Tindwa hafai kuwa mkuu wa mkoa

“Kwa mujibu wa Sheria za nchi, Wakuu wa Mikoa hawapaswi kushiriki siasa, hivyo vitendo vya Juma Kssim Tindwa ‘kuvaa’ mashati ya CCM na kutumia nafasi yake ya Ukuu wa Mkoa kutoa vitisho kwa wananchi wenye msimamo wa kisiasa tafauti na yeye na chama chake ni kinyume na utaratibu na haikubaliki. Hivyo, CUF kinamataka Dk. Ali Mohamed Shein kumfukuza kazi mara moja kiongozi huyo kutokana na kukosa sifa na kupoteza hadhi ya kuwa Kiongozi wa Umma wenye itikadi tafauti za kisiasa.”

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Juma Kassim Tindwa.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Juma Kassim Tindwa.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Itakumbukwa kwamba vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vimetangaza kususia Kura ya Maoni iliyoitishwa na Serikali kufanyika tarehe 30, Aprili 2015.

Msimamo huo wa UKAWA unafuatia kuvurugwa kwa Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hatua mbalimbali ikiwemo kupuuzwa kwa maoni ya wananchi, na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulazimisha kujadiliwa kwa Rasimu ya Chama hicho kwa lengo la kuhalalisha sera na matakwa yake katika upatikanaji wa Katiba Mpya.

Kutokana na msimamo huo wa UKAWA kuishitua Serikali na Chama Cha Mapinduzi, na kubainika kuwa wananchi wamefahamu mbinu na hila za CCM za kuiuza na kuipotezea Zanzibar hadhi yake na Mpango wa chama hicho kuhakikisha Zanzibar inaendelea kupoteza Mamlaka yake iliyonayo sasa, kumekuwa na mikakati mbalimbali ya kuwahadaa, kuwarubuni na kuwatisha wananchi wanaoonekana kwenda kinyume na msimamo wa Serikali na Chama tawala.

Kwa mfano, mnamo tarehe 08/03/2014 katika sherehe za kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika katika kijiji cha Nungwi CCM, kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Juma Kassim Tindwa, ilitoa vitisho vya kukamata, kupiga na kuuwa kila mwananchi atakayeonekana kwenda kinyume na matakwa ya CCM na kuendesha Kampeni ya ‘hapana’ dhidi ya Katiba inayopendekezwa.

Ni katika muktadha huu, The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kinatoa tamko lake:

  • Kwamba, asasi za kiraia na Jumuiya za Kimataifa zilizopo Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kufahamu kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimedhamiria kuendeleza uhuni wake wa kisiasa, kufanya vurugu kabla na wakati wa kura ya maoni na kuwa haina nia ya dhati ya kupatikana kwa Katiba Mpya kama ilivyodhihirishwa na chama hicho na viongozi wake kwa nyakati tafauti.
  • Kwamba, Kwa mujibu wa Sheria za nchi, Wakuu wa Mikoa hawapaswi kushiriki siasa, hivyo vitendo vya Juma Kssim Tindwa ‘kuvaa’ mashati ya CCM na kutumia nafasi yake ya Ukuu wa Mkoa kutoa vitisho kwa wananchi wenye msimamo wa kisiasa tafauti na yeye na chama chake ni kinyume na utaratibu na haikubaliki. Hivyo, CUF kinamataka Dk. Ali Mohamed Shein kumfukuza kazi mara moja kiongozi huyo kutokana na kukosa sifa na kupoteza hadhi ya kuwa Kiongozi wa Umma wenye itikadi tafauti za kisiasa.
  • Kwamba, kwa kuwa Juma Kassim Tindwa, ameshindwa kutafautisha baina ya Uongozi na ushabiki wa kisiasa, aachie ngazi ili awe na fursa nzuri kuitetea CCM na kwa upande wake CUF itakuwa tayari kupambana na mwanasiasa huyo mpya kwa hoja katika majukwaa ya kisiasa.
  • Kwamba, wananchi wasikubali kutishwa na wala wasirudi nyuma katika mapambano ya kuirejeshea Zanzibar Mamlaka yake Kamili. Kwa kuwa CCM imepoteza dira na mwelekeo na imebaini kuwa haina nafasi tena kwa Wazanzibari na watanzania kwa ujumla, wananchi wafahamu kuwa vitisho hivyo ni sawa na ‘tapatapa ya mfa maji’
  • Kwamba, wananchi wanaoendelea kuiunga mkono CCM wafahamu kuwa chama hicho hakina nia njema kwa mustakbali wa Zanzibar na watu wake. Vitisho, kejeli na kigeugeu cha viongozi wa chama hicho kabla na baada ya Bunge Maalum la Katiba imedhihirisha kuwa ni watu wa kujali matumbo yao na familia zao.
  • Kwamba, wananchi wote, bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, kuikataa Katiba inayopendekezwa na kwa wafuasi wa CCM kuipigia kura ya ‘Hapana’ Katiba inayopendekezwa ili kuyanusuru, kuyalinda na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya 1964.

HAKI SAWA KWA WOTE

……………………………………..

SALIM A. BIMANI

MKURUGENZI WA H/U/M/UMMA

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s