Lowassa apeta Zanzibar

Ilikuwa ni majira ya saa 5:30 asubuhi hapo ambapo mgombea wa urais kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa aliwasili katika Uwanja wa ndege wa hayati Abeid Amani Karume hapa visiwani Zanzibar.

s47

Katika kuwasili kwake Edward Lowasasa, alilakiwa na na mwenyeji wake ambaye ni Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sarif Hamad. Miongoni mwa viongozi wengine walioambatana naye kwenye msfara huo, ni wenye viti wote wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) akiwemo James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Emmanuel Makaidi wa NLD, Freeman Mbowe wa CHADEMA na Twaha Taslima ambaye anakaimu nafasi ya uwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF ambayo ilikuwa wazi mara baada ya kujiuzulu kwa Profesa Ibraaim Lipumba.

Hali ilivyokuwa

Kabla ya kuwasili kwa mgombea wa Chadema na Ukawa, Ndugu Edward Lowassa askari walizingira katika maeneo tofauti ya uwanja wa ndege ili kuakikisha maandamano hayafanyiki na hali ya usalama inadumishwa. Wapenzi na wafuasi wa vyama vinavyounda umoja huo walionekana kutekeleza kile kinachoitwa “Tii Sheria bila ya ushuruti” kwa kukaa kwa uvumilivu bila ya fujo lolote ambalo lingesababisha polisi hao kufyatua mabomu ya machozi.

Mara baada ya msafara kuanza, vifijo na nderemo vilianza kurindima. Ulikuwa ni msafara wa gari zisizopunua hamsini. Kando ya barabara ambayo msafara huo ulikuwa ukipita, maelfu ya wanachama na wafuasi wa vyama hivyo walijipanga pembezoni mwa barabara na kumpigia makofi huku huku wakisema “Raisi! Raisi! Raisi!”.

Wako walioziacha kazi zao majumbani na kuja barabarani ili kumshuhudia mgombea huyo. Vijana kutoka katika jamii ya kimasai walijipanga barabarani pia na kuupigia saluti msafara huo, ikiwa ni ishara ya heshima na imani kubwa waliyonayo kwa Edward Lowasa. Binafsi nilishuhudia baadhi ya watu wakipigana vikumbo vya hapa na pale ili angalau waweze kumuona mgombea huyo wa uraisi kupitia Chadema na Ukawa.

Magari ya msafara yalilazimika kutembea kidogo kidogo ili kutoa fursa kwa wanachama na wapenzi mbali mbali kushuhudia.

Akiwasili katika uwanja wa Kibanda Maiti

Mara baada ya dakika kama ishirini hivi, msafara uliwasili katika kiwanja cha demokrasia Kibandamaiti. Ardhi ilitetemeka na anga likasema kutokana na vifijo na nderemo vilivyorindima mara baada ya msafara wa Lowassa kuwasili kiwanjani hapo. Watu walijipanga mstari mmoja kila upande na kuacha nafasi katikati ili gari zipite kuelekea uwanjani hapo.

Punde tu magari yakasimama na viogozi nao wakiongozwa na Maalim Seif na Edward Lowassa  walishuka na kuelekea katika nafasi zao walizoandaliwa na timu nzima ya itifaki.

Mgeja chupu chupu kuchinjwa

Katika hali isiyotarajiwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja ambaye hivi juzi tu alijiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alidai kuwa chama cha CCM kilishawai kumtishia maisha kwa kutaka kumchinja, jambo ambalo limepelekea yeye kuanza kutokuwa na imani na chama hicho.

Akielezea sababu za kutaka kuchinjwa kwake, mgeja alisema kuwa ni kutokana na mapendekezo yake ambayo aliyatoa katika kikao cha halmashauri kuu (NEC) ambapo alipendekeza kuwa  Rais asiteuliwe kuwa Mwenyekiti wa CCM.  Hali hiyo ndiyo iliyopelekea hadi akatishiwa maisha.

Pia Mgeja aliongezea kuwa kitendo cha Ndugu Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kuwa mgombea mwenza, ilikuwa ni zawadi ambayo kada huyo wa CCM alipewa kufuatia mchango wake mkubwa alioutoa kwa kufanikisha kuiangamiza Zanzibar Kwenye bunge maalum la katiba.

