Maalim Seif: Jeshi la Polisi halitendi haki

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amelitupia lawama Jeshi la Polisi kwa madai ya kwamba halitendi haki kwa vyama vya siasa. Lawama hizo alizitoa juzi wakati akiwahutubia wananchi, baada ya kufungua ofisi mpya ya Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la Dole, Wilaya ya Magharibi, Unguja.
Wafuasi wa CUF kwenye mkutano.

Wafuasi wa CUF kwenye mkutano.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alisema mwanzoni baada ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Jeshi  la Polisi lilikuwa likifanya kazi zake bila ya upendeleo, lakini kwa sasa limetekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema anasikitishwa kuona Jeshi la Polisi limeingia katika siasa kwa kuviwekea vikwazo vyama vya siasa kutofanya mikutano na kuzuia watu kutoka wilaya moja kwenda nyingine kuhudhuria mikutano ya vyama hivyo.
Alisema Jeshi la Polisi halipaswi kuwazuia kufanya mikutano ya hadhara kwani ni haki yao kikatiba na kisheria kwa mujibu wa sheria namba tano ya vyama vya siasa nchini ambayo inasema vyama vina haki ya kufanya mikutano pahali popote.
“Tunaliambia Jeshi la Polisi lisiturejeshe tulipotoka, kwani kuna watu hawataki maridhiano katika nchi yetu hii na polisi mmekuwa mkiwafuata watu hao wasiotaka maridhiano,” alisema.
Alisema CUF kitaendelea kufanya mikutano yake ya kuwahamasisha wananchi mpaka mamlaka kamili ya Zanzibar  yatakapopatikana na hilo haliwezi kuzuilika.
Alisema Zanzibar haina utawala bora, lakini Oktoba mwaka huu utawala bora utapatikana na kwamba CUF itaongoza dola chini ya mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Akizungumzia kuhusu viongozi wanaowataka katika chama hicho, alisema hawataki kuona viongozi mizigo ambao wanajinufaisha wao binafsi badala ya chama na wananchi.
Aliwataka wananchi hao anapotokea mtu katika chama hicho anataka uongozi wampime uwezo wake kama anafaa kukitumikia chama na wananchi na sio kujinufaisha yeye binafsi.
“Wapo baadhi ya viongozi wamehama hata katika majimbo yao na wanajinufaisha wenyewe badala ya kukinufaisha chama na wananchi, viongozi hawa hatuwataki katika uchaguzi mkuu,” alisema Maalim Seif.
CHANZO: NIPASHE
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s