CCM machinjio ya Wazanzibari

Mahakama kuu ya Zanzibar imetakiwa kufuata haki zote na sheria ili mashehe wa jumuia ya uamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar (JUMUKI)waweze kutoka nje alau kwa kupatiwa dhamana kama wanavopewa washtakiwa wengine ambao wanaotenda makosa mbali mbali ndani ya Zanzibar au Tanzania kwa ujumala.

Kauli hio imetolewa na mkurugenzi wa haki za Binadamu habari uenezi na mawasiliano ya umma Mh,Salim Bimani wakati alipokuwa akizungumza na wanachama mbali mbali wa chama cha wananchi CUF pamoja na wazanzibar wanaopenda mamlaka ya nchi yao huko katika uwanja wa komba wapya wilaya ya mjini Unguja.

Akizungumzia kuhusu suala la kuyadai mamlaka kamili ya Zanzibar Bwana Bimani ameleza kuwa kwa wakati huu wazanzibar wenye mshikamano mkubwa wa kudai nchi yao wapo tayari kwa lolote lile na watahakikisha kuwa watapambana kwa njia ya amani na yoyote yule ambae haitakii mema Zanzibar mpaka pale watakapoyapata mamlaka kamili ya nchi yao.

Aidha alifahamisha kwamba kuna baadhi yawatu wasiojielewa wanadai eti mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Bwana Othman Masoud Othman afukuzwe kazi kutokana na msimamo wake wakuitetea Zanzibar na hatimae kuwa na mamalaka kamili kama zilivo nchi nyengine dunia.

‘’Tunataka tuwaambie hao wasiojua nini wanafanya wakisema wanajaribu tu kuandamana kwa kusisitiza mwanasheria mkuu afukuzwe basi na sisi wazanzibar wenye kutaka mamlaka ya nchi yetu tutandamana pia asifukuzwe’’alisema Bimani.
Sambamba na hayo aliwataka maelfu ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo kujua kwamba sasa sio tena hule wakati wa akupigae kulia ukamgeuzia kushoto badala yake akikupiga kulia na wewe mpige kushoto.

Pia Mh,Bimani alitoa wito kwa wananchi wote wa Zanzibar kuhakikisha wanaidai nchi yao katika njia za kisheria na amani tena bila ya kukubali kushawishiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kufanya vitendo vya hujma vyenye nia ya kuichafua Zanzibar kimataifa.

Nae mgeni rasmi katika mkutano huo ambae ni mjumbe wa baraza kuu taifa CUF na mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mh,Ismail Jussa Ladhu aliwashuru wananchi mbali mbali wa Zanzibar kwa kuwa na utamaduni wakufatilia kwa kina shughuli zote za uendeshwaji wa baraza la wawakiliahi kwani lengo la Mzee wetu Aboud Jumbe wakati analianzisha baraza hilo alilita ngome ya wananchi hivyo basi ni vyema zaidi kwa wananchi wa Zanzibar kuendelea na utaratibu walionao juu ya suala hili.

Jussa wakati akibainisha miongoni mwa kasoro kubwa zinazofanywa na baadhi ya watu wenye nyadhifa kubwa serikalini amesema kuwa kila mmoja wetu nadhani wameshuhudia jinsi wawakilishi wao walipofichua wizi mkubwa wa fedha unaofanywa na baadhi ya watu kwa makusudi kutokana tu na sababu za kutokuipenda kwao na kuiona Zanzibar inanawirika’’nataka wale wenye taka za mashikio wasikie makusudi juu ya maovu yao ili waiwache Zanzibar na hatimae iwe pepo ya dunia’’alisema Jussa.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa chama cha mapinduzi CCM Zanzibar ni kwamba wao wenyewe CCM tayari wameshaelewa tena kwa kina kabisa ninani anaiharibu nchi yao na tayari watu hao wamekuwa wakisema wazi wazi kwamba watamchagua Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na timu yake ili iwaongoze wazanzibar katika safari hii ya nchi yetu kushika mamlaka yake na hatimae kuwa dola kamili na kutambuliwa ulimwenguni kote.

Pamoja na hayo alizungumzika kuhusu suala uandikishwaji wa wapiga kura katika daftari lakudumu amebainisha kwamba ndani ya CCM kuna watu hivi sasa tayari wamebadilika mno na wanataka wale wote wasiohusika ndani ya daftari hio ambao wameorodheshwa kama ni wapiga kura basi watolewe haraka sana ili kuinusuru nchi katika matatizo na hatimae kuleta uchaguzi huru na wahaki wa mwaka 2015.

‘’Tena nataka nitume salamu hizi waziwazi kwa Mh Makamo wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, katika kikao kijacho cha baraza la wawakiliahi tutampa salamu zake Barazani, lakini leo acha nimpe hapa hapa, atafute wa kumtisha Jussa,Hija, Hamza, Omar Sheha, Asha Bakari, Salmin Awadh, hawatishikia tena na wote kwa pamoja hawatorudi nyuma katu na wataendelea kufichua uoza wao na ubatilifu wa mamilioni ya mali za umma ambazo ni kodi za wananchi wenye kipato cha chini hapa Zanzibar’’alieleza Jussa.

‘’Nataka niseme wazi mimi Jussa nimechaguliwa na wananchi wangu kwa ajili ya kufanya kazi zao kule barazani hivo Basi kama unanitishia amani nakuambia njoo unichukue hapa na unitie pingu lakini katu sitorudi tena nyuma kwa suala la kuyatetea maslahi ya wazanzibar’’alieleza.

Aidha alisema kwamba wanamshukuru Mungu kwa kujalia kumaliza salama mchakato wa utowaji wa maoni juu ya mabaraza ya katiba kwa salama na amani kwani lengo la baadhi ya wanan CCM ilikuwa nikuharibu mchakato huo lakini kwa uwezo wa Mwenyezimungu hawakuweza kufanya hivo, aliwataka wananchi wote waendelee kuwa na ustarabu huu wa utulivu na amani mpaka pale Zanzibar itakapokuwa na mamalaka kamili.

Alieleza kuwa katika wakati huu unadhani ninani asiejua kuwa wazanzibar wanataka nini kwa nchi yao mfano mdogo tu nadhani mulimsikia Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji warioba wakati alipofanya uzinduzi wa rasimu mpya ya katiba ya jamuhuri ya muungano Tanzania alisema wazi wazi kuwa wazanzibar wanahoja nzito sana na zinapaswa kusikilizwa lakini kwa kuhofia kuvunjika kwa muungano wameamua kuleta serikali tatu,Jussa aliwataka wananchi waliohudhuria katika mkutano huo kutokushuhulika na vutabu vya CCM hapa hakuna tena wa kuzuia mamlaka kamili isipokuwa Mwenyezimungu tu na Inshalla atatujalia.

Alisema kuwa muungano huu ni tofauti na miuungano yote, huu ndio muungano pekee wa kikatiba wa Nchi zilizokuwa zishakuwa huru jambo ambalo katika sheria za kimataifa ni lazima mahusiano hayo yawe na usawa na dola husika udogo au ukubwa wa nchi au uchache au wingi wa watu hayana nafasi, ndio maana ukienda Umoja wa mataifa unakuta nchi ndogo ya Nauru, ndani ya Umoja wa Mataifa ina haki sawa na nchi yeyote ile.

Akieleza kuhusu mfumo wa muungano alisema kwamba hakuna asiejua kuwa mambo ya muungano yalikuwa 22 lakini sasa sihaba wameyabakisha 7 na hayo 7 tunasema mengi tunataka mambo matatu lazima yarejee katika Mamlaka ya Zanzibar miongoni mwa mambo tunayoiyataka ni Nchi za nje,ili Zanzibar iweze kujiunga na jumuia yoyote hile ulimwenguni bilka ya vikwazo kama vilivyopo hivi sasa kwani mpaka leo hii tumeshindwa kujiunga na FIFA.

Uraia na uhamiaji lazima urudishwe Zanzibar,kwani hayo mataifa yote yalioendelea huko ulimwenguni basi nguvu kubwa iliyowasukuma kimaendeleo basi ni suala la uraia na uhamiaji hivo basi suala hili la urai na uhamiaji tunasema litolewe pia na liwe chini ya Zanzibar wenyewe.

Sarafu na benki kuu, kuendelea kutumia pesa hii isiyokuwa na baraka kutoka kwa wazanzibar wenyewe hatutaki tena, tunataka Safaru yetu ya Zanzibar na Benki Kuu ili turatibu shughuli zetu za kiuchumi wenyewe bila ya kuingiliwa na mtu yoyote yule au taifa lolote lile.

Akifafanua kuhusu baadhi ya watu wanaosema kwamba muundo wa serikali tatu ni mzigo nadhani mwanasheria mkuu wa serikali ambae ameteuliwa na raisi mwenyewe tena kwa kumuamini ameshawajibu na kuwaweka sawa tena kwa hoja nzito,na amebainisha waziwazi kuwa serikali tatu ndio suluhisho pekee kwa wazanzibar na nchi yao kwa sasa.

Wakati akieleza kuhusu tuhuma zilizopelekwa Dodoma za mwana kindakindaki Mansour Yussuf Himid ni nzito nazinatokana na msimamo wake wa kudai mamlaka kamili ya Zanzibar jambo ambalo sikosa na ni jema kabisa kwa kila mzanzibar anaeipenda kwa dhati nchi yake na kwa hili nataka niwapongeze vijana imara kutoka CCM kukubali kuwa hakuna kurudi nyuma juu ya suala hili na watashirikiana kwa kila mtu mwenye lengo jema kwa nchi yetu mpaka kuipata Zanzibar huru.

Lakini pia Jussa aliwataka vijana wa CCM kujua kwamba chama hicho kimezoea kuwa machinjio ya wazanzibar kutokana na viongozi kadhaa huku miaka ya nyuma kufukuzwa ndani ya chama hicho kwa sababu tu ya misimamo yao, lakini kwanini wasiwafukuze ili wapate kusheherekee kwa pamoja na katika suala hili wazanzibar tunawapongeza sana Mzee Moyo, Mansour, Edy Riyami na Marais wastaafu Karume na Salmin, na nataka niwahakikishieni kuwa tupo pamoja katika suala hili la kuirudishia Zanzibar sifa yake, na CCM kama hamujui basi munakizika chama chenu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s