CUF News/Press

Kujiuzulu kwa Mheshimiwa Jussa si mgogoro wala kuyumba kwa CUF

Kujiuzulu ni jambo la kawaida lakini tu katika taasisi iliyopevuka kidemokrasia na kiuwajibikaji. Hii ndio maana si jambo la kawaida katika vyama vyote vya siasa hapa nchini ukiwachia CUF. Mheshimiwa Jussa amejitathmini na kujiona kuwa chama kimemkabidhi majukumu mawili makubwa, Mtendaji Mkuu wa chama kwa upande wa Zanzibar na Mpambanaji katika baraza la wawakilishi. Majukumu haya… Endelea hapa

Jussa ajiuzulu

Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa, muda mchache uliopita, ikielezea azma yake ya kujiuzulu nafasi hiyo. Hata hivyo, Jussa anabakia na nafasi zake nyengine kwenye Chama, ikiwemo ya ujumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, na pia nafasi yake ya kuchaguliwa na wananchi ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jimbo la Mji Mkongwe. Bonyeza hapa kuendelea….

Elimu ya dini iimarishe Madrasa – Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Al-haj Maalim Seif Sharif Hamad amesema mafanikio yaliyopatikana katika chuo cha Madrasat Nuur Islamiya cha Ukutani Zanzibar ni neema kwa Wazanzibari wote na wanapaswa kuithamini na kuiendeleza neema hiyo.

Endelea hapa

CUF chama pekee cha kuondosha ufisadi – Maalim

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ameupongeza uongozi wa Chama hicho Wilaya ya Kinondoni mjini Dar es Salaam kutokana na juhudi unazozichukua katika kukiendeleza Chama hicho.

Endelea hapa

Taarifa kwa vyombo vya habari

Kama ilivyobainika kwa umma wa Wazanzibari, Chama cha Wananchi, CUF, kimepokea kwa moyo mmoja Hatua ya Kamati Teule ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, tokea kuteuliwa kwake hadi Ripoti yake Rasmi, juu ya namna ambavyo Serikali…..Endelea hapa….

Katiba mpya iziweke rslimali mikononi mwa wananchi -Lipumba

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amewataka Watanzania kusimama imara na kujipanga katika kutoa maoni ya katiba mpya, ili kuhakikisha kuwa katiba inaweka wazi suala la maliasili kuwa rasilimali za Watanzania. Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na maliasili nyingi zikiwemo dhahabu, almasi, Tanzanite, shaba na…. Endelea hapa

Uamuzi wa baraza kuu ni sahihi – Lipumba

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba amesema uamuzi wa kumfukuza uanachama mwakilishi wa Jimbo la Wawi Bw. Hamad Rashid Mohd ulikuwa sahihi na wala hayakuwa maamuzi magumu kama baadhi ya watu wanavyofikiria.    Endelea hapa

CUF yatangaza ‘vita’ kupigania eneo la kiuchumi katika  bahari kuu.

Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi mambo ya nje wa Chama cha CUF, Ismail Jussa Ladhu
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema.. Endelea hapa

Wakati umefika kuzungumzia ajenda ya Zanzibar

ATIKA utamaduni wetu wa Kiswahili tuna usemi usemao: ‘Ukimstahi mke ndugu huzai naye.’ Staha na kuoneana haya ni miongoni mwa sifa za uungwana wetu. Hata hivyo, kuna nyakati ambapo huwa hatuna budi ila tuziweke kando sifa hizo ili tuweze kuambizana ukweli kwa madhumuni ya kujenga, si kubomowa.  Endelea hapa

Balozi Hamza amuaga Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar na Misri zina uhusiano mkubwa wa kidugu na kihistoria katika nyanja za kiuchumi, kijamii na maendeleo na kuna haja uhusiano huo ukaendelezwa na kuimarishwa zaidi. Endelea hapa….

