Poli-CCM itashindwa tu

Bila shaka sote ni mashahidi wa hali ya kisiasa na mwenendo wa vitendo vya hujuma dhidi ya wananchi wanyonge hususan wafuasi wa CUF-Chama Cha Wananchi. Mifano ya kushushwa, kuchanwa kwa bendera za CUF, kutiwa moto kwa ofisi za Chama hicho na kushambuliwa kwa wafuasi wake katika siku za hivi karibuni ni sehemu tu ya mifano mingi ya vitimbi vingi vinavyopangwa na kuratibiwa na wanasiasa muflisi kutoka Chama kilichikosa uhalali wa kisiasa,CCM.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, katika ziara ya kuwatembelea majeruhi wa mkasa wa Makunduchi tarehe 10 Aprili 2015.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, katika ziara ya kuwatembelea majeruhi wa mkasa wa Makunduchi tarehe 10 Aprili 2015.

Kwa bahati mbaya, Mamlaka zilizotarajiwa kuchukua hatua, kutokana na matukio tunayoyashuhudia, zimeshindwa kufanya kazi zake. Kushindwa huko kunaonekana kusababishwa na moja kati ya mawili haya: ama Mamlaka hizo zinajitisha na hivyo kuogopa kuwachukulia hatua wale wote wanaosikika kuchochea haya yanayoendelea na kufadhili uhuni huu au Mamlaka hizo zimeamua kuwa sehemu au tawi la hao waliotajwa hapo juu kwa lengo la kurakhisisha kufanikiwa kwa mipango yao michafu.

Tamko la hivi karibuni la jeshi la Polisi kuzuia wafuasi wa vyama vya siasa wa wilaya moja kutoshiriki shughuli za kisiasa, hasa mikutano, katika wilaya nyingine ni mfano tosha kuthibitisha maelezo haya kwamba Jeshi la Polisi limeamua kuwa tawi la CCM au limeamua kuacha dhamana yake iliyopewa kisheria; kulinda raia na mali zao, na badala yake wameamua kutoa ulinzi kwa makundi ya kiharamia yanayotia khofu wananchi.

Bila ya kumung’unya maneno, tamko hili la Polisi si tu limevunja Katiba ya nchi, lakini pia halina mashiko kwa mujibu wa Sheria za nchi na kwa hivyo linabaki kuwa ni la kishabiki na kwa hivyo hatupaswi kupoteza muda wetu kulijadili na ni bora kuliacha kwa yule aliyelitoa.

Lililo la muhimu kwetu ni kuhakikisha kwamba tunalipinga kwa mbinu mpya ili kuwaonesha vibaraka wote kuwa sisi wananchi tumechoka nao, tumeamua na hatuzuiliki tena.

Moja ya mfano wa mbinu tunazoweza kuzitumia ili kuhakikisha kuwa Jeshi la Polisi halifanikiwi katika mkakati wake, ni kukubaliana nao kutotumia magari ya wazi tuendapo mikutanoni, hasa mkutano wetu wa leo katika jimbo la master mind wa hujuma zote hapa Zanzibar, Seif Ali Idd-Kitope.

Ushauri wangu huu unatokana na ukweli niliouleza hapo juu kwamba hakuna mashiko kisheria katika kuzuia watu kwenda katika mikutano, hata hivyo jeshi la Polisi linaweza kutumia Sheria ya Usalama barabarani kukamata magari yote ya wazi, kuwafungulia mashtaka na kulazimisha hukumu za faini sambamba na vifungo kwa madereva wote watakaoshiriki kusafirisha wananchi kwenda katika mikutano ya CUF. Lengo la mpango huu ni kuwaogopesha wananchi ili kupunguza idadi ya watu katika mikutano ya CUF.

Ili kuwazodoa na kuwaonesha wajinga kwa kiwango cha juu ni vyema tukatumia mbinu mbadala kama vile kutumia mabasi kwa idadi kubwa hata ikiwezekana kusababisha upungufu wa daladala kwa watumiaji wa usafiri huo na kuhamasishana kutumia hikma na busara kwani mbali na yote mikakati yao inalenga kutuchokoza ili tuchokozeke na wafanikiwe kututoa katika mstari na wasababishe machafuko yatakayopelekea umwagikaji wa damu usio na sababu na kuchelewa kupatikana kwa Mamlaka Kamili ya Zanzibar kwa njia za kidemokrasia. Ni muhimu kusikiliza na kuzingatia maelekezo ya Viongozi wetu.

Hawakukosea wale waliolibatiza Jeshi la Polisi na kuliita POLICCM kutokana na kukubali kwake kuwatumikia wanasiasa uchwara.

Makala ya Hissham Abdulkadir

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s