CUF: Polisi chunguzeni la Makunduchi

“CUF inalitaka jeshi la Polisi kutodharau hujuma zinazofanywa dhidi yake na kwa hivyo lifuatilie kwa kina na kubaini njama za upangaji wa mipango ya hujuma kwa kuwachukulia hatua za kisheria bila ya kujali cheo cha yeyote miongoni mwao wale wote wanaochochea na kushabikia dhulma za aina hii kwa wananchi.”

Mmoja wa watu waliojeruhiwa

Mmoja wa watu waliojeruhiwa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Itakumbukwa kwamba jana, tarehe 29/03/2015 The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kilifanya ziara na mkutano wa hadhara Wilaya ya Kusini, jimbo la Makunduchi katika uwanja wa Jamhuri.

Wakihutubia Mkutano huo Viongozi wa CUF walizungumzia mwenendo na kuibuka kwa vitendo vya hujuma dhidi ya wafuasi wa CUF na majengo ya Ofisi za Chama hicho katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mfano, wakati akihutubia katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui alitahadharisha kuwa kuna taarifa za uhakika zilizoletwa uwanjani hapo kuwa kuna mpango ulioandaliwa wa kuwadhuru kwa kuwashambulia wananchi waliohudhuria mkutano huo na kwa hivyo kulitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha ulinzi katika maeneo yote ili kudhibiti na kuzima mpango huo.

Mbali na tahadhari hizo zilizotolewa mapema, Jeshi la Polisi lilishindwa kutoa mashirikiano kwa kuwapatia wananchi hao ulinzi hali iliyosababisha msafara wa uliokuwa ukitoka katika mkutano huo kuvamiwa, na wafuasi wa CUF kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.

Kufuatia matukio hayo, CUF-Chama Cha wananchi:
• Kinalitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kwa kuanza na wale wote waliotajwa kushiriki na kufadhili hujuma na uhuni dhidi ya wananchi waliokuwa wakitumia haki yao ya Kikatiba ya kushiriki katika shughuli za kisiasa kwa mujibu wa sheria za nchi.

• Kinalitaka Jeshi la Polisi kuwafuatlia na kuwachukulia hatua vijana wote waliohusika kuwavamia, kuwapiga na kuwajeruhi wananchi hao wasio na hatia yoyote.

• Kinalitaka Jeshi la Polisi kutodharau hujuma zinazofanywa dhidi ya CUF na kwa hivyo kufuatilia kwa kina na kubaini njama za upangaji wa mipango ya hujuma kwa kuwachukulia hatua za kisheria bila ya kujali cheo cha yeyote miongoni mwao wale wote wanaochochea na kushabikia dhulma za aina hii kwa wananchi.

• Kinalitaka Jeshi la Polisi kukomesha utaratibu wa CCM wa kukusanya vijana (JANJAWEED) kutoka maeneo mbalimbali ya nchi katika makambi na kuwapa mafunzo ya utumiaji wa silaha na kuwatia mori wa kupiga, kujeruhi na kuuwa kila asiyekubaliana na sera na matakwa ya CCM.

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO NA UMMA

……………………………………..
SALIM A. BIMANI

MKURUGENZI WA H/U/M/UMMA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s