CUF yaitaka JKU iende mahakamani

“Ili kuondoa shaka miongoni mwa wananchi juu ya kauli iliyotolewa na CUF na utetezi wa Kanali Ali Mtumweni kuhusu utendaji wa JKU, CUF inalitaka jeshi hilo kwenda katika vyombo vya Sheria, na kwamba ipo tayari kukutana na jeshi hilo katika vyombo hivyo na kutoa ushahidi utakaohitajika.”

Askari wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) wakishirika gwaride la heshima katika sherehe za Mapinduzi.

Askari wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) wakishirika gwaride la heshima katika sherehe za Mapinduzi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari, Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) limekanusha kauli iliyotolewa hivi karibuni kwamba jeshi hilo linapokea orodha ya majina ya vijana kutoka majimboni walioteuliwa kwa upendeleo kwa ajili ya ajira za vikosi.

Katika kukanusha kauli hiyo, Mkuu wa Utawala wa Jeshi hilo, Kanali Ali Mtumweni alisema ajira zote za Vikosi huratibiwa na Wizara ya Nchi (OR), Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ kwa kushirikiana na Tume ya Utumishi ya Idara Maalum ya SMZ.

Huku akishindwa kutaja jina la Kiongozi wa CUF alietoa kauli hiyo, Kanali Ali Mtumweni aliitaka CUF kutoa orodha ya majina hayo kwa kuyawasilisha Wizara husika na alitishia kuwa endapo CUF itashindwa kufanya hivyo ndani ya kipindi cha wiki moja Jeshi hilo litachukua hatua za kisheria.

Hatua hii ya JKU inafuatia Mkutano wa Hadhara wa CUF wa tarehe 21/02/2015 ambapo CUF-Chama Cha Wananchi kilieleza kwamba kina ushahidi wa jinsi upendeleo huo unavyofanyika katika uajiri wa Vijana wanaoomba kazi katika Vikosi vya SMZ na hasa katika Jeshi hilo.

Kwa kuwa CUF-Chama Cha Wananchi ni Taasisi kamili inayoendeshwa kwa mujibu wa taratibu na kuongozwa na watu makini, kinatambua uzito wa taarifa iliyozitoa na kwamba haikukosea wala kutoa kauli yake juu ya mfumo wa uendeshaji na utendaji wa Jeshi la JKU kwa kukosea.

Hivyo kwa msingi huo, CUF–Chama Cha Wananchi kinalitaka Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) kutambua dhima yake katika ulinzi na usalama wa nchi yetu na kuacha mara moja utaratibu wake uliozoeleka wa kufanya kazi kwa mashinikizo ya kisiasa na kutumikia matakwa ya wanasiasa.

Aidha, CUF-Chama Cha Wananchi kinalitaka Jeshi hilo kushughulikia kiini cha matatizo yake yaliyopo na kujikita katika kutimiza wajibu wake kisheria ili kuinusuru nchi na matatizo yanayoweza kuepukika, na

Ili kuondoa shaka miongoni mwa wananchi juu ya kauli iliyotolewa na CUF na utetezi wa Kanali Ali Mtumweni kuhusu utendaji wa JKU CUF-Chama Cha Wananchi kinalitaka jeshi hilo kwenda katika vyombo vya Sheria, na kwamba CUF-Chama Cha Wananchi kipo tayari kukutana na jeshi hilo katika vyombo hivyo na kutoa ushahidi utakaohitajika.

HAKI SAWA KWA WOTE

SALIM A. BIMANI

MKURUGENZI WA H/U/M/UMMA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s