Ni wazi, CCM ya Kikwete haiwezi kutoa raisi bora

Siku mmoja Socrates aliwasha mishumaa mia moja mchana na akachukua meza na kwenda kukaa kwenye njia panda. Mtu wa kwanza akapita, akamshangaa na kutikisa kichwa tu akaenda. Socrates akazima mshumaa mmoja. Watu wakawa wana pita na kumshangaa na baadae wanaenda zao na kila aliyepita na kushangaa Socrates alizima mshumaa mmoja.

Rais Jakaya Kikwete.

Rais Jakaya Kikwete.

Alipofika mtu wa mia moja, ndipo huyo mtu akamwuuliza, “Wewe Socrates mbona umewasha mishumaa na umekaa hapa njia panda ?” Socrates akajibu, “Pamoja na kiwango kikubwa cha elimu mlichofika, bado watu wengi wa Athens hamna tabia ya kudadisi matukio yanayotokea kwenye jamii yenu, watuweni mna tabia ya kushangaa na kusubiri matokeo. Hivyo watu wengi hawatumii muda mwingi kuchunguza jambo na kutoa majibu sahihi kwa jambo hilo. Umeona kati ya watu mia moja, asilimia moja tu ndiyo watu wanaoweza kudadisi jambo linapotokea katika jamii wakati asilimia tisini na tisa hushangaa tu” Baada ya kuwaambia hayo alizima mishumaa yake na akaondoka pale njia panda.

Ili jamii ifikie mabadiliko na mafanikio ya kweli ni lazima jamii hiyo ivunje vunje ile minyororo ya kifikira ambayo imewakamata baadhi ya wananchi katika jamii kiasi kwamba hawawezi kuchunguza na kuhoji mambo yanayotokea katika jamii hiyo na hatimaye kufikiri tofauti.

Mwaka 1995 Bejamini William Mkapa aliteuliwa na CCM kuwa mgombea urais. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alimpigia kampeni kali na alimnadi Bwana Mkapa kama mtu safi, Mr Clean. Mwaka huo wa uchaguzi upinzani ulikuwa bado ni mchanga lakini tayari upepo wa mabadiliko ulikuwa umeeanza kuvuma kwani tayari watanzania walikuwa wameonyesha kuanza kuichoka CCM. Kwa ushawishi wa Mwalimu Nyerere CCM ilishinda na Mkapa akaapishwa kuwa Rais wa awamu ya tatu.

Katika kipindi cha Mkapa aliyepigiwa kampeni ya kwamba alikuwa ni msafi, mtakumbuka ufisadi mwingi ulijitokeza. Tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa Rada, tuhuma za wizi wa fedha katika Akanti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT – chombo nyeti kwa uchumi), Kashfa ya Deepgreen, uuzaji wa nyumba za serikali. Matokeo ya kashfa hizi ilisababaisha Tanzania kuanza kushuka chati kiulimwengu katika rushwa na uadilifu. Kwa nini Mkapa aliyekuwa mtu safi serikali yake ilikumbwa na kashfa lukuki katika utawala wake na watanzania tunajifunza nini ?

Chama Cha Mapinduzi ni taasisi yenye mfumo wake. Narudia, Lakini tangu mwaka 1995 kumetokea mabadiliko makubwa ndani ya CCM. Narudia kueleza, matatizo ndani ya CCM yalianza baada ya wafanyabiashara kujiunga kwa wingi na CCM kama wafadhili na baadaye kupata nafasi za uongozi ndani ya chama na hatimaye serikalini. Hali hii ilianza kujitokeza kwa nguvu mwaka 1995 kwa wafanyabiashara wengi kujiunga na CCM na baadaye kugombea ubunge na hatimaye kupata nafasi za uongozi.

Baada ya wafanyabiashara kuingia kwenye serikali, ndipo ubadhirifu mkubwa au ufisadi ulianza kutokea na kushamiri
Kutokana na umri wa CCM kuwa mkubwa watu wengi wenye kasoro, wasiofaa, wasio na maadili, wala rushwa wamejiingiza ndani ya CCM na kukichafua. CCM imekuwa kama kokoro. Kokoro wakati mwingine hubeba viumbe visivyohitajika. Ndani ya CCM sasa kuna watu wa ajabu sana . Katika hili kokoro la CCM kumevutwa samaki wazuri na wabovu, vigae na maganda ya minazi, minofu na mapanki. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema “CCM kwa sasa ni kivuko kuelelekea kupata madaraka na utajiri,hivyo si hatari kwa chama chenyewe tu bali kwa mustakabali wa nchi hii kwa kuwa CCM ndio chama tawala. Kwa kifupi mfumo wa CCM ni mbovu, umeoza. Ni mfumo wa kulindana.
Nina amini, moja ya sababu ya Mkapa aliyekuwa msafi lakini serikali yake ilikumbwa na kashfa nyingi za ufisadi ni kutokana na mfumo mbovu na mfumo uliooza wa CCM.

Hivi karibuni Chama cha Mapinduzi kimefanya uteuzi wa mgombea urais, John Pombe Magufuri. CCM imeanza kuwaaminisha watanzania kwamba wametoa chaguo bora kwa sababu John Pombe magufuli hana kashfa ni mtu safi. Mkapa alikuwa mtu safi lakini kwa kuwa alikuwa kwenye Chama ambacho mfumo wake ni mbovu alibadilika na hivyo katika utawala wake ufisadi mkubwa ukaanza kutokea.