Pingeni mafuta kuingizwa kwenye Muungano – Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya demokrasia kibandamaiti mjini Zanzibar. Endelea hapa…

CUF yafunika Uzi

 • vijana 142 wapewa kadi
 • shangwe, nderemo mji mzima

Na Said Kombo Hamad, CUF Makao makuu 

Nianze kwa kuelezea ‘uwezo wa kukubali’ kwa kiumbe kiitwacho binaadamu. Uwezo huu hutofautiana sana katika jamii za watu, na pengine hata kupelekea kuwa ni sehemu ya tabia za binadamu huyo. Endele hapa…

Karafuu lazima ifanyiwe utafiti – Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuelekeza nguvu zake katika kufanya utafiti wa zao la karafuu kuliwezesha listawi vizuri zaidi na kupata thamani kubwa zaidi katika soko la Kimataifa. Endelea hapa…

Utaratibu wa kumpata  mgombea urais wa Tanzania, lazima uzingatie na Zanzibar – Maalim

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema miongoni mwa changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi katika marekebisho ya katiba mpya ya Tanzania ni utaratibu wa kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano, ili wazanzibari nao waweze kuitumikia nafasi hiyo… Endelea hapa...

Zanzibar iwe na Benki kuu yake – Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ni muhimu kwa sasa Zanzibar kuwa na benki kuu yake ikiwa inataka kutumia kikamilifu rasilimali zake kujenga uchumi wake. Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akizungumza katika viwanja vya Kibandamaiti mjini hapa juzi alisema kuendelea kutegemea Benki Kuu ya Tanzania (BoT),… Endelea hapa

Wazanzibari tuungane – Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema hana tatizo la wanaotetea serikali mbili lakini kuwepo na mfumo maalumu utakaokubalika na wananchi wote. Alisema wale wanaotetea mfumo wa Serikali mbili, kama ni hivyo yeye hana tatizo. Ila ziwepo Serikali mbili, moja ya Zanzibar na …. Endelea hapa

Kuwamo kwenye serikali, hakujanitoa kwenye dhamira – Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amepinga vikali shutuma za baadhi ya watu kwamba tangu kuingia madarakani katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, yeye na chama chake wameacha kupigania maslahi ya Zanzibar kwenye Muungano. Endelea hapa

Chokochoko ndani ya CUF zimalizwe haraka

Chama cha Wananchi, ama Citizen United Front (CUF), sio chama cha siasa cha Kiislamu wala si cha Waislamu. Kisingeweza kuwa hivyo na kikasajiliwa na kikaruhusiwa kutangaza sera zake nchi nzima, Bara na Visiwani, kwa vile sheria ya nchi hii imepiga marufuku kabisa vyama vya siasa vyenye mlengo wa…. Endelea hapa

 

Hakuna migogoro CUF , zilizopo ni chokochoko – Maalim seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema miongoni mwa changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi katika marekebisho ya katiba mpya ya Tanzania ni utaratibu wa kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano, ili wazanzibari nao waweze kuitumikia nafasi hiyo. Endelea hapa…Afya ni kipaumbele katika serikali yetu – Maalim Seif.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kutoa kipaumbele kwa sekta ya afya kutokana na umuhimu wake kwa jamii katika kuchangia maendeleo ya wananchi na taifa kwa jumla. Kauli hiyo imetolwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa… Endelea hapa….. 

Maalim Seif atoa ovyo kwa wachafuaji chama.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF)Maalim Seif Sharif Hamad amesema Chama hicho kiko imara na kimejipanga kukabiliana na mtu yoyote atakayejaribu kukichafua. Amesema licha ya Chama hicho kuandamwa na kusemwa vibaya kupitia vyombo mbali mbali vya habari katika siku za hivi karibuni, lakini…Endelea hapa…

Tanzania ina fursa nyingi ya kutumia rasilimali zake-Maalim Seif.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar ina nafasi nzuri ya kujiendeleza kiuchumi baada ya kufanikiwa kumaliza migogoro ya kisiasa iliyokuwa ikiikabili kwa muda mrefu.Endelea hapa…

Maalim ataka elimu zaidi kukabiliana na utapeli wa mitandao.

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amelitaka Jeshi la Polisi kuzidisha bidii katika kuwapa watendaji wake taaluma ya utambuzi wa njia zinazotumika kufanikisha uhalifu kupitia mtandao (cyber crimes) kwa nia ya kukomesha uhalifu wa aina hiyo hapa nchini. Endelea hapa…

Maalim Seif aeleza mafanikio ya serikali.

Maalim Seif aeleza mafanikio ya serikali
Norway imesema itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika juhudi zake za kudumisha umoja na mshikamano uliopatikana baada ya kufikiwa maridhiano ya kisiasa, kwa vile hali hiyo imeonesha dalili nzuri za kukuza maendeleo ya wananchi katika kipindi cha mwaka mmoja chini ya serikali ya umoja wa kitaifa

Endelea hapa….

