CCM wamezowea vya kunyonga, vya kuchinja hawaviwezi

Mtu ambaye katika maisha yake yote anapenda dhuluma, basi ni vigumu kuibadili tabia hiyo. Tabia hiyo ndio waliyonayo wanachama na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao sisi Waswahili husema wamezoea vya kunyonga, vya kuchinja hawaviwezi. Dhuluma, wizi, rushwa na ubabe ndiyo itikadi ya chama chao.

Picha hii iliyotumwa kwenye mtandao wa Facebook wa kijana wa CCM anayejiita  Boscó Ône Twëlve wa Zanzibar ina maelezo haya:

Picha hii iliyotumwa kwenye mtandao wa Facebook wa kijana wa CCM anayejiita Boscó Ône Twëlve wa Zanzibar ina maelezo haya: “Kataa kupiga kura bila ya chóchóte ki2.. wapiga kura lazima wathaminiwee sio munakwênda kupangishwa mafoleni utadhani madumu ya maji kule Ifakara !!
haiwi Mapenz na ndio starehe yko mwnyeo bac lazma hela iwepo’ itakuw kupga kura manufaa ya mwengine ??? “Kura bila ya pesa haiwezekani”

CCM kimehitimisha kwa sehemu kubwa mchakato wa kupiga kura za maoni kwa wagombea wa urais, ubunge, uwakilishi, na udiwani. Lakini tangu mwanzo hadi mwisho, kilichodhihirika ni hila, rushwa na uchakachuaji wa kura katika maeneo tofauti ya vituo vya kupigia kura.

Licha ya CCM kujinadi kuwa ni chama chenye uadilifu na kinachofuata misingi ya kidemkrasia na utawala wa sheria unaopingana vikali na rushwa, lakini chama hicho kimejikuta kikikumbwa na aibu ya mwaka kwenye kura za maoni, hasa za kuanzia tarehe 1 Agosti. Aibu iliyoje! Wagombea wanatafuta madaraka kwa udi na uvumba.

CCM, ambayo viongozi wake husimama majukwaani na kuwadanganya wananchi kuwa wanaendesha chama chao kwa kuzingatia misingi aliyowaachia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, sasa haina pa kuuweka uso wake. Kwa sababu hawawezi kusema ikiwa rushwa, wizi na ubabe ndiyo misingi waliyoachiwa na muasisi huyo. Hapo zamani, walikuwa wakitumia uelewa mdogo wa wananchi kuficha maovu yao, lakini sasa kasi ya mawasiliano imewaumbua.

Katika uchaguzi wa juzi ambao ulifanyika Tanzania nzima, Bara na Zanzibar wagombea wa CCM walionekana wakitoa rushwa ya waziwazi kwa wapiga kura wao bila ya hata chembe ya aibu. Kuna ushahidi wa kura kununuliwa baina ya shilingi 50,000 hadi 1,500 tu. Ujinga ulioje!

Zaidi ya hayo, katika uchaguzi huo uchakachuaji wa kura ulikuwa hauna mfano. Kura ambazo tayari zilikuwa zimeshawekwa alama za “NDIYO” zilikutikana kwenye vituo kadhaa vya kupiga kura, Bara na Zanzibar. Kwa mfano, katika jimbo la Tarime mjini na vijijini, karatasi zaidi ya 20,000 zenye alama ya “NDIYO” zilikutwa zikiwapa ushindi Waziri wa Kazi na Ajira, Bi Gaudensia Philipo Nyirabu (Tarime mjini) na Nyambari Nyangwine wa Tarime Vijijini kwa mujibu wa gazeti la Majira la tarehe 2 Agosti 2015.

Labda mtu angelisema kuwa huko Tarime ni mbali sana na kilipo kitovu cha miji mikubwa ya nchi na hivyo CCM inaweza kujifaragu ipendavyo kufanya madudu yake, lakini taarifa kutoka kwa aliyekuwa wakala wa mgombea Andrew Uswege Kimbombo huko Kiwalani Minazi Mirefu jijini Dar es Salaam zinasema kulikuwa na vioja vingi sana katika mchakato huo wa uchaguzi. Kadi feki zilikuwa zikigawiwa kama njugu. Zaidi ya hayo anasema amejionea wapiga kura ambao ni watoto wadogo tu lakini kadi walizonazo ni kati ya mwaka 1999 au 2000 wakati ukiwaangalia ndiyo kwanza hawana umri wa miaka 18. Huo ni ubabaishaji na wizi wa hali ya juu unaofanywa na makada wa CCM ndani ya chama chao.

Ubabe pia ulitawala katika siku za awali za upigaji kampeni. Baadhi ya viongozi walidiriki hata kuwapiga viongozi wenzao. Ni hapo majuzi tu ambapo aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania, Job Ndugai, ambaye pia ni mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Kongwa alimshambulia kwa magongo mgombea mwenzake, Dk. Joseph Chilongani, katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni na wana-CCM wenzao. Huo ni ubabe na kuishiwa na sera. Matukio hayo yanatuonesha wazi kuwa viongozi wa CCM hawana uvumilivu wa kisiasa ndani ya chama chao wenyewe.

Uchakachuaji pia ulifanyika katika jimbo la Mahonda kwa upande wa Zanzibar ambapo juzi uchaguzi huo ulighairishwa kutokana na sintofahamu na mizengwe iliyojitokeza katika upigaji wa kura. katika jimbo hilo ambalo miongoni mwa wagombea wake ni makamu wa Pili wa raisi wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, limekumbwa na mizengwe, hali ambayo ililazimisha kurudiwa kwa uchaguzi huo baada ya kukamatwa masanduku ya kura ambayo yanasadikiwa yalishapigwa kura kabla ya upigaji kura rasmi kuanza. Hali hiyo ilizusha taharuki na vurugu kubwa huku baadhi ya wapiga kura hao wakitaka masanduku hayo yafunguliwe na kuchomwa moto makaratasi yote na uchaguzi huo uanze tena upya hali ambayo imelazimisha uchaguzi huo kuakhirishwa na kuanza tena upya jana.

Ni wazi sasa CCM wamemeshindwa kusimamia maadili ya wanachama wake, jee watawezaje kusimamia uadilifu katika serikali na nchi?Ni khatari iliyoje kuwakabidhi mamlaka viongozi wa namna hii amabo kwao wao ubabe, rushwa na wizi ni jambo la kawaida. Imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa chama cha mapinduzi kuipa kisogo misingi ya kidemkrasia jambo ambalo limepelekea wananchi wengi kukihama chama hicho na kuingia vyama vyengine. Wamezoea vya kunyonga, vya kuchinja hawaviwezi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s