Viongozi wa CCM kupelekwa The Hague

Katika hatua nyengine, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi na Mgombea ubunge wa Jimbo la Vunjo James Mbatia amesema tayari wamesawatuma wmawakili wao waandike maovu yote wanayofanyiwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ili baadae wayapeleke katika mahakama ya ICC huko The Hague.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Mbatia alisema CCM wameingia choo cha kike kwani wanachi kutoka Tanzania bara ambao waliandikiswa kwa matakwa ya CCM ili baadae waipigie kura chama hicho, wote wamehamia Ukawa. Kumekuwa na tabia ya Chama Cha Mapinduzi kuwapatia fursa ya kujiandikisha vijana kutoka Tanzania ili baadae wawapigie kura CCM lakini katika hali ya kile kinachoitwa “Wakati wa Mabadiliko” vijana hao wamejiunga na Ukawa.

Aidha Mbatia alisisitiza kwa kuitaka tume ya uchaguzi kuakikisha wanendesha uchaguzi ulio huru na wa haki ili kwani kutokufanya hivyo amani hiyo haitokuwepo.

Mbowe asema Ukawa upo Ngangari

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ukawa umepitia katika majaribio mengi na changamoto kadhaa, wengine walishindwa kuzikabili changamoto hizo na wakaachia njiani.

Amesema kuna kila sababu ya kubadilisha mfumo wa kiutawala nchini kwani hali za wananchi zinaendelea kuzorota siku hadi siku hivyo amewataka watanzania bara wanaoishi Zanzibar kuakikisha wanamuunga mkono Maalim Seif na Edward Lowassa ili watimize azma yao ya kuin`goa CCM madarakani.

Akifafanua kuhusu vyombo vya ulinzi na usalama, Mbowe alisema kuwa vyombo hivyo hususan bara vinatumika vibaya kupora demokrasia nchini. Hivyo amevitaka vyombo hivyo kuhakikisha wanalinda usalama wa raia na sio kuwashambulia kwa kuwapiga na kuwafyatulia mabomu ya machozi.

Maalim Seif Atoa ya moyoni

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, aliweka wazi kuwa Chama Cha Mapinduzi kimeanza kuvuruga amani ya nchi kufuatia kutekwa na Majanjaweed kwa mgombea wa Ubunge wa jimbo la Shaurimoyo, Abdi Seif Hamad. Aidha majanjaweed hao pia walimnyan`ganya fomu zake za ubunge hapo jana.

Maalim Seif alisema imekuwa ni kawaida ya Chama Cha Mapinduzi kuvuruga amani ya nchi licha ya wao (CCM) kuwa wahubiri wakubwa wa amani hiyo hasa pale unapokaribia uchaguzi mkuu.

Vile vile aliwaakikishia maelfu ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo kuwa wataiondoa CCM madarakani ifikapo hapo Agosti 25.

Lowassa awakuna Wazanzibari

Katika kile kilichoonekana kuwakuna maelfu ya Wazanzibari waliohudhuria katika mkutano huo, Lowassa aliwahakikishia wananchi hao kuwa atasimamia misingi ya ya rasimu ya katiba ya Jaji Joseph Sinde Warioba iliyo chini ya serikali tatu ili kuweza kuleta katiba bora ambayo itaheshimu maoni ya wananchi.

Hata hivyo aliongeza kuwa atahakikisha mashekhe wa Kizanzibari walioko katika magereza ya Tanganyika wanapata haki zao katika muda stahiki. Hatua hiyo iliibua hamasa kubwa kwa wanachi hao na kuendelea kumshangiria mgombea huyo kwa kumwita Raisi! Raisi! Raisi!.

Lowassa aliwataka wananchi hao kuzitunza kadi zao za kupigia kura ili itakapofika oktoba 25 waweze kuin`goa CCM madarakani.

Mkutano wa Edward Lowassa visiwani Zanzibar, ni muendelezo wa mikutano  yake mengine ya kutafuta wadhamini ambao watamuunga mkono katika harakati zake za kuwania uraisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Mikutano mengine iliyofanywa na Lowassa ni pamoja na ile iliyofanyika mkoani Mbeya, Arusha, na Mwanza.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s