Katiba ya Zanzibar ni Gari letu la mwisho!

Katiba yetu ya Zanzibar ndio dira! Kama kuongeza au kupunguza ni ndani ya Katiba ya Zanzibar. Tukiishadidia Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni sawa na kuutawadhisha ubatili wa Muungano.Ni sawa na kuambiwa nguruwe ni haramu ukasema utamtawadhisha na utakapomchinja utaelekea kibla. Endelea hapa

Kikwete asifiwa kuheshimu hadhi ya Z’bar

WAKATI  Tanzania inajiandaa kutunga Katiba mpya, Katibu  Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema umoja na sauti moja  ndio silaha pekee ya kuwawezesha Wazanzibari kulinda maslahi ya Zanzibar ndani ya serikali ya Muungano. Endelea hapa…

Muungano ni kama koti likikubana unalivua – Sheikh Karume…

ALASIRI moja nikiwa kwenye hoteli niliyoshukia mji mkuu wa Sudan, Khartoum Hilton, nilishuhudia  vurumai kubwa katika sehemu ya karibu na lifti. Watu wakikimbilia huko wakiambizana kwa msisimko kuwa ‘sheikh amefika, sheikh amefika.’ Endelea hapa

Utiaji Saini wa Mkataba wa Muungano na Matokeo Yake {UHARAMU WA MUUNGANO}

“Hapana shaka yoyote kuwa Mkataba [wa Muungano] uliandaliwa kwa siri sana. Maofisa wawili [wa Kiingereza] Brown na Fifoot walihusika kwa karibu sana. Hakukuwa na mshauri wa kisheria kwa upande wa Zanzibar. Karume hakuliarifu Baraza la Mapinduzi. Jumbe alikuwa hajui. Endelea hapa….

Sheria za uchaguzi zifuatwe – Maalim Seif

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF); Maalim Seif Sharif Hamad amezitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhakikisha Sheria ya Gharama za Uchaguzi iliyotungwa nchini, inafuatwa na kutekelezwa kivitendo ili uchaguzi unaofanyika uwe huru na haki na usiotawaliwa na rushwa. Endelea hapa…

Kuwanyima vitambulisho wananchi hakutovumiliwa – Maalim Seif

Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF amesema cha chake hakiwezi kukubali kuona baadhi ya wazanzibari wanaendelea kunyimwa haki yao ya kupatiwa vitambulisho vya uzanzibari ukaazi.   Endelea hapa…..

Mswaada mpya wa mabadiliko ya katiba mtego kwa Zanzibar

Mswada mpya wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao utafikishwa bungeni hivi karibuni kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa kuwa sheria bado unaonekana kubeba vifungu vya mitego dhidi ya upande wa Zanzibar, ili kutoa mwanya kwa watanganyika kupenyeza maslahi yao katika katiba hiyo. Miongoni mwa maeneo yanayoonekana kuwa ni mitego ni yakiwemo haya yafuatayo. Endelea hapa

Maalim Seif awakia masheha Zanzibar

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ambaye piya ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema viongozi wa serikali za mitaa (Masheha) wanawanyima fomu za kuombea vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi wafuasi wa CUF kwa makusudi ili kinapoteza nguvu ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.  Endelea hapa

Tamko la MUWAZA juu ya kiapo cha Rais wa Zanzibar katika baraza la mawaziri la Muungano

MUWAZA imepata mshangao na kusikitishwa na hatua ya rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kuamua kula kiapo kwa minajili ya kuingia katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunakiona kitendo hiki kama ni muendelezo wa udhalilishaji kwa Serikali ya Zanzibar pamoja na wananchi wake. Endelea hapa…

CUF yatamka

Chama cha Wananchi CUF kimeridhia muundo wa tume ambayo imeteuliwa na Rais  wa Zanzibar kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa ajali ya meli ya MV Spice Islanders iliyotokea tarehe 10 usiku katika  mkondo wa Nungwi ikwa njiani kuelea kisiwani Pemba. Endelea hapa….

