Ilani ya CUF kuelekea Zanzibar yenye Mamlaka Kamili na Neema Kwa Wote

Imani kubwa ya kihistoria tunayoendelea kupewa kupitia ridhaa ya wananchi inaturejesha tena kwao na mpango kazi uliotayarishwa kuirejeshea hadhi na heshima kwa nchi yetu pamoja na kuleta mabadiliko ya haraka ya kisiasa na kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya jamii nzima na taifa letu kuanzia tarehe 25 Oktoba 2015.

1.Tutayarejesha Mamlaka Kamili ya Zanzibar kwa kuimarisha Muungano utakaozingatia Misingi ya Haki, Usawa na Heshima kwa nchi zote mbili zinazounda Muungano huu.

3. Tutajenga Uongozi Mwema kwa Kuimarisha Misingi ya Uhuru, Haki na Maridhiano kwa wananchi wa Zanzibar.

4. Tutailinda, kuienzi, kuendeleza, kuijenga na kuiboresha misingi yote ya Umoja wetu wa Kitaifa ulioasisiwa na viongozi wetu wa kisiasa wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Amani Karume na Maalim Seif Sharif Hamad tarehe 5 Novemba, 2009 na kupewa ridhaa na wananchi kupitia Kura ya Maoni ya tarehe 31 Julai 2010.

5. Tutapambana kuondosha rushwa, ufisadi, upendeleo, uonevu, ubaguzi na woga ndani ya taasisi zetu pamoja na jamii kwa kurekebisha muundo wetu wa utawala, uwajibikaji, na utendaji katika kazi na utoaji wa huduma sambamba na kupanua viwango vya elimu na uelewa wa kutosha kwa jamii.

6. Tutayaendeleza mashirikiano yetu ya kimataifa (International Relations and Cooperation) na majirani zetu, washirika wa maendeleo, taasisi, nchi wahisani na jumuiya mbali mbali za kimaendeleo kwa lengo la kuifanya Zanzibar inufaike na mahusiano na mashirikiano hayo. Mafanikio ya mashirikiano haya yatatokana na Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani ya muungano wa haki, heshima na usawa.

7. Tutatetea haki ya Zanzibar kushirikishwa katika Shirika la Kimataifa la Bahari (International Maritime Organization) pamoja na kusimamia kwa uwazi na kwa mujibu wa sheria za kimataifa mikataba na itifaki mbali mbali za Shirika la IMO ikiwemo suala la usajili wa meli (International Shipping Registry) na fursa zaidi kwa Wazanzibari katika uajiri melini.

8. Tutasimamia na kuitetea haki ya Zanzibar katika sera, mipango na matumizi ya maeneo maalum ya kiuchumi ya bahari kuu (Exclusive Economic Zone) na yale ya madini ya chini ya bahari (Extended Constinental Shelf) kwa faida ya wananchi wa Zanzibar.

9. Tutaingia kwenye uongozi tukiwa na dira ya mabadiliko itakayotupeleka kujenga mashirikiano ya kikanda katika sekta ya uvuvi wa bahari kuu (Regional Deep Sea Fisheries Management).

10. Tutauondoa uonevu na ukiritimba unaofanywa na viongozi na watendaji wachache juu ya haki za msingi za wavuvi wetu wa mwambao na kuhakikisha haki na usawa kwa wavuvi wote ikiwemo wazalishaji wa mwani.
11. Tutahakikisha tunapiga hatua kubwa mbele katika kuijenga nchi, uchumi na jamii yenye fursa ya maendeleo yanayoongozwa na sayansi na teknolojia yakiwemo matumizi endelevu na ya gharama ndogo kwa wananchi ya teknolojia ya taarifa na mawasiliano (Information and Communications Technology).

12. Tutasimamia sera, sheria, na mfumo wa uendeshaji bora wa sekta ya mafuta na gesi (Oil and Gas for Development) ikiwemo ugawaji wa mipaka ya baharini, utafutaji, uzalishaji na mapato yanayotokana na maliasili hizo na kuhakikisha ajira na maslahi kwa wananchi wa Zanzibar.

13. Tutausimamia na kuuendesha uchumi utakaozingatia malengo ya Uchumi Endelevu (Sustainable Development Goals) inayozingatia vipaumbele kwa nchi za visiwa vidogo vidogo na kuendeleza mashirikiano na washirika wetu wa maendeleo katika kufikia malengo hayo.

14. Tutajenga uchumi imara unaokua kwa kasi na unaotoa ajira na tija kwa misingi ya haki na uwiano kwa wote.

15. Tutahakikisha upatikanaji wa ajira kwa wananchi wetu katika sekta zote za kiuchumi za utalii, kilimo, uvuvi, biashara, viwanda, na kukuza huduma za ujasiriamali kwa ajili ya sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi.

16. Tutaunga mkono na kuusimamia utalii endelevu (Sustainable Tourism) unaojali maslahi ya wananchi, na sio viongozi tu, na kuhakikisha uwiano baina ya wawekezaji na wananchi wa maeneo husika katika utoaji wa huduma za maji, nishati, matumizi ya ardhi, ajira, na fursa nyingine za sekta hii.

