CUF yatangaza wagombea wa majimbo mapya

Chama cha Wananchi (CUF) kimetangaza wagombea wa nafasi ya ubunge na uwakilishi kwa majimbo 54 ya uchaguzi kwa nafasi na uwakilishi na majimbo 50 kwa nafasi ya ubunge huku kikiwatema vigogo wake, Muhammed Habibu Mnyaa na Rajabu Mbarouk kufuatia hatua ya ugawaji mpya wa mipaka ya majimbo uliofanywa na Tume ya Uchaguzi (ZEC).

Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango, Omar Ali Shehe, akitangaza majina ya wagombea kwenye ofisi za CUF, Vuga, Zanzibar siku ya Ijumaa tarehe 8 Mei 2015.

Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango, Omar Ali Shehe, akitangaza majina ya wagombea kwenye ofisi za CUF, Vuga, Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Vuga mjini Unguja, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, amesema baada ya ZEC kufanya mabadiliko ya mgawanyo wa majimbo na kuongeza majimbo manne mapya, chama hicho kililazimika kufanya mabadiliko ya wagombea wa majimbo.

“Ni kweli kuwa Mheshimiwa Muhammed Habibu Mnyaa na Rajabu Mbarouk waliteuliwa na Baraza kuu lakini ilikuwa ni kabla ya makato ya majimbo. Baada ya ukatwaji upya wa majimbo ilipelekea jimbo moja kuwa na wagombea wanne. Kwa mfano katika jumbo la Mkoani na Mkanyageni lilikuwa na wagombea wawili wa uwakilishi na wawili wa ubunge, sheria haikubali kuwa na wagombea wanne, kwa hivyo ilibidi tupate mgombea mmoja wa uwakilishi na mmoja wa ubunge na hivyo wengine ikapelekea wengine kuachwa,” alisema.

Baraza Kuu la CUF lilirejesha majina ya Mnyaa na Rajab Mbarouk kabla ya ZEC kutoa ripoti ya mapitio na mgawanyo wa majimbo ambapo ilipelekea wanachama hao majimbo yao kugawanywa.

Alisema baadhi ya wagombea waliogombea majimbo ya zamani na sasa yamebadilishwa majina wamewapa majimbo hayo yaliyobadilishwa majina na kuwaongeza wagombea wanne kwa majimbo mapya kwa nafasi za uwakilishi.

Akizungumzia utaratibu uliotumika wa kuwapata wagombea wagombea wa majimbo mapya,Shehe alisema jana kuwa wamefuata katiba ya chama ambayo inaruhusu kufanya mabadiliko katika hali ya dharura.

Waliobadilishwa majimbo baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutaja majina mapya kwa baadhi ya majimbo ni Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu (sasa Malindi) wakati ni Ali Saleh aliyekuwa anagombea ubunge Mji Mkongwe (sasa Malindi).

Wengine ni mwakilishi wa jimbo la Mtoni, Nassor Ahmed Mazrui amepelekwa jimbo la Mtopepo, Mansour Yussuf Himid uwakilishi jimbo la Chukwani badala ya Kiembe Samaki na Abdillahi Jihadi Hassan uwakilishi jimbo la Mwanakwerekwe badala ya Magogoni.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s