CUF yamjia juu Lowassa 

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema hakuna sababu ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, kukaripia vyombo vya habari na madai ya kuwaonea huruma Watanzania na kuwalaumu wenzake wakati na yeye ni sehemu ya matatizo yao. Endelea hapa

Tume ya Uchaguzi “kitanzini” Igunga

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaweza “kutiwa kitanzini” iwapo itathibitika kuwa ilichakachua daftari la wapigakura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Igunga,  Endelea zaidi hapa…

KESI ZA UCHAGUZI MKUU:CUF yaanguka, CHADEMA, CCM wakwama

WANAODAIWA kuwa wafuasi wa CUF wamefanya vurugu mahakamani, kuvamia maduka na kuiba mali na kutaka kuichoma moto nyumba ya Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mtwara, kwa kile kilichoelezwa kuwa kutoridhishwa na hukumu ya Mahakama Kuu iliyompa ushindi Mbunge wa CCM, Asnain Murji, dhidi ya mpinzani wake, Hassan Uledi wa CUF. Endelea zaidi hapa…

INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAAJIUN THE CIVIC UNITED FRONT (CUF- Chama Cha Wananchi) Kurugenzi ya Haki za Binadamu, Habari na Uenezi. Office of the Secretary General P.O.BOX 3637,Zanzibar,Tanzania E-mail: cufhabari@yahoo.co.uk

Weblog:http:hakinaumma.wordpress.com Our Ref: CUF/HQ/KR/U/01/011/31                                             Date: 18/10/2011. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wairan kujenga hospitali za kisasa Zanzibar

 • Moja kujengwa Wete Pemba na nyengine Mjini Magharibi Unguja.
 • Maalim Seif ashuhudia utiaji saini.

Juhudi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuinuwa huduma yza afya kwa wananchi, ikiwemo kuwapunguzia gharama za kwenda kutibiwa nje ya nchi zimeanza kuonesha dalili za mafanikio  baada ya Serikali kutiliana saini makubaliano ya ujenzi wa hospitali mbili zqa kisasa zitakazojengwa katika mji wa Wete Pemba na mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Endelea hapa….

CCM, CUF serikalini ‘tuko makini’

MIEZI saba baada ya kuundwa kwa serikali iliyoshirikisha vyama viwili vilivyokuwa hasimu kisiasa visiwani Zanzibar – Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar imethibitisha kuwa hakuna kisichowezekana. Endelea hapa…

Jinamizi la  laing’ang’ania CCM

 • Mabalozi 18 wajiengua, wadai rushwa ilitawala
 • Madiwani Songea wagomea kikao kupinga uchaguzi
 • M’kiti Lushotoa ajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi
 • Madiwani wagomea kikao

Wakati hali ikiwa hivyo Igunga, baadhi ya madiwani wa Chama CCM Manispaa ya Songea wamesusia kikao kilichoitishwa na viongozi wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa ni mgomo wa kudumu kushinikiza kujiuzulu kwa Meya wao aliyechaguliwa hivi karibuni Bw. Charles Mhagama. Endelea nayo…..

Hatimae mrithi wa Rostam ajulikana, Igunga

 • Kafumu aibuka kidedea
 • Amzidi mgombea wa CHADEMA kura 3,224
 • Mahona wa CUF aambulia kura 2, 104
 • Mabomu ya machozi yafunika mji wa Igunga

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimeiubuka kidedea katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga baada ya mgombea wake Dkt. Peter Kafumu kumzidi mpinzani wake wa karibu, Bw. Joseph Kashindye wa CHADEMA kwa kura 3,224. Endelea nayo….

 

Igunga kwachafuka

 • mabomu ya machozi yatumika
 • CCM  watumia mapanga kuwatimua CHADEMA

MJI wa Igunga jana uligeuka uwanja wa mapambano kati ya wafuasi wa Chadema na Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ambao walilazimika kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya.Milio ya mabomu yaliyofyatuliwa nje ya ofisi za msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na ving’ora vya polisi vilitikisa mji huo kiasi cha kuzifanya kutanda moshi mweupe. Endelea nayo….