Tukumbuke pia, rais wa awamu ya nne aliingia madarakani kwa hamasa kubwa akibeba matumaini na matamanio ya mioyo ya watanzania. Utawala wake ulikuja na kila ahadi za kurudisha utukufu wa Taifa hili ikiwemo maisha bora kwa kila mtanzania. Maisha bora ambayo yangepatikana kwa kasi mpya na nguvu mpya. Lakini Kikwete anawacha watanzania katika masha duni zaidi. Sababu kubwa iliyosababisha ashindwe kutekeleza ahadi zake ni mfumo mbovu wa chama chake CCM. CCM inakumbatia matajiri na wafanyabiashara. CCM imepoteza dira na imeacha itikadi yake ya kutetea wanyonge, masikini, wakulima na wafanyakazi.

Wapare wana msemo unaosema, “Ukitaka kuepuka nzi, tupa kibudu au mzoga”. Nzi hufuata harufu ya mzoga. Mtu yeyeote aliyemsafi lakini akawa amebeba mzoga lazima inzi wamfuate. CCM imechafuka, ina harufu ya ufisadi, rushwa nakadhalika. John Pombe Magufuli aliyeibeba bendera ya CCM ni dhahiri anayo harufu ya mzoga, CCM. Lakini lililo mhimu zaidi, Serikali ya John Pombe Magufuli kama watanzania watamchagua haiwezi kutoa uongozi totauti na serikali ya Mkapa kwa sababu Magufuli yuko ndani ya mfumo wa CCM. Magufuri ni chupa mpya lakini mvinyo ni ile ile.

Nawaasa Watanzania, ngonjera za CCM; maisha bora kwa kila Mtanzania, Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya, Ari zaidi, nguvu zaidi, na kasi zaidi, na baadae kujivua gamba hazitaleta mabadiliko yoyote kwa maisha yetu. Bila kufanywa mabadiliko katika mfumo wa kifisadi, unaokumbatia rushwa katika kupata viongozi, taifa letu halitanusurika. CCM imeshindwa kufanya mabadiliko ya kweli. Watanzania wasitegemee uongozi tofauti chini ya ya John Pombe magufuli.

Naomba niwatahadharishe watanzania, mtu kuumwa na nyoka yule yule mara tatu kwenye shimo lile lile ni uzembe uliopitiliza. Tuwe wadadisi kama Socrates alivyo waasa wananchi wa Athens. Ili jamii ifikie mabadiliko na mafanikio ya kweli ni lazima jamii hiyo iuvunje vunje ile minyororo ya kifikira ambayo imewakamata baadhi ya wananchi katika jamii kiasi kwamba hawawezi kuchunguza na kuhoji mambo yanayotokea katika jamii hiyo na hatimaye kufikiri tofauti.

Ili Tanzania ifikie mabadiliko na mafanikio ya kweli ni lazima tuvunje vunje ile minyororo ya kifikira ambayo imewakamata baadhi ya watanzania kiasi kwamba hawawezi kuchunguza na kuhoji mambo yanayotokea na hatimaye kufikiri tofauti. Watanzania tufikiri tofauti, kwamba John Pombe Magufuli akiwa ndani ya CCM hawezi kuleta mabadiliko chanya kwa sababu yuko ndani ya CCM ambayo si madhubuti tena, na imeyumba. CCM haiwezi kutoa rais bora tena kutokana na mfumo wake mbovu. Tatizo kubwa la Tanzania ni mfumo mbovu uliojengwa na CCM ndani ya serikali.

Aidha, niwakumbushe tena aliyowahi kusema mwanafalfasa nguli Albeit Einstern, “Ni ujinga kudhani kwamba unaweza kutumia watu wale wale walioiangusha taasisi kuiinua taasisi hiyo. Maana yake, akili iliyotengeneza tatizo, kamwe akili hiyo hiyo haiwezi kutumika kupata jawabu la tatizo hilo. CCM haitaweza kuleta mabadiliko ya kweli kwani ni chanzo cha kuayumba kwa Taifa letu. CCM ni taasisi ina mfumo wake. Ni muhimu watanzania waungane kuindoa CCM kwanza. Ccm ya Kikwete haiwezi kutoa rais bora.

CCM mara kadhaa imefanikiwa kuwadanganya watanzania. Lakini ikumbuke kwamba, unaweza kuwadanganya watu wachache wakati wote, na unaweza kuwadanganya watu wote kwa muda, lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote. Watanzania wamebadilika, hawadanganyiki wanatambua kwamba CCM hii ndiyo iliyolifikisha Taifa letu mahali lilipo sasa.

Jambo la pili ambalo linasemwa chini chini ni kwamba watanzania wa kanda ya ziwa wampe kura John Pombe Magufuli kwa sababu tu anatoka kanda hiyo. Watanzania naomba tuzingatie, hatumpeleki mtu Ikulu kwenda kutambika. Tunampeleka mtu Ikulu kwenda kuwatumikia watanzania wote. Lakini hata hivyo, tukiwa wakweli, kabila lake John Pombe Magufuli siyo msukuma, wala siyo mkerewe, wala siyo msunva. Kabila lake halisi na la kweli ni CCM damu. Na CCM ni kabila ambalo haliwezi tena kutoa rais bora. Mimi sina tatizo na John Pombe Magufuli, tatizo langu kubwa ni kabila lake la kweli na halisi, ambalo ni CCM.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s