Z’bar iwe na Benki Kuu yake – BAKAZA

Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar ambae pia ni katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad.

Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar ambae pia ni katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad.

BARAZA la Katiba Zanzibar (BAKAZA) limekuja na mapendekezo mapya kuhusu rasimu mpya ya Katiba ya Muungano.

Katika mapendekezo hayo, BAKAZA limetaka