CUF hairudi nyuma

CUF inatoa wito kwa Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wake kwa misingi ya haki, sheria na uadilifu; na kuepuka kutumiwa kisiasa na kuwacha ukereketwa, huku likielewa kwamba kwa mujibu wa Sheria No.5 ya Mwaka 1992 ya Vyama vya Siasa, halina mamlaka yoyote ya kuzuia Mkutano Halali wa Chama cha Siasa Kilichosajiliwa.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Mhe. Nassor Mazrui.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Mhe. Nassor Mazrui.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waheshimiwa Wakurugenzi, Viongozi, Watendaji wa Chama, Wahariri, Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbali mbali, Ndugu Wananchi, Mabibi na Mabwana……Assalaamu Alaykum!

Waheshimiwa!

Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezu Mungu kwa kutujaalia tukakutana wakati huu na katika kikao hiki muhimu.

Waheshimiwa! Hizi ni zama ambazo Nchi yetu ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, inahitaji mafanikio na maendeleo ya kweli katika ngazi zote, kupitia misingi muhimu ya demokrasia na utawala bora, chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo sasa imeanza kuangaza matumaini mema ya ukombozi thabiti wa Wazanzibari wote.

Waheshimiwa! Katika kuendeleza na kufanikisha azma hiyo ni lazima yawepo mashirikiano ya wananchi wote bila kutanguliza utashi binafsi, pamoja na kuzingatia siasa za kistaarabu, demokrasia, utawala bora na umoja wa kitaifa, na pia kuweka mbele maslahi ya Nchi yetu.

Waheshimiwa! Sote ni mashahidi wa namna umma wa Wazanzibari ulivyokwisha kujiunga na wimbi kubwa, zito, la kihistoria la kisiasa katika safari ndefu sasa ya kupigania na kurejesha mamlaka kamili ya Zanzibar, ambapo tunasema hilo halizuiliki, kwani si rahisi kuushinda wakati.

Waheshimiwa! Hiyo ni safari na hayo ni mapambano ambayo kama ilivyo kawaida hayakosi wasaliti, ingawa pia hatimaye hakuna mapambano ya dhati yasiyokuwa na mafanikio; nataka nikuhakikishieni kwamba na sisi hatutarudi nyuma.

Historia inathibitisha kuwepo wasaliti wa Zanzibar na Wasaliti wa Mamlaka kamili ya Zanzibar, na pia wasaliti wa maendeleo na matumaini ya watu wa visiwa hivi vya Unguja na Pemba; tena usaliti huo ulikuwepo zamani na awamu zilizotangulia, na sasa dhahiri unajionyesha kupitia hata baadhi ya watendaji wa ngazi za juu za Serikali, ambao kimsingi wamedhihirisha kutokuitakia mema Nchi hii na watu wake; tunasema hao ni vibaraka na huko ni kushindwa kwa kiasi kikubwa.

Waheshimiwa! Usaliti na azma mbaya ni mambo yasiyoweza kujificha, ni mithili ya moto ulianzia kufuka moshi na hatimaye ukawaka na kuleta madhara kwa wahusika wenyewe na kisha kwa umma ambao katu sasa umeshaamua kuachana na kila asiyeitakia mema Zanzibar.

Historia inaashiria hivyo Waheshimiwa, tangu pale kabla na baada ya Mapinduzi ya Tarehe 12 Januari 1964; kupitia Awamu zote za Uongozi; Awamu ya Pili ya Mzee wetu Aboud Jumbe; mpaka kufikia katika Awamu ya Sita ya Uongozi chini ya Raisi Mstaafu Mheshimiwa Dr. Amani Abeid Karume, ambapo Umma wa Wazanzibari uliamua kwa Sauti kubwa kuyachagua Maridhiano ya Kisiasa na hatimaye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Yote hayo Waheshimiwa ni ishara kwamba Wazanzibari walikwishachoshwa na usaliti wa maendeleo na usaliti wa mamlaka kamili; na hivyo basi pia wameelekeza kwa ujasiri kabisa matumaini yao ya maendeleo ya kweli na utaifa wao katika misingi ya umoja wa kitaifa, na asilan hawaonyeshi dalili za kurudi nyuma, na wala hawatakubali kudanganywa tena.

