Liwale mkutano waendelea

Picha ya Jumatatu tarehe 4 Mei 2015, mkutano wa hadhara Liwale.

Picha ya Jumatatu tarehe 4 Mei 2015, mkutano wa hadhara Liwale.

Kikiwa kwenye ziara yake ya kuwatayarisha wananchi kwa ajili ya uandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapiga kura katika mikoa ya kusini ya Tanzania Bara, jana Chama cha Wananchi (CUF) kilipaswa kuchukuwa maamuzi magumu ya kukaidi amri ya polisi wa eneo hilo kukitaka kisitishe kufanya mkutano wake wa hadhara leo Jumatatu ya tarehe 4 Mei 2015 katika eneo la Liwale kwa madai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) nacho kilikuwa kinafanya mkutano kwenye eneo hilo hilo.

Mapema Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya, alilionya jeshi la polisi dhidi ya kuingilia haki za kisiasa cha chama chake kukusanyika kwa kuibeba CCM ambayo inaonekana kulemewa vikali kwenye mikoa yote ya kusini, na ambako sasa CUF inaimarisha ngome yake. Kambaya alisema kwamba CUF haioni sababu ya kuahirisha mkutano huo na kuufanya siku ya pili yake ili kuipisha CCM kwa siku ya Jumatatu, akisema kwamba chama chake kingelifanya mkutano kama ulivyopangwa.

Hadi tunachapisha taarifa hii mtandaoni, CUF ilikuwa inaendelea na mkutano wake huo, huku Kambaya akitoa wito kwamba CUF inasimamia kile inachoamini kuwa ni sheria.

This slideshow requires JavaScript.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s