 na Julai 1963 na katika kipindi hiki cha kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi tokea mwaka 1992, CUF imelalamikia uendeshaji na matokeo ya chaguzi za 1995, 2000 na 2005. Kikubwa kinachokosekana ni imani kwa taasisi zinazoendesha na kusimamia chaguzi.” Mada ya Maalim Seif

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s