Polisi wawatawanya CHADEMA

 • matokeo ya kura
 • Mchuano wabaki kwa CHADEMA na CCM, CUF vyama vyengine hoi!
 • Awali CHADEMA walifurika mitaani kushangilia
 • CCM yageuza kibao matokeo ya vijijini
 • Utulivu watawala katika upigaji kura

WAKATI matokeo ya uchaguzi mdogo wa Igunga yakionyesha kuwapo kwa mchuano mkali kati ya CCM na Chadema, jana jioni Polisi  walilazimika kuwatawanya wafuasi wa chama hicho kikuu cha upinzani ambao walikuwa wakishinikiza kubandikwa kwa matokeo kwenye vituo huku wengine wakiimba nyimbo za hamasa kushangilia kile walichokiita ushindi wa mgombea wao, Joseph Kashindye. Endelea nayo…    

Igunga kumekucha

WAKATI leo wananchi wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora wanapiga kura kumchagua Mbunge wao mpya, vituko, vijembe na shamrashamra viligubika mikutano ya mwisho ya kampeni kwa vyama vinane vilivyosimamisha wagombea jana. Moja ya makosa ambalo lingeweza kuchafua ufungaji wa kampeni za uchaguzi mdogo Igunga jana, ni uamuzi wa vyama vya CCM, Chadema na CUF, kufanya mikutano yao katika viwanja vilivyo jirani na Igunga mjini kiasi kwamba mgombea akizungumza uwanja mmoja, viwanja vingine vinamsikia. Endelea nayo….

Hukumu ya Igunga leo Ile siku imefika • Wananchi wa Igunga kumtaka nani awe mbunge wao

MACHO na masikio ya Watanzania, leo yanaelekezwa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, ambako wananchi wanapiga kura kumchagua mgombea mmoja kati ya wanane wanaoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge, kuwa mbunge wao.Mgombea atakayechaguliwa atamrithi Rostam Aziz, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, ambaye alijiuzulu katika tukio lililohusishwa na mchakato wa kujivua gamba ndani ya chama hicho. Endelea nayo….

Igunga moto NEC kutangaza matokeo ndani ya masaa 24

PRESHA imezidi kupanda Igunga. Wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ikiahidi kutangaza matokeo ya ubunge katika jimbo hilo ndani ya saa 24, vyama vitatu vikubwa CCM, Chadema na CUF vimeendelea kushutumiana kila kimoja kikidai kuhujumiwa.Usiku wa kuamkia jana, CCM kikiwatumia walinzi wake wa Green Guard kiliwazingira vijana 120 wa Chadema kwa tuhuma za kuingia na silaha ili kuvuruga uchaguzi huo uliopangwa kufanyika kesho. Wakati Chadema kwa upande wake kikidai kwamba kitendo hicho cha CCM ni kiwewe cha kushindwa uchaguzi huo, CUF kimekuja na tuhuma nzito dhidi ya Nec kwamba inakiandalia ushindi chama tawala, CCM. Endelea nayo…..

Helicopta ya CCM yapotea Igunga

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, helikopta inayotumiwa na  CCM katika kampeni za Igunga imeripotiwa kupotea ikiwa angani wakati ikijaribu kutafuta vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Dk Dalaly Kafumu.Taarifa za kupotea kwa helikopta hiyo zilianza kuzagaa jana majira ya saa tano asubuhi mjini Igunga na baadaye zilithibitishwa na mmoja wa maofisa wa CCM ambaye hakutaka jina lake litajwe kuwa walipotea mara kadhaa baada ya mtu wanayemtegemea kuwaongoza njia kupoteza ramani akiwa angani.“Unajua tumemchukua mtu ambaye anaifahamu vizuri Igunga ili aweze kuielekeza helikopta mahala pa kwenda, lakini kwa bahati mbaya mtu huyo alipokuwa angani alishindwa kwa sababu ya kupoteza ramani,” alisema ofisa huyo.Endelea nayo……

Mahona: Natembea na ushindi Igunga

LEOPOLD Lucas Mahona, mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepitishwa kuwania ubunge Jimbo la Igunga amesema tayari ana mtaji wa ushindi kutokana na kura alizopata katika uchaguzi mkuu mwaka jana. Katika uchaguzi mkuu uliopita, Mahona alipata kura 11,321, huku Rostam Aziz wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akishinda kwa kura 35,674. Endelea nayo… Helikopta ya Chadema yatikisa Igunga

WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilitikisa anga la Igunga baada ya kuanza kutumia helikopta kufanya kampeni zake, zile mbili za wapinzani wao, CCM zikishindwa kuwasili jimboni humo na kubaki Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutokana na sababu za kiufundi.Wakati Chadema ikipasua anga na mbili za CCM zikibaki KIA, helikopta ya Chama cha Wananchi (CUF) nayo imeshindwa kutua Igunga jana na sasa inatarajiwa hapa leo. Endelea nayo….

