Shahada mara nne, ya tano lazima CUF iongoze dola

Kutokana na umri wangu nilionao, nimewahi kuona mara mbili mgombea mmoja wa urais katika nchi fulani akigombea mara nne mfulululizo na akashinda kwenye mara ya tano kuiongoza nchi yake aipendayo. Moja ni Senegal na nyengine ni Nigeria. Kuna kila dalili kuwa sasa nitashuhudia mara ya tatu ndani ya Zanzibar yangu mwenyewe.

Kijana anayeiunga mkono CUF.

Kijana anayeiunga mkono CUF.

Nitafafanua tu historia ya Abdoulaye Wade aliyekuja kuwa rais wa Senegal kupitia chama chake cha Senegal Democratic Party (SDP) kuanzia tarehe 1 Aprili 2000 hadi 2 Aprili 2012. Kabla ya kuwa rais, Wade alikuwa amegombea kiti cha urais kwa mihula minne kama ilivyo kwa Maalim Seif Sharif Hamad wa Chama cha Wananchi (CUF) visiwani Zanzibar.

Kama ilivyokuwa kwa Zanzibar, katika kila muhula wa uchaguzi nchini Senegal yale yale ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na CUF ndio yale yale ambayo Wade na SDP waliyokuwa wakiyalalamikia. Miongoni mwa hayo ni kunyimwa haki wapiga kura wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wake na Tume ya Uchaguzi ya Senegal, kutumiwa vibaya vyombo vya dola dhidi ya wafuasi wa Wade hadi kufikia vyombo vya dola kuwaua wafuasi hao.

Chama kilichokuwa madarakani nchini Senegal ambacho ndicho kilichopigania uhuru wa nchi hiyo, Socialist Party of Senegal, kama kilivyo Chama cha Mapinduzi (CCM), kilijiona ndicho chenye haki pekee ya kukamata hatamu za uongozi. Lakini Wade na  SDP hawakuvunjika moyo na badala yake walizidi kushajihishana kwa njia mbalimbali kila wakiangushwa kwenye uchaguzi mmoja, hadi kufikia kuingia katika muhula wa tano mwaka 2000. Kama kwenye chaguzi nyengine, tayari mwaka huo dalili zote za ushindi zilionyesha wazi kwamba hakukuwa na sababu ya Wade kutokuwa mshindi katika uchaguzi wa mwezi Machi na kweli alishinda kwa 58.49% dhidi ya Rais Abdou Diouf wa chama tawala cha SPS.

Basi kwa dalili hizo hizo za CUF, ndizo hizo hizo zilizofanya kuwa ukomo wa ugombea urais ukiwa kama mpinzani uwe shahada mara nne kwa Senegal na kumfanya Wade na chama chake cha SDP kuingia madarakani na kuingoza Senegal. Maalim Seif amegombania uchaguzi kwa mihula minne kupitia CUF na chama hiki na wafuasi wake wamefanyiwa waliyofanyiwa ya unyama na ushetani, lakini bado chama kinakwenda mbele kwa kasi na hadi kuwa chama tishio zaidi siku hadi siku. Kila uchaguzi mmoja upitapo na CUF kubwagwa kwenye wizi wa kura, chama hiki huimarika zaidi. Kinazidi kuwa kivutio kwa wananchi Wazanzibari walio na uchungu na mapenzi ya nchi yao, kwani ni CUF ndiyo iliyobeba matumaini ya haki sawa kwa wote.

Kila Kona ya Zanzibar kwa sasa kuna wafuasi wa CUF lukuki, ambao ni wapigakura hata katika yale maeneo ambayo miaka ya nyuma hakukuwa na watu wanaokiunga mkono chama hiki. Kitu hiki kimewafanya watawala kupata homa ya mara kwa mara isiyo na ponyo.

Ndugu Mzanzibari, kwa kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na ukaipigia kura CUF mwezi Oktoba 2015 na ukasimama imara kuilinda kura yako, ndipo utakapoiangusha chini ile kauli ya “hatutoi” inayotolewa leo. Ukifanya hivyo, utaitoa nchi kwenye madhila yaliyokithiri, na ndipo utaibakisha Zanzibar katika mikono salama kwa ajili ya urithi wa kizazi chako.

Makala ya Ali Mohammed Ali

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s