Ilani ya Chama Cha Wananchi CUF katika kuyalinda na kuyaenzi Maridhiano na Umoja wa Kitaifa

CUF inaamini kwamba usimamizi mzuri wa haki za wananchi na utawala wa sheria ni sharti muhimu katika kufikia maendeleo na ustawi wa jamii na taifa, katika kulinda heshima ya taifa, kuhifadhi na kuendeleza heshima ya Wazanzibari na kulinda haki zao. Maridhiano ya Kisiasa yaliyofikiwa Novemba 2009 baina ya vyama vya CUF na CCM vikiwakilishwa na viongozi wake wakuu kwa hapa Zanzibar, Mhe. Dk. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, na kupata ridhaa ya wananchi kupitia Kura ya Maoni tarehe 31 Julai 2010, yamebadilisha kabisa takriban miaka 50 ya siasa za uhasama, chuki na mgawanyiko na kuleta mwelekeo mpya wa kisiasa Zanzibar uliolenga kuleta umoja, maelewano na amani katika nchi.

Pamoja na wananchi na viongozi walio wengi kuyaunga mkono Maridhiano ya Kisiasa yaliyofikiwa, bado wapo viongozi wa kisiasa wanaojaribu kutaka kuyavuruga na hata kuwapotosha wananchi juu ya dhamira halisi za Maridhiano haya kwa maslahi yao binafsi. CUF inaamini kuwa maridhiano si tukio lakini ni mwendelezo wa hatua nyingi zinazochukuliwa kupelekea lengo lake lifikiwe.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na CUF itachukua hatua zifuatazo:-
1.Itaheshimu na kutekeleza kikamilifu mambo yote yaliyokubaliwa kupitia Maridhiano ya Kisiasa ya Wazanzibari.

 Itaendeleza muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa uliyo imara na utakaoshirikisha vyama vyote vya siasa vitakavyopata ridhaa ya Wazanzibari na kuwa na uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi kama ilivyoelekezwa katika Marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar.

 Itaandaa utaratibu wa kuyatekeleza mapendekezo mengine yaliyotokana na Muafaka wa 2001 yakiwemo yale yanayohusu marekebisho mbali mbali katika utendaji wa vyombo vya serikali na pia yanayohusu wananchi waliopata athari mbali mbali za moja kwa moja wakati wa kipindi cha mgogoro wa kisiasa.

 Tutachukua hatua za kuhakikisha kuwa dhamira na utekelezaji wa misingi ya maridhiano yanakwenda hadi ngazi ya chini ya kitaasisi na kijamii.

 Tutatangaza tarehe maalum ya kuadhimisha Siku ya Maridhiano na Umoja wa Kitaifa wa Wazanzibari.

 Itashirikisha wananchi katika kuwepo kwa haja ya kuingiza umuhimu wa mardhinao na umoja wa kitaifa kwa Wazanzibari katika mitaala ya elimu ili kuyaenzi maridhiano haya kwa vizazi vijavyo.

 Itafungua ukurasa mpya wa maelewano kwa kuwataka wananchi wote kusamehe na kusahau maovu yote waliyotendeana katika kipindi cha uhasama wa kisiasa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s