Kibano chawageukia CCM, Igunga

 • Makada wake wakamatwa kwa kuchoma bendera za Chadema
 • Mukama awaangukia wananchi, adai ametumwa na Kikwete
 • Prof. Safari awajibu wanazuoni wa kiislamu kuhusu DC
 • Nyumba ya Katibu Kata wa CUF Nyandekwe yachomwa moto

JESHI la Polisi Wilayani Igunga mkoani Tabora, linawashikilia kiongozi mmoja na kada mwingine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kosa kuchoma mabango ya picha ya mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kushusha bendera za chama hicho. Endelea nayo

CUF yaitolea uvivu CCM

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeng’ara katika mdahalo wa vyama vyenye nafasi kubwa ya kutwaa kiti cha ubunge wa Jimbo la Igunga baada ya Naibu Katibu Mkuu wake , Bw. Julius Mtatiro kukitolea uvivu CCM kuwa ndicho kinasababisha vurugu na kuandaa makundi ya vijana nje ya  Igunga. Bw. Mtatiro aliyepata nafasi ya mwisho kutoa nasaha zake upande wa viongozi wa vyama vilivyoshiriki mdahalo huo, alisema CCM imeshindwa kuwasaidia wananchi wa Igunga kwa miaka 50 tangu uhuru, hivyo kimezeeka, kinatakiwa kipishe maendeleo yaletwe na wapinzani hasa mgombea wa chama chake, Bw. Leopold Mahona. Endelea nayo……

CUF ‘kidedea’ mdahalo Igunga

CHAMA cha Wananchi (CUF) juzi usiku kiliibuka ‘kidedea’ katika mdahalo wa wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda ubunge wa Igunga, huku CCM na Chadema wakijikuta katika wakati mgumu wa kujibu tuhuma zinazowakabili wagombea wao. Hata hivyo, katika mdahalo huo uliotawaliwa na vurugu za mashabiki wa vyama hivyo tangu mwanzo hadi mwisho, mgombea wa CCM, Dk. Dalaly Kafumu, aliwashangaza wana CCM kwa utulivu na uwezo wake wa kutumia Ilani ya CCM, usomi na ufahamu wake wa jimbo hilo kujibu tuhuma ziliwandama kuhusu mikataba mibovu ya madini. Bamiza hapa kuendelea na taarifa hii…

Ni kufa na kupona, Igunga;

 • Hesabu zavibakisha CUF,CHADEMA na CCM katika kinyang’anyiro

KAMPENI za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga, leo zinaingia katika wiki ya lala salama huku tathmini ikionyesha kuwa mchuano mkali ni baina ya vyama vitatu, licha ya vyama nane kusimamisha wagombea wake. Vyama vyenye ushawishi mkubwa kisiasa jimboni humo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2, ni CCM kilichomsimamisha Dk Dalaly Kafumu, CUF kilichomsimamisha Leopard Mahona na Chadema ambacho kimemsimaisha, Joseph Kashindye.

Bamiza hapa kuendelea na habari hii…

CUF yaituhumu CCM Igunga.

CUF kimelitaka Jeshi la Polisi kumkamata na kumchukulia hatua kali, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana ya CCM Taifa (UVCCM), Martine Shigela kutokana na msafara wake kumshambulia kiongozi wa CUF.   Akizungumza na waandishi wa habari Mjini hapa jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (bara), Julius Mtatiro, alisema kitendo cha msafara wa katibu huyo kushambulia mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya CUF ni uchokozi. Endelea kusoma taarifa hii….

CCM  yakaliwa pabaya Igunga

Upepo wa kisiasa si shwari kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa Igunga baada ya wafanyabiashara mashuhuri walioombwa na chama hicho kuchangia sh milioni 300 kugoma kutoa fedha hizo.Habari za uhakika kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara hao waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina, zinasema wafanyabiashara hao wamegoma kwa sababu wamegundua CCM kinafuja pesa kwa anasa badala ya kampeni

Endelea kusoma habari hii…

SABABU 10+ ZA PROF. LIPUMBA KUWA RAIS 2010 Dira ya Mabadiliko tunayowapelekea Watanzania, ambayo ndiyo itakuwa msingi wa ilani ya Uchaguzi wa CUF kwa mwaka huu wa 2010, na ambayo tutawaomba waiunge memkono kupitia uchaguzi Mkuu huu inatilia mkazo mambo 22 ambayo tuaamini chini ya Serikali ya CUF yatatujengea Tanzania Mpya inayojili haki sawa kwa wananchi wote na itakayojenga uchumi imara unaoongeza ajira na utakaoleta neema na tija kwa wote. Endelea kusoma hotuba ya Prof. Lipumba CUF YAGUNDUA ‘MADUDU’ MINGINE YA ZEC

