Tumekwenda Kitope na Kitope imekuja kwetu

Leo Jumapili ya tarehe 12 Aprili 2015, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ameongoza ujumbe mzito wa viongozi, wanachama na wafuasi wa CUF kwenda kwenye jimbo la Kitope, ambako pamoja na mengine amefunguwa matawi mapya manne na baraza mbili za vijana. Kubwa kuliko yote ni kuwa wanachama wapya 400 wamejiunga na chama chetu hivi leo katika eneo hili ambalo lilikuwa likifahamika kuwa ni ngome ya CCM.

Ni kweli kwamba mkutano mkubwa wa hadhara ambao tulikuwa tumeupanga kuufanya huko ulizuiwa na jeshi la polisi ambalo awali lilidai kwamba mtu aliyekuwa amekubali kutupa kiwanja, alighairi baadaye.Lakini wakati jeshi hilo likidai hivyo, mmoja wa wanachama wapya aliamua hapo hapo kutoa kiwanja chake kilichoko Kilombero huko huko Kitope.

Kwa hivyo, kizuizi hasa hakikuwa ukosefu wa eneo la kufanyia mkutano, bali jeshi la polisi kutumikia amri ya mmoja wa kiongozi mkubwa wa seriikali ambaye alidhani kwamba angeliweza kuisukuma CUF kwenye mtego wake wa kuangukia kwenye vurugu.

Sisi tunathamini sana maisha na usalama wa watu wetu na wa wananchi wote wa Zanzibar. Ndio maana tuliwashawishi maelfu ya watu ambao tayari walishafika kwenye viwanja vya mkutano kurejea nyumbani kwa usalama bila kuchukuwa hatua yoyote kuitumia haki yao ya kikatiba ya kukusanyika. Na kwa kuwa tuna uongozi kwa maana halisi ya uongozi, watu wetu walitusikiliza.

Ujumbe mkubwa na wa pekee leo kwa viongozi wa SMZ ambao wanalazimisha kuiingiza nchi kwenye machafuko ni kwamba sisi CUF tumefika Kitope na Kitope imefika kwetu. Mageuzi hayazuiliki tena.

Maalim Seif Sharif Hamad akifungua barza mpya ya CUF kijijni Upenja ambayo imepewa nina la HATUDANGANYIKI.

Mwanachama mpya wa CUF ametoa nyumba yake hii itumike kama tawi la chama baada ya hamashauri ya wilaya kukataa kutoa kibali cha kujengea tawi hilo kijijini Upenja.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wananchi kwenye tawi jipya la CUF Upenja, ambapo aliwanasihi kuendelea kuwa na subira na kujizuwia kuchokozeka licha ya viongozi wa CCM kupania kuwaondoa kwenye mstari.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wananchi kwenye tawi jipya la CUF Upenja, ambapo aliwanasihi kuendelea kuwa na subira na kujizuwia kuchokozeka licha ya viongozi wa CCM kupania kuwaondoa kwenye mstari.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akipandisha bendera kuashiria kufunguliwa kwa barza moya ya Hatudanganyiki kijijini Upenja.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akipandisha bendera kuashiria kufunguliwa kwa barza moya ya Hatudanganyiki kijijini Upenja.

Sehemu ya mania ya polisi waliomwagwa leo Kitope kwa azma ya kuzuia kufanyika kwa mkutano wa hadhara wa CUF.

Sehemu ya mania ya polisi waliomwagwa leo Kitope kwa azma ya kuzuia kufanyika kwa mkutano wa hadhara wa CUF.

Advertisements

One thought on “Tumekwenda Kitope na Kitope imekuja kwetu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s