Maalim Seif ‘abadili taratibu’ kortini Kisutu

Ulinzi uliimarishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu na watu waliofika kusikiliza kesi zao walilazimika kukaguliwa kwa vifaa vya kutambua vitu hatari kutokana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwenda kusikiliza kesi ya wafuasi wa CUF.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (katikati) akiagana kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam alipohudhuria kesi ya Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba ilipokuwa ikiendelea mahakamani hapo jana. Picha na Said Khamis.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (katikati) akiagana kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam alipohudhuria kesi ya Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba ilipokuwa ikiendelea mahakamani hapo jana. Picha na Said Khamis.

Maalim Seif, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alikuwa miongoni mwa watu waliofika katika Mahakama hiyo kusikiliza kesi ya kuandamana bila kibali inayomkabili Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wengine 30 wa chama hicho.

Msafara wa magari manne wa Makamu huyo wa Rais, ulifika mahakamani saa 3.46 asubuhi, akiwa ndani ya gari aina ya Toyota, Land Cruiser.

Katika kesi hiyo, Profesa Lipumba na wafuasi wake 30, wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kufanya mkusanyiko usio halali na kupinga amri halali ya ofisa wa polisi iliyowazuia kuandamana Januari 27, Temeke, Dar es Salaam.

Baada ya kufika Kisutu, Maalim Seif alipanda ghorofa ya kwanza na kusubiri hadi saa 5.02 asubuhi pale maofisa wa Mahakama, Profesa Lipumba na wafuasi wake walipoingia ndani ya Mahakama ya wazi. Baada ya muda mfupi, Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha aliingia mahakamani na kama ilivyo ada, watu wote akiwamo Maalim Seif walisimama kuonyesha utii kabla ya kesi kuanza kusikilizwa.

Kesi yenyewe

Wakili wa Serikali Mkuu, Bernard Kongora aliyeambatana na mawakili wenzake, Tumaini Kweka, Joseph Maugo, Nassoro Katuga na Salum Mohammed alisimama na kufanya uhakiki wa washtakiwa na kisha aliwasomea mashtaka, washtakiwa wawili ambao walijisalimisha jana mahakamani hapo, wakiwa miongoni mwa wafuasi 30 wa CUF walitokomea mwezi uliopita baada ya kuachiwa huru kwa muda kwa lengo la kuunganishwa kesi zao kuwa moja.

Baada ya kuwasomea mashtaka, Shaweji Mohamed (39) na Hemed Joho (46), Kongola aliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na akaomba ipangwe tarehe ya kusomewa maelezo ya awali.

Mawakili wa upande wa Utetezi, Job Krerio, Peter Kibatala, Hashim Mziray na John Mallya waliondoa mapingamizi ambayo awali, waliyawasilisha mahakamani wakidai suala la Profesa Lipumba lilizungumzwa bungeni na kuundiwa kamati, hivyo mahakama hiyo haina uwezo wa kulisikiliza.

Hoja nyingine ni kwamba matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe bungeni kuhusu kesi hiyo yaliathiri msingi wa kesi kwa kuwaonyesha kuwa washtakiwa wana hatia.

Licha ya upande wa utetezi kuondoa mapingamizi hayo, Wakili Kongola alieleza kuwa walikuwa wamejiandaa kuyajibu. Washtakiwa 18 wa kesi hiyo waliojisalimisha awali na wawili wa jana, walipatiwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja akisaini hati ya Sh2 milioni. Kesi imeahirishwa hadi Mei 6 watakaposomewa maelezo ya awali.

Washtakiwa

Mbali na Lipumba wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Shabani Ngurangwa (56), Mohammed Kirungi (40), Juma Mattar (54), Mohamed Mbaruk (31), Kaisi Kaisi (51), Issa Hassani (53), Mohamed Mtutuma (33) Salehe Ally (43), Abdallah Said (45) na Bakari Malija (43).

Shabani Tano au Kasakwa (29), Shabani Polomo (40), Athumani Ngumwai (40), Shaweji Mohamed (39) na Abdul Juma (40), Hassan Saidi (37), Hemed Joho (46), Allan Ally (53), Abdina Abdina (47) na Allawi Msenga (53).

Pia wamo Abdi Hatibu (34), Abdallah Ally (32), Said Mohamed (40), Salimu Mwafisi, Saleh Rashid (29), Rehema Kawambwa (47), Salma Ndewa (42), Athumani Said (39), Dickson Leason (37) na Nurdin Msati (37).

Chanzo: Mwananchi la tarehe 14 Aprili 2015

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s