“Kwa ugunduzi huu, moja kati ya matatu linadhihirika. Aidha, la kwanza, Tume yako haitumii ZAN ID kama kigezo cha mtu kuandikishwa kuwa mpiga kura, vyenginevyo idadi ya waliopewa ZAN ID na wale walioandikishwa na Tume yako ingelikuwa sawa, au, la pili, moja kati ya taasisi zenu mbili (ZEC na Idara ya ZAN ID) inasema uongo kwenye data zake na au, la tatu, kuna uwezekano mkubwa kwamba watu wanapandikizwa kutoka majimbo mengine na masheha, ambao ni mawakala wenu wanaridhia kwa vile ni njama ya kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM). Kama hili linatokea, hakuna uhakika kwamba waliopandikizwa kuandikishwa katika majimbo ambayo si yao hawataandikishwa tena katika majimbo yao muda utapofikia. Kwa hivyo, mnaandaa mazingira yatakayowaruhusu baadhi ya watu kupiga kura zaidi ya mara moja wakati wengine wananyimwa haki ya kujiandikisha.Soma barua kamili ya Katibu Mkuu kwa ZEC hapa “HUU SI UBORESHAJI WA DAFTARI, NI UCHAFUZI TU”

Katika ofisi ya vitambulisho Gamba, Mahonda, Amani na Mwera bado kuna watu wengi ambao wamepewa fomu lakini hawapewi huduma kwa sababu tulizoeleza hapo awali.  Utaratibu uliowekwa wa kuwahudumia wananchi wa kila jimbo kwa siku mbili umewaacha kwa mamia bila kuipata huduma hiyo.  Mfano katika ofisi ya Gamba zaidi ya wananchi 1,000 wa majimbo ya Nungwi, Mkwajuni na Tumbatu wameshindwa kuhudumiwa na majimbo yao yameshamaliza kazi ya uandikishaji na, kwa hivyo, wameshapoteza haki ya kupiga kura 2010. Soma taarifa kamili kwa vyombo vya habari TAMKO LA MAALIM SEIF KUHUSU HALI YA PEMBA

Ukweli unabaki pale pale kwamba chanzo na sababu za mgogoro uliopo ni njama ovu kabisa za CCM na Serikali zake kuwazuia wananchi wengi wa Zanzibar wenye sifa zote za kujiandikisha kuwa wapiga kura na ambao wanasadikiwa kuwa wanaunga mkono CUF wasiweze kujiandikisha, lengo likiwa ni kupunguza kura za upinzani. Sambamba na hilo, njama hizo zinahusisha kutumia idadi hiyo ya wapiga kura halali inayopunguzwa kwa kuwajaza watu wasio na sifa ambao ni pamoja na watu wanaoletwa maalum kutoka Tanzania Bara kuja kuandikishwa na baadaye kuipigia kura CCM, vijana malum walioandaliwa na CCM (maarufu kama Janjaweed) waliosajiliwa na chama hicho na baadaye kupelekwa kuandikishwa zaidi ya mara moja katika majimbo tofauti ya uchaguzi, na watoto wadogo wa umri wa chini ya miaka 18.” Soma tamko kamili VITAMBULISHO: WANANCHI WASONGE MBELE

“Hicho kinachoambiwa kimeghushiwa, kwa mfano, ni cheti ambacho mchapishaji mwenyewe wa serikali aliandika jina la Mohammed kwa ama kifupi cha Moh’d au kwa kuondoa ‘o’ na kuweka ‘u’ na hivyo kuwa Muhammed. Katika mifano mingine, jina kama la Haji limeandikwa Hajj au Hamad limeandikwa Hamadi. Wakati mwengine ni mwenye cheti kukozeshea jina lake kwa kalamu baada ya kuwa hati za mchapishaji wa serikali zimefifia kwenye cheti chake”. Endelea kusoma taarifa hii kwa vyombo vya  habari SMZ IWACHE KUSHABIKIA NA KUENDELEZA UBAGUZI DHIDI YA RAIA

