Maalim Seif: Ushindi wangu hautachezewa

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad jana alichukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wa Zanzibar kwa mara ya tano huku akisema ushindi wake hautachezewa na mtu.

Katibu Mkuu wa CUF ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar,  Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha fomu za kuwania nafasi ya urais wa kisiwa hicho kupitia chama hicho baada ya kukabidhiwa na Katibu wa chama hicho wa Wilaya ya Magharibi,  Saleh Muhammed Saleh.  Kulia ni  Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Duni Haji

Katibu Mkuu wa CUF ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha fomu za kuwania nafasi ya urais wa kisiwa hicho kupitia chama hicho baada ya kukabidhiwa na Katibu wa chama hicho wa Wilaya ya Magharibi, Saleh Muhammed Saleh. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Duni Haji

Mara ya kwanza Maalim Seif aliwania urais wa Zanzibar mwaka 1995 na amekuwa akifanya hivyo katika chaguzi zilizofuatia na sasa anawania tena kuingia Ikulu Oktoba.

Baada ya kuchukua fomu katika ofisi za chama hicho zilizopo Bububu jana, Maalim Seif alisema ataheshimu matokeo ya urais endapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisema matarajio yake makubwa katika uchaguzi ujao ni kwamba utafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

Alisema ni matumaini yake kwamba mara hii ataongoza na kuibuka kuwa rais endapo uchaguzi utakuwa huru na haki.

“Kama wananchi wa Zanzibar watanipigia kura kwa wingi nawahakikishia hakuna mtu yeyote atakayechezea ushindi wangu,” alisema Maalim Seif.

Akizungumzia afya yake kuelekea Uchaguzi Mkuu, Maalim Seif alisema anagombea nafasi hiyo akiwa mzima wa afya na hana shaka, hivyo wananchi waondoe hofu katika hilo.

“Nachukua fomu ya urais na matarajio yangu makubwa ni kushinda katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika katika mazingira ya amani,” alisema.

Kuhusu masuala ya uchumi, alisema atahakikisha ajira zaidi kwa vijana zinaimarishwa na kuongeza maeneo huru ya uchumi.

“Hivyo ndivyo vipaumbele vyangu nikichaguliwa na wananchi wa Zanzibar kuwa Rais katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema.

Hafla ya Maalim Seif kuchukua fomu ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo mawaziri katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutoka CUF. Maalim Seif aliwataka wanachama wengine kujitokeza kugombea nafasi hiyo kwa kuwa ni haki yao kikatiba.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s