Mnaelewa waheshimiwa Chama cha Wananchi, CUF, kilikotokea, na kinakoenda; namna kilivvyohimili mawimbi mazito ya hila, hujuma, idhilali, vitisho na kila aina ya mateso na udhalilishaji, ambayo matunda yake ya subira na uvumilivu na ya kujivunia yanaonekana sasa ambapo umma umeamua kuwekeza matumaini yao ya dhati kabisa kwa Chama hiki kisichoyumba na kilichothibiti katika kuwajali na kuwatetea wananchi wote kwa hali na mali bila ubaguzi huku kikitanguliza maslahi ya Nchi.

Waheshimiwa! Moja ya matunda ya uvumilivu na hikma za Viongozi wa Chama cha Wananchi, CUF, chini ya Majemedari Maalim Seif Sharif Hamad, Profesa Ibrahim Lipumba na wengine wote ni kuiona Zanzibar ikibaki salama, licha ya fitna na misukosuko, iliyogharimu hata maisha ya watu wasiokuwa na hatia; na Inshaallah itaendelea kubaki salama, hata mbele ya maadui wasioitakia mema Nchi hii.

Mnakumbuka vyema Waheshimiwa namna Wananchi walivyouwawa kikatili na Jeshi la Polisi katika Mauaji ya Tarehe 26 na 27 Januari 2001, Unguja na Pemba; namna Viongozi na Wananchi walivyosulubiwa kila mara kwa vipigo na namna walivyoweza kubambikiziwa kesi na kila aina ya hujuma; namna Nchi hii ilivyotikisika na hatimaye ikazalisha wakimbizi katika Kambi za Shimoni na Dadaab, Nchini Kenya.

Waheshimiwa! Lazima muelewe kwamba si rahisi kuirejesha historia na mambo yaliyokwishapita; lakini pia ni lazima kujifunza kutokana nayo, hivyo mwanadamu si vyema kufumbia macho dhulma iliyokwishatendeka kwa kisingizio tu kwamba watu wamejaribu kusahau; Na huo ndio pia wito wetu kama wasemavyo wahenga, “mwenye kovu usidhanie kapoa”.

Waheshimiwa! Zama za ubabaishaji, ubadhirifu, ufisadi wa kupindukia, ubaguzi, vitisho na kila aina ya hujuma dhidi ya wananchi, Viongozi wapenzi wa wananchi, watendaji waaminifu na waadilifu, na watetezi wote wa umma na watetezi wa Zanzibar, zimepitwa na wakati, siyo hapa tu bali duniani kote; huu ni wakati wa kuishi kwa kuchunga haki, demokrasia, utawala bora, sheria, umakini, na uwazi usioleta shaka.

Mmeshuhudia Waheshimiwa katika mfululizo wa matukio ya hivi karibuni, na zaidi dhidi ya Chama cha CUF, Viongozi wa CUF, Wapenzi na Wafuasi pamoja na Wananchi wasiokuwa na hatia, na pia dhidi ya Ofisi za CUF; na ndiyo maana tukaamua kuyakumbusha hayo.

Chama cha Wananchi, CUF, umma wote, na kila waungwana, hawakupendezewa hata kidogo na kitendo cha hivi karibuni cha kuteketezwa vibaya na moto, Ofisi ya Jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi Unguja, Usiku wa kuamkia tarehe 24 Machi, 2015 majira ya saa 8.30, iliyogharimu zaidi ya Shilingi 150 Milioni.

Umma wote umestushwa na kulaani kwa nguvu zote kitendo cha kupigwa na kuhujumiwa wananchi waliokuwa wakirejea katika Mkutano wa Hadhara, uliofanyika Jumapili Tarehe 29 Machi, 2015, Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja, ambapo zaidi ya watu 30 walijeruhiwa vibaya.

Pamoja na yote, ya kushangaza, ya kuudhi na ya kusikitisha sana ni matokeo ya Jana Jumapili, Tarehe 12 April, 2015 katika Jimbo la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja; katika hali isiyotarajiwa kabisa, wakati huu tunaohitaji siasa za kistaarabu kwa maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari wote, kuona vurugu zilizoandaliwa kwa makusudi ili kuparaganya na kutiribua hali ya utengamano wa kisiasa Nchini.