“….ni kiwango cha juu cha ubaguzi na upotofu kwa SMZ kuendeleza sera zake za kibaguzi dhidi ya Wazanzibari wa makundi tafauti. Misingi hii ya kibaguzi ilianza kujengwa dhidi ya Wazanzibari wenye asili ya Pemba kwa kuwanyima fursa na haki kadhaa za msingi zikiwemo za kielimu, kiuchumi na kisiasa; na sasa baada ya kwisha kuwabagua Wapemba, SMZ inawageukia Wangazija. Serikali ya kweli ya watu haisimamii ubaguzi na utengano, bali mapenzi baina ya watu wake na mshikamano.” Endelea kusoma taarifa hii CUF KUONGELEA DAFTARI JUMAPILI

The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) kinawaalika katika mkutano wake na waandishi wa habari utakaofanyika katika ofisi za Chama zilizoko Vuga, mjini Zanzibar, siku ya Jumapili ya tarehe 31 Agosti, 2009, saa 4.00 asubuhi. Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma, Mhe. Salim Bimani atatoa taarifa maalum ya Chama kuhusu Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pamoja na hali ya jumla ya kisiasa nchini. Endelea kusoma taarifa hii UCHAGUZI Z’BAR 2010 MATATANI

“Tumekuwa na makubaliano ya kubadilishana taarifa na Serikali lakini nimeandika barua zaidi ya nne kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu mwafaka huu lakini hakuna majibu hadi sasa. Pamoja na mimi kuandika barua hizo nne pia Katibu wangu Malim Seif Sharif Hamad naye ameandika barua mbili kuhusu utekelezaji wa mwafaka lakini hadi sasa hakuna majibu kutoka kwa Rais.” Anasema Prof. Lipumba. Soma habari kamili STANDOFF IN ZANZIBAR WORRISOME – MAAJAR

Tanzania’s High Commissioner to the United Kingdom, Mwanaidi Maajar, has cautioned over the belief by some investors that efforts to resolve the post-election political standoff in Zanzibar were slowing down and might not bear fruit. Speaking in an exclusive interview with The Guardian in London recently, the envoy said the investors’ risk analysis was not an issue as such but she was worried over their general perception of developments in the Isles. Read the story SMZ TEGUA BOMU HILI PEMBA

Linalosikitisha zaidi, masheha ambao walitegemewa kutoa msaada, pia wako kazini kukwamisha wananchi kuandikishwa. Wanakataa kuwapa barua wasiokuwa na Zan ID ili kuthibitisha kwenye Idara ya Vitambulisho ya Zanzibar kuwatambua wapatiwe kitambulisho hicho, wakidai wameelekezwa na wakuu wao. Katika mlolongo huo, Idara ya Vitambulisho Zanzibar, nayo kwa upande wake imejipanga sawa kuhakikisha inawakomoa wananchi. Soma makala kamili “SMZ/SMT WATUMIA KISINGIZIO CHA KITAMBULISHO CHA MZANZIBARI KUIINGIZA NCHI KATIKA MACHAFUKO”

Hoja inayotolewa na ZEC ni kwamba hayo ndiyo matakwa ya sheria ya Uchaguzi ya 1984 kwenye Kifungu 12 (b). Lakini inaeleweka kwamba kifungu hiki cha sheria kimekwenda kinyume na kifungu cha 11 cha katiba ya Zanzibar na hilo limethibitishwa na hata Mkurugenzi wa ZEC alipoongea na waandishi wa habari huko Pemba. Vile vile, sheria Namba 7 ya 2005 inayohusu Vitambulisho inaweka wazi kwamba ni lazima kwa kila Mzanzibari kuwa na kitambulisho hicho na kwamba, kwanza, kutokuwa nacho ni kosa na, pili, kumzuwia Mzanzibari asikipate ni kosa vile vile. Hivi sasa kuna malalamiko na mifano kadhaa ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kwa kutumia masheha wake, inawazuia Wazanzibari wasipate kitambulisho hicho na wakati huo huo inawapatia wasiokuwa Wazanzibari. Kuna mifano pia ambapo Wazanzibari wanaoonekana na SMZ kuwa wafuasi wa CCM wanapatiwa vitambulisho, lakini wale wanaoonekana kuwa CUF wananyimwa hata kama wanakaa nyumba moja na ni ndugu wa kuzaliwa. Soma taarifa kamili

strong

Advertisements