Kura za maoni CUF kuanza rasmi Mei 16

cuf.jpg

TAARIFA KWA WANACHAMA WOTE WA CUF

Kura za maoni za udiwani na ubunge zinaanza rasmi Jumamosi tarehe 16 Mei 2015 na zitafanyika kwa kanda na ratiba yake itatolewa kwa awamu kulingana na zoezi la uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura. Kama itabidi kuahirisha uchaguzi wa kura za maoni katika majimbo ambayo yatakuwa yametangaziwa tarehe na ikawa inagongana na zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu, basi tutawaomba radhi wanachama wa majimbo husika mtuvumilie.

Kwa upande wa Tanzania Bara, kura za maoni zitapigwa siku ya Jumamosi tarehe 16 Mei 2015 kwa ngazi ya udiwani kwenye wilaya ya Temeke na zitaendelea tena Jumapili tarehe 17 Mei 2015 kwa wilaya za Ilala na Kinondoni.

Jumatano, tarehe 20 Mei 2015, ni uchaguzi wa kura za moni za ubunge kwa wilaya zote tatu za Dar es Salaam – yaani  Temeke, Ilala na Kinondoni.

Chaguzi zote zitasimamiwa na Kamati Tendaji Taifa.

Kata au Jimbo ambalo halina mgombea au mgombea wake wa jukwaa ni mmoja, halitakuwa na kura za maoni hata kama kuna wagombea wa viti maalum zaidi ya mmoja, isipokuwa kamati ya Uchaguzi/Utendaji ya Kata au Wilaya itaweka sifa kwa mujibu wa vigezo vilivyoandaliwa na Kamati Tendaji Taifa na kushushwa ngazi za chini kwa utekelezaji.

Ahsanteni kwa ushirikiano wenu

HAKI SAWA KWA WOTE

Abdulrahman Lugone
Afisa Uchaguzi – CUF Taifa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s