Taslima aitabiria mazuri CUF

Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), Twaha Taslima, amesema chama hicho kitaendelea kuwa imara licha ya mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba, kujiuzulu.

Wafuasi wa CUF

Wafuasi wa CUF

Kadhalika, amesema watu wasijiingize kwenye siasa kwa ajili ya kutafuta manufaa yao ya kiuchumi bali waiingie kwenye siasa kwa lengo la kusaidia kuimarisha uchumi wa nchi.

Alisema hayo jana katika mahojiano maalum na Nipashe kuhusu utekelezaji wa mikakati iliyopangwa na kamati hiyo katika kuhakikisha chama hicho ambacho ni moja ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Baraza Kuu la CUF Jumapili iliyopita liliunda kamati ya watu watatu ambao ni Taslima (Mwenyekiti), Abubakar Khamis Bakary na Severina Mwijage kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kikatiba yaliyopaswa kufanywa na Prof. Ibrahimu Lipumba, aliyejiuzulu nafasi hiyo wiki iliyopita.

Prof. Lipumba alijiuzulu kwa madai kuwa alichukua hatua hiyo kutokana na kuonekana kuwa kikwazo katika baadhi ya mambo ndani ya CUF na dhamira yake kumsuta kufuatia hatua ya Ukawa kumpokea na kumpa nafasi ya kugombea urais Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Baada ya kujiuzulu, Prof. Lipumba alikwenda Rwanda kwa maelezo kuwa amekwenda kufanya utafiti.

Taslima alisema wanasiasa wanalo jukumu la kusaidia kuimarisha uchumi wa nchi, hivyo halitakuwa jambo la afya inapotokea mtu anatumia nafasi yake ya kisiasa kujinufaisha.

Alisema katika kipindi cha miezi sita ambacho kamati hiyo itakuwa madarakani, itahakikisha wanachama wa CUF waliopo hawaondoki na kufanya mikakati ya kuwaingiza wanachama wapya.

Aliongeza kuwa kamati hiyo itahakikisha CUF inashiriki vyema katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kushirikiana na Ukawa ili kuibuka na ushindi.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alisema juzi kuwa Baraza Kuu la CUF limeteua kamati hiyo, ambayo itatayarisha taarifa fupi ya kazi ilizozitelekeza na kuwasilisha kwa baraza hilo.

Kwa mujibu wa Katiba ya CUF, mwenyekiti anapojiuzulu au kupotea nafasi yake kwa njia nyingine, nafasi hiyo inajazwa baada ya kipindi cha miezi sita.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s