17. Tutakuza biashara kwa kupunguza viwango vya ushuru na kodi na kuitangaza Zanzibar kuwa Bandari Huru sambamba na kuimarisha viwanda na miundombinu ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi na makaazi, barabara, umeme, maji mawasiliano ya simu, bandari na viwanja vya ndege vya kisasa.

18. Tutaendeleza uzalishaji wa zao la karafuu na usimamizi endelevu wa sekta hii na kutekeleza programu za ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji wa mpunga na miwa katika mabonde yetu.

19. Tutaunga mkono na kushirikiana na wawekezaji na wananchi kuharakisha huduma mbali mbali muhimu (Service Providers) katika uzalishaji wa mazao mbali mbali ya chakula na biashara yakiwemo matunda, mboga mboga, na nafaka kwa ajili ya maslahi ya wananchi.

20. Tutaanzisha Benki ya Uwekezaji ya Zanzibar (Zanzibar Investment Bank) pamoja na kuunda mazingira bora ya kisera na kisheria katika uwekezaji wa mabenki ya kimataifa (Offshore Banking) na makampuni ya kimataifa (Offshore Companies).

21. Tutaufanyia marekebisho ya kitaasisi na kiuendeshaji mfumo mzima wa utoaji wa elimu Zanzibar ili uende sambamba na haja ya kutoa elimu bora na yenye viwango vya kikanda vya Afrika Mashariki na vya kimataifa itakayokuza vipaji na vipawa vya wanafunzi wetu na kuwafanya waweze kushindana katika soko la ajira la kikanda na kimataifa.

22. Tutaboresha maslahi ya wafanyakazi na kuongeza kima cha chini cha mishahara kwa kiwango cha kutosheleza mahitaji pamoja na kuhakikisha maslahi zaidi na bora kwa wastaafu (Pensioners) na wazee (Senior Citizens).

23. Tutawekeza zaidi katika usimamizi bora, upanuzi wa miundombinu, pamoja na viwango vya uhakika vya huduma katika sekta ya afya kwa ajili ya wananchi wetu na kuifanya iwe sekta bora na iliyoimarika.

24. Tutaendelea kupambana na Malaria, UKIMWI, ugonjwa wa presha, moyo, kisukari, kansa, na maradhi mengine yanayoambukiza, yaliyodharauliwa na yasiyoambukiza.

25. Tutapambana vikali na janga la dawa za kulevya kwa kuhakikisha uimarishaji ulinzi na usalama katika viwanja vya ndege.
na bandari zetu, viwango na miundombinu bora katika upekuzi na upelelezi, huduma bora za tiba kwa walioathirika na dawa za kulevya pamoja na elimu ya jamii kuhusu madhara yake.

26. Tutasimamia hifadhi ya mazingira yetu pamoja na kuijenga jamii iliyo tayari na uchumi wenye uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi (Climate Change Adaptation).

27. Tutawekeza katika mipango ya maendeleo ya uchumi na maendeleo ya jamii inayojali utayari wa kujikinga na hatari za majanga ya kimaumbile (Disaster Risk Reduction).

28. Tutatengeneza mpango kazi wa kuanzishwa kwa miundombinu ya kitaifa ya nishati mbadala (Renewable Energy) ikiwemo ya jua, upepo, takataka na biogas itakayochangia katika suala zima la mageuzi katika sekta ya nishati Zanzibar.

29. Tutahakikisha kuwa hifadhi zote za misitu zinalindwa na kuhifadhiwa pamoja na kushajiisha matumizi endelevu ya misitu.

30. Tutatunga sera na sheria mpya za usimamizi wa hifadhi za baharini (Marine Conservation Areas) na kuweka mipaka maalum (zonation) katika matumizi ya maeneo haya ya bahari kwa ajli ya wavuvi, watalii, na shughuli nyingine.

31. Tutaondoa kodi zote kandamizi zinazouathiri utalii wa hifadhi za mazingira na kuweka viwango vipya vya kodi vinavyokubalika kwa maslahi na faida ya wahusika wote.

32. Tutahakikisha utekelezaji kwa ukamilifu wa matamko yote ya kimataifa kuhusiana na haki, wajibu, na dhamana za taifa na jamii kwa wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu.

33. Tutaendelea kuuthamini utamaduni na urithi wetu wa kihistoria (Culture and Heritage) na kusaidia katika kukuza malezi bora kwa vijana wetu pamoja na utunzaji wa wazee wetu.
34. Tutatilia mkazo katika uwekezaji na uimarishwaji wa michezo mbali mbali na kutoa fursa kwa vijana wetu katika ngazi zote za ushirikishwaji katika michezo yote.

35. Kwa ridhaa ya wananchi, tutahakikisha tunaiongoza Zanzibar yenye Mamlaka Kamili na inayotoa fursa, haki, na usawa kwa lengo la kujenga nchi yenye neema kwa wote ndani ya Muungano wa haki, heshima na usawa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s