Maalim Seif athibitisha kugombea urais

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amethibitisha nia yake ya kugombea tena nafasi ya Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.

Mwenyekiti wa Zoni ya Mjini na Maalim Seif.

Mwenyekiti wa Zoni ya Mjini na Maalim Seif.

Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na kamati maalum ya (CUF) Zoni ya Mjini iliyokwenda kumdhamini kugombea nafasi hiyo huko nyumbani kwake Mbweni, Maalim Seif amesema anatarajia kugombea tena nafasi hiyo ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwatumikia wananchi.

Kamati hiyo ya CUF Zoni ya Mjini imemdhamini Maalim Seif kwa fedha taslim shilingi milioni mbili na laki tano, ili iweze kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar wakati utakapofika.

Maalim Seif ameishukuru kamati hiyo kwa uamuzi wa busara waliochukua, hali inayoonyesha kuwa wananchi wa Zanzibar wanaendelea kuwa na imani naye kutokana na mwelekeo wake wa kutaka kuleta mabadiliko ya kweli kwa Zanzibar.

Amesema iwapo wananchi watakipa ridhaa Chama hicho kuongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, kitatandika misingi imara ya utawala bora, uchumi na kuendeleza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Ameyataja mambo mengine ya msingi kuwa ni pamoja na kurejesha heshima ya Zanzibar katika jamii ya Kimataifa, kuimarisha huduma za kijamii ziliwemo afya na elimu, pamoja kuandaa mazingira ya kuongeza ajira kwa vijana.

Amesema tofauti na chaguzi zilizopita, Chama hicho kimejiandaa vizuri kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, na kuwaomba wananchi waendelee kukiunga mkono ili kiweze kupata ushindi mkubwa na kuweza kuongoza serikali.

Mapema akisoma risala ya kamati maalum ya (CUF) zoni ya mjini, mjumbe wa kamati hiyo Bw. Salim Abdallah Salim amesema wameamua kumdhamini Maalim Seif kutokana na utendaji wake ndani ya chama hicho pamoja na matumaini aliyonayo kwa Wanzibari.

Aidha kamati hiyo imetoa tamko rasmi la kumuunga mkono Maalim Seif kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar wakati utakapofika, na kutoa wito kwa vijana kutafuta vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi (ZAN ID) na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, ili waweze kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s