CUF yavuna wanachama kisiwani Pemba

 

Chama Cha Wananchi CUF kimevuna wanachama wapya zaidi ya  mia nane kutoka Wilaya ya Micheweni baadhi yao wakiwa kutoka vyama vya ADC, ACT Wazalendo na CCM.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika viwanja vya skuli ya Micheweni, wanachama 16 ni kutoka ADC, 17 ACT Wazalendo, 40 kutoka CCM na 750 wakiwa wanachama wapya.

Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, alipokea kadi za vyama hivyo na kuwakabidhi kadi za CUF ambapo baadhi ya wanachama wapya walishindwa kukabidhiwa katika hizo baada  ya kumalizika.

Akizungumza katika mkutano huo Maalim Seif alisema wimbi la mabadiliko ni kubwa na hakuna anayeweza kulizuia.

Alisema wakati umefika kwa wananchi kufanya maamuzi ya kuiondosha CCM madarakani katika uchaguzi mkuu ujao, ili chama hicho kiweze kutekeleza sera zake za kuleta mabadiliko.

Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi kinajidanganya ni kisahau kupata jimbo lolote katika kisiwa cha Pemba, kwani wananchi wa Pemba wamekuwa na mwamko wa kutaka mabadiliko na mamlaka kamili.

Kauli hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa CCM kina mpango wa kupata majimbo matatu katika kisiwa cha Pemba bila ya kutajwa majina ya majimbo hayo, na kwamba jambo hilo haliwezekani.

Kuhusu mipango ya maendeleo Maalim Seif amesema anakusudia kuanzisha benki maalum itakayowasaidia wajasiriamali kwa kuwapatia mikopo ili waweze kujiendeleza.

Maalim Seif alitumia fursa hiyo kukemea tatizo la ajira za watoto ambalo linaonekana kuendelea kwa kasi katika Wilaya ya Micheweni.

Amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atapigania maslahi ya Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano na kuikataa kabisa katiba inayopendekezwa ambayo amesema haikuzingatia maoni ya wananchi.

Ameahidi kudumisha ushirikiano kwa nchi jirani za Afrika Mashariki pamoja na jumuiya za kimataifa, ili Zanzibar iendelee kutambuliwa katika Jamii ya Kimataifa.

Amesema suala la ushirikiano wa kimataifa halikuwa katika orodha ya mambo ya Muungano bali liliingiza kinyemela, na kwamba iwapo ataingia madarakani atalishughulikia suala hilo.

Amewataka wananchi wa Micheweni kuepukana na siasa za vurugu, chuki na uhasama, na kwamba siasa za aina hiyo zimepitwa na wakati.

Kabla ya mkutano huo, Maalim Seif alifanya ziara ya kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo ya wajasiriamali katika Wilaya ya Micheweni, na kufungua matawi mapya ya CUF likiwemo tawi la Kwale eneo ambalo lilikuwa ngome kubwa ya Chama Cha Mapinduzi.

Na: Hassan Hamad, OMKR.

 

 

Hussein Al-wahaibi

Recent photos

 

Show details

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s