Maalim Seif: Wananchi musikubali vitisho vya dola, wenye dola ni nyinyi wenyewe

Mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukwa), Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka wananchi wa Zanzibar kutokubali vitisho vya dola vinavyotolewa na viongozi wa CCM kwani wenye dola ni wananchi wenyewe.

“Wapo viongozi wa CCM wanaowatisha wananchi kwa kutumia dola, nawambia musitishike kwani wenye dola ni nyinyi wananchi wenyewe” Alisema Maalim Seif.

Maalim Seif ambaye alikuwa akiwahutubia wananchi wa majimbo ya Donge, Kiwengwa na Mahonda katika uwanja wa Mwanakombo nje kidogo ya mji wa Unguja ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya kampeni inayofanywa na chama cha CUF, aliwataka wananchi hao kuwachagua viongozi watakao tetea maslahi ya Zanzibar.

Akitolea mfano kupitia bunge Maalum la Katiba, mgombea huyo aliwataka wananchi wa Zanzibar kuacha kuwachagua viongozi wa CCM kwani hawana uzalendo na Zanzibar kutokana na kile alichosema kuwa viongozi hao walishiriki kuiangamiza Zanzibar kwenye mchakato wa kupata katiba mpya.

Hata hivyo Maalim Seif ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa rais aliwahakikishia wananchi kuwa endapo watamchagua kuwa rais wao atatumia wiki moja tu baada ya kuapishwa kuwarudisha Mashekhe waliowekwa kwenye magereza ya Tanzania bara.

“Mahakama kuu ya Zanzibar ina mamlaka sawa na Mahakama kuu ya Tanzania bara, Mukinichagua, nitahakikisha mashekhe wetu wanarudishwa Zanzibar na kuhukumiwa kwenye mahakama ya Zanzibar” Aliongeza.

Aidha alisema atahakikisha anaimarisha usalama kwa Wazanzibari ili waweze kuishi kwa amani katika nchi yao.

Maalim Seif alitumia muda huo kuwaombea kura kwa wananchi wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani wa majimbo ya Donge, Kiwengwa na Mahonda.

Wagombea kwa upande wa jimbo la Donge ni Kombo Mohammed Kombo (Ubunge), Salim Khamis Malik-Uwakilishi, Hussein Kassim Shehe-Udiwani wodi ya Mkataleni na Shaame Haji Machano- Donge vijibweni.

Katika jimbo la Kiwengwa, wagombea walikuwa ni Nassor Mohammed Rashid- Ubunge, Hassan Khatib Kheir- Uwakilishi, Abubakar Ali Suleiman- Udiwani wodi ya Kiwengwa na Khamis Haji Hemed- Udiwani wodi ya Mbaleni.

Wagombea katika jimbo la Mahonda, ni Suleiman Ahmed Suleiman-Ubunge, Mwinsheha Shehe Abdalla- Uwakilishi, Machano Omar Masanja- Udiwani wodi ya Mahonda na Salim Abdalla Salim- Udiwani wodi ya Fujoni.

Kwa upande wake msaidizi meneja kampeni, Mansour Yussuf Himid amewaeleza wananchi juu ya umuimu wa maridhiano ya Kitaifa na hivyo wakatae viongozi ambao wanahubiri chuki na siasa za kibaguzi kwani hazina tija katika kujenga mustakbali mwema kwa Zanzibar.

Mansour ambaye pia ni mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Chukwani amesema wakati umefika sasa kwa Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili ili iweze kujiendeleza kiuchumi.

“Mamlaka kamili kwa Zanzibar yanaumuhimu mkubwa sana, kwani ndiyo msingi wetu wa uchumi kwa nchi yetu” Alisema Mansour.

Pia aliwataka wananchi kumuunga mkono Maalim Seif kwani ni kiongozi mwenye dhamira ya dhati katika kuwaletea Wazanzibari Maendeleo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s