“Madhara ya mafuriko yanaweza kuepukwa”

Hali iliyojitokeza tokea juzi na kuwaacha wananchi wengi katika maafa makubwa, inaonesha ni jinsi gani baadhi ya taasisi za Serikali zilivyokosa uwezo kiutekelezaji na kukosa kujiweka tayari kila wakati katika kukabiliana na hali za dharura zinazojitokeza na kupunguza madhara yake kwa wananchi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mitaa ya Zanzibar ikiwa imefurika maji na uchafu baada ya mvua kali ya siku mbili.

Mitaa ya Zanzibar ikiwa imefurika maji na uchafu baada ya mvua kali ya siku mbili.

Chama Cha Wananchi (CUF) kinaungana na Wazanzibari wote katika kuwapa pole wananchi wote waliokumbwa na maafa, ikiwemo waliopoteza maisha, waliokosa makaazi na walioharibikiwa na nyumba zao na mali zao, kufuatia mvua kubwa iliyofikia milimita 172 kwa muda wa masaa matatu, zilizonyesha katika visiwa vya Zanzibar kwa takriban siku tatu.

Chama cha Wananchi (CUF) kinawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira wanafamilia za wananchi wawili, Tabiru Othman Khamis (28) na Hamad Juma Suleiman (26) waliopoteza maisha baada ya kutumbwikia katika bwawa la maji lililopo eneo la Mwanakwerekwe, na kwamba Chama Cha Wananchi (CUF) kipo pamoja na wana familia hao na wananchi wote katika kipindi hichi kigumu cha msiba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu hao mahali pepa peponi. Amin.

Aidha, Chama cha Wananchi kinawapongeza wananchi wote katika mitaa mbali mbali waliojitokeza kuwasaidia wananchi wenzao waliokumbwa na maafa hayo kwa kuwahifadhi katika nyumba zao, kusaidia harakati za kuondoa maji katika makaazi mara baada ya kujitokeza hali hiyo.

Vile vile Chama cha Wananchi (CUF) kinatoa wito kwa Mamlaka zinazohusika na Maafa, ikiwemo Idara ya Maafa Zanzibar iwe na utaratibu mzuri unaoeleweka katika kutekeza mipango na mikakati mbali mbali iliyokwisha fikiwa katika kumaliza tatizo la miaka mingi la mafuriko ya maji ya mvua katika Mji wa Zanzibar.

Hali iliyojitokeza tokea juzi na kuwaacha wananchi wengi katika maafa makubwa, inaonesha ni jinsi gani baadhi ya taasisi za Serikali zilivyokosa uwezo kiutekelezaji na kukosa kujiweka tayari kila wakati katika kukabiliana na hali za dharura zinazojitokeza na kupunguza madhara yake kwa wananchi.

Chama cha Wananchi (CUF) kinaaamini iwapo kutakuwa na umakini mkubwa na kutekelezwa kwa vitendo mipango na mikakati ya kitaalamu iliyokwisha andaliwa tena kwa gharama kubwa, baadhi ya athari za maafa zinaweza kuepukwa.

Chama cha CUF kinajua kuwa kazi kubwa na nzuri ya kuanisha maeneo yanayokumbwa na maafa ya mafuriko ya maji kila mara katika Mji wa Zanzibar ilifanyika tokea mwaka 2007. Lakini ikiwa ni takriban miaka minane sasa, hadi sasa mafanikio ya utekelezaji wa mpango huo yamekuwa finyu kabisa na watu wanaendelea kupoteza maisha na mali nyingi pamoja kupata athari kubwa kila msimu wa mvua kubwa unapowadia.

Kwa hivyo, Chama Cha Wananchi (CUF) kinaendelea kuzizindua Mamlaka zinazohusika, zikiwemo Idara ya Maafa na Baraza la Manispaa Zanzibar kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Mpango wa kudhibiti Maji ya Mvua katika maeneo mbali mbali ya Mji wa Zanzibar kwa azma ya kuwaepushia madhila makubwa Wananchi.

Chama cha Wananchi (CUF) kinaamini maisha ya watu yana thamani kubwa kuliko kitu chengine chochote kile, hivyo ni wajibu wa Mamlaka zilizopewa majukumu ya kusimamia maisha hayo kutekeleza ipasavyo wajibu huo na wananchi wa Zanzibar waendelee kuwa katika hali ya amani, utulivu na usalama wa maisha na mali zao.

Imesainiwa na:
SALIM BIMANI
MKURUGENZI WA H/U/M/UMMA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s