Moyo: Nitaendelea kutetea Zanzibar huru

Aliyekuwa muasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Hassan Nassor Moyo (pichani) , aliyevuliwa uanachama na chama hicho, amesema ataendelea na msimao wake wa kuitetea Zanzibar yenye mamlaka kamili bila ya kuwa na chama chochote cha siasa. Akizungumza na NIPASHE, Moyo alisema lengo lake la kutetea mfumo wa serikali tatu halitarudi nyuma kwani ana imani kuwa chama kimemfukuza, lakini wananchi bado wanamkubali.

Mzee Hassan Nassor Moyo

Mzee Hassan Nassor Moyo

 Alisema kwa sasa hana haja ya kuwa na chama chochote cha siasa, lakini ataitumia nafasi yake ya kuhakikisha Zanzibar inakuwa na mamlaka kamili.
“Kutokana na umri wangu sasa sitaki kujihusisha na chama chochote cha siasa na hatua ya CCM kunifukuza haijaniathiri hata kidogo,” alisema Moyo.
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa Chama cha Wananchi (CUF), Salum Bimani, alisema kitendo cha CCM kumfukuza muasisi huyo ni kuchanganyikiwa kisiasa.
“Wazee kama wale ambao wanahekima na busara wanahitaji kuenziwa kwani ni wazee wa kitaifa,” alisema Bimani.
Alisema muasisi huyo wao wanamuhitaji kwa busara zake za kuendeleza nchi na sio kichama, hivyo wataendelea kumuunga mkono katika kutetea maslahi ya Zanzibar.
“Muasisi kama Mzee Moyo ni  hazina katika nchi na kutokana na umri wake, sasa hawezi kujihusisha na vyama, ila ana mchango mkubwa katika nchi,” alisema.
 Juzi hii Mzee Moyo alifukuzwa CCM kwa madai ya kwenda kinyume cha maadili ya chama hicho ikiwamo kutetea muundo wa serikali tatu.
 Chama tawala kilisema baada ya kutafakari kwa kina kimebaini kwamba kauli zake na matamshi yake zimekuwa zikipotosha jamii na wanachama wake, hivyo kupoteza sifa za kuwa mwanachama.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s