Waheshimiwa! Kilichotokea hiyo jana ni hali iliyoandaliwa kwa makusudi kwani dalili ziliashiria tangu mapema za kushawishi na kulazimisha au pia kuuhujumu Mkutano Halali kabisa wa Chama chetu uliopangwa kufanyika katika Jimbo hilo, katika Shehia ya Kipandoni, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CUF, ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Maalim Seif Sharif Hamad.

Waheshimiwa! Waandaaji, wahamasishaji, wafadhili na watekelezaji wa hujuma zote hizo, wakitumia mamlaka waliyonayo serikalini, na pia kwa kushirikiana na vyombo vya dola, wanajulikana na umma umeshathibitisha kupitia mfululizo wa matukio hayo azma mbaya waliyonayo katika kukihujumu Chama cha CUF, kuwahujumu wananchi wasiokuwa na hatia, kuihujumu Zanzibar, na kuirejesha tena Nchi hii katika zama za siasa chafu za chuki, ubaguzi, mizozo na migogoro.

Chama cha Wananchi, CUF, kinalaani kwa nguvu zote mwenendo huo na kinaitaka Serikali kuwa makini hasa wakati huu ambao wananchi wanashuhudia mwelekeo mwema wa kisiasa na matumaini ya maendeleo chini ya maridhiano na hali ya umoja wa kitaifa.

Aidha, Chama cha Wananchi, CUF, kinatoa wito kwa Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wake kwa misingi ya haki, sheria na uadilifu; na kuepuka kutumiwa kisiasa na kuwacha ukereketwa, huku likielewa kwamba kwa mujibu wa Sheria No.5 ya Mwaka 1992 ya Vyama vya Siasa, halina mamlaka yoyote ya kuzuia Mkutano Halali wa Chama cha Siasa Kilichosajiliwa.

Pongezi za dhati kwa wanachama, wapenzi na wananchi, pamoja na wakaazi wa Kitope, kwa uungwana, hikma na ustahamilivu wao, waliouonyesha ambao uliodhihirisha ukomavu wa hali ya juu kisiasa wa Wana-CUF, licha ya hujuma, uchokozi na usumbufu wa makusudi uliofanywa na Jeshi la Polisi. Jeshi la Pilisi linaonekana wazi kwamba limebeba mbeleko Chama cha CCM kutoka katika kina kirefu cha Maji.

Jeshi la Polisi linatoa vibali na kuvifuta hii inadhihirisha wazi kwamba Jeshi hilo halina uhuru wa kufanya kazi zake bila kuingiliwa na viongozi wa Chama cha CCM.

Wameshindwa kufanya kazi yao ya Ulinzi wa Raia sasa wananyima haki na uhuru wa watu ambao kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar wanaouhuru wa kutembea Zanzibar bila ya vizuizi vyovyote.

Mpango wa Jeshi la Polisi kuzuia Wazanzibari kutembea wanapotaka na siku wanayoitaka ni kukiuka Katiba Halali ya Zanzibar.

Chama cha Wananchi, CUF, kinatoa pole kwa waandishi wa habari, kutokana na usumbufu na udhalilishaji wa Jeshi la Polisi uliolenga kuzuia utekelezaji wa majukumu yao ya kazi hasa pale walipotaka kushiriki ziara ya ndani ya Mhe shimiwa Katibu Mkuu katika Uzinduzi wa Matawi Mapya na Uwekaji wa Mawe ya Msingi wa Matawi na Baraza za CUF katika Jimbo hilo.

Na mwisho kabisa, Chama cha Wananchi, CUF, kinatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu, wasikivu, na wastahamilivu wakizingatia umuhimu wa amani, utulivu na mshikamano, mambo ambayo hayapatikani pasi na kutenda haki, huku wakielewa kwamba mwisho wa fitna zote ni fedheha.

HAKI SAWA KWA WOTE

Nassor Ahmed Mazrui

Naibu Mkuu wa CUF, Zanzibar

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s