Maalim Seif aahidi kuleta Mapinduzi Katika Sekta ya Elimu

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema anakusudia kuiendeleza sekta ya elimu kwa kuongeza maslahi ya walimu na kuweka mazingira bora ya kusomea.

Amesema hadhi ya elimu imeshuka Zanzibar, na kwamba iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao atahakikisha kuwa sekta ya elimu inapewa nafasi yake kwani ndio msingi wa maendeleo.

Maalim Seif ameeleza hayo wakati akiendelea kuichambua ilani ya Chama hicho katika mkutano wa hadhara iliofanyika viwanja vya Uondwe jimbo la Mtambwe.

Amesema iwapo atachaguliwa ataongeza idadi ya madarasa ya kisasa, ili kupunguza msongomano wa wanafunzi madarasani.

Amefahamisha kuwa elimu itakayotolewa itazingatia viwango vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kuzingatia idadi ya wanafunzi madarasani, ili kuwawezesha wanafunzi watakaohitimu masomo yao kuweza kukabiliana na soko la ajira.

Kuhusu walimu Maalim Seif amesema watapangiwa vipindi vinavyoendana na uwezo wao kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, sambamba na kuyatazama upya maslahi ya mishahara na marupurupu yao.

Mtambwe 1Wafuasi na Wapenzi wa Chama Cha Wananchi CUF wakifuatilia mkutano huo katika viwanja vya Uondwe
Aidha amesema serikali yake inakusudia kujenga nyumba za kutosha za walimu, ili kuwawezesha walimu wanaotoka mbali kuweza kuishi bila ya wasiwasi wowote.

Akizungumzia masomo yenye upungufu wa walimu yakiwemo ya sayansi, Maalim Seif amesema wakati wakiwaandaa wataalamu wa ndani kwenye masomo hayo, watashirikiana na nchi wahisani ili kuweza kuwafundisha watoto masomo hayo hadi hapo walimu wazalendo watakapopatikana.

Amefahamisha kuwa chini ya serikali yake hakuna mzazi atayetozwa mchango wowote wa skuli kwa mtoto wake na kuahidi kurejesha utaratibu wa zamani wa serikali wa kuwapatia watoto huduma zote za elimu zikiwemo madaftari na vitabu vya kusomea.

Mtambwe 2

Wanachama na Wapenzi wa Chama Cha Wananchi CUF Wakiwa wamenyanyua mikono juu ikiwa ni ishara ya Kumuunga mkono Maalim Seif Sharif Hamad.

Kuhusu vifaa vya skuli Maalim Seif amesema serikali yake itaboresha masomo ya sayansi kwa kuzipatia skuli hizo vifaa vya maabara, ili walimu na wanafunzi waweze kutekeleza masomo hayo kwa vitendo.

Aidha amesema wanafunzi na walimu watapatiwa Kompyuta za kutosha, ili kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani.

Nae Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi ya CUF Taifa, Twaha Taslima amesema mabadiliko mwaka huu hayaepukiki, na kuwataka walioko nje ya umoja wa UKAWA kujiweka tayari kwa mabadiliko hayo.

Katika mkutano huo jumla ya wanachama 169 wamejiunga na CUF wakiwemo 7 kutoka Chama Cha ADC na 15 kutoka CCM.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s