Musimuwachie Maalim Seif pekee urais – CUF

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimewataka wanachama wake wenye sifa za kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar wajitokeze kuchukua fomu kugombea nafasi hiyo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango, Omar Ali Shehe, akitangaza majina ya wagombea kwenye ofisi za CUF, Vuga, Zanzibar siku ya Ijumaa tarehe 8 Mei 2015.

Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango, Omar Ali Shehe, akitangaza majina ya wagombea kwenye ofisi za CUF, Vuga, Zanzibar siku ya Ijumaa tarehe 8 Mei 2015.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe, amewaambia waandishi wa habari jana kwamba, wanachama wanatakiwa wasimuachie Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad, kuchukua fomu ya urais peke yake.

“Tunawataka wanachama wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea urais, wasimuachie Maalim Seif peke yake ili kuondoa manung’uniko kuwa ndiye anayefaa katika chama.

“Kazi ya kuchukua fomu hizi inaanza kesho (leo) kwa muda wa wiki moja na kumalizika Mei 31, mwaka huu, siku hiyo ndiyo mwisho wa urejeshaji wa fomu hizo zitakazouzwa kwa Sh 500,000 na zitatolewa kwa makatibu wa wilaya,” alisema Shehe.

Alisema pamoja na mambo mengine, chama hicho kimekubaliana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa mgombea urais upande wa Zanzibar atakayesimama atatoka CUF.

Alisema katika Jimbo la Kikwajuni, kwa nafasi ya ubunge watasimamisha mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alisema baada ya kukamilika uchukuaji na urejeshaji, majina ya wagombea yatapelekwa Kamati Tendaji Taifa ili kupigiwa kura ya maoni. Baada ya hapo, yatapelekwa Baraza Kuu kwa ajili ya ukaguzi na kutoa uamuzi kama mgombea anafaa au la.

“Hata kama atajitokeza mtu mmoja tu kuchukua fomu ya urais, lazima apitie hatua za mkutano wa Kamati Tendaji kama taratibu zetu zinavyoonyesha.

CHANZO: MTANZANIA

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s