“Haya ni mashambulizi dhidi ya Zanzibar”

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Salim Bimani.

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Salim Bimani.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. Kila mwananchi wa Zanzibar ameshitushwa na kusikitishwa na tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Kiengereza usiku tareh 7 Agost 2013 huko katika maeneo ya Mji mkongwe Zanzibar yaliopo mahoteli mengi na makazi ya wageni wanaotembele nchi yetu kutoka sehemu mbali mbali duniani.

Chama Cha wananchi CUF kinalaani kwa nguvu zote tukio hilo la kikatili la kuwamwagia tindi kwa wageni wetu hao,na kinalitaka Jeshi la Polisi Zanzibar kufanya uchunguzi wakina na waharaka pamoja na kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na tukio hilo la kikatili  wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Matokeo haya ya kikatili ya kumwagiwa kwa watu tindi kali yamekuwa yakishamiri siku hadi siku ndani ya visiwa vya Zanzibar,ambayo yamekuwa  yamewathiri watu kadhaa tena bila ya wahusika kuweza kupatikana na kuchukuliwa hatuwa za kisheria kiasi ambacho sasa jamii ya wazanzibar imejengeka katika hofu juu ya  usalama wa maisha yao ya kila siku,Hii ni dalili mbaya kwa Nchi ya Zanzibar kwani matukio haya ya tindikali yamekuwa yanaonekana kama ni masuala ya kawaida jambo ambalo linatishia uchumi wa Visiwa vyetu.

Kufanyiwa hujuma raia hao wakike wawili wa kigeni kutoka nchini Uengereza kigeni ambao walikuwa Zanzibar kwa kazi za kujitolea (valantia) kusomesha katika skuli za msingi (primary)
ni dhahiri kuwa  Sekta muhimu inayotegemewa katika kukuza uchumi wa Zanzibar (utalii)inaweza kutetereka.

Chama cha wananchi CUF kinawataka wananchi wote wa Zanzibar kutoa kila aina ya mashirikiano ya kuweza kufanikisha kukamatwa wahalifu hao na hatimae kufikishwa katika sehemu husika.

Sambamba na hilo Chama cha wananchi CUF Kinawataka Wanachi wote, Polisi jamii kutoa kila aina ya mashirikiano kwa Jeshi la Polisi ili jeshi hilo liweze kukomesha kabisa vitendo vyote vya kihalifu ndani ya nchi yetu, kwa lengo la  kuiendeleza sifa ya asili ya zanzibar isemayo kuwa Zanzibar ni njema atakae na aje…

Haki sawa kwa wote.

Salim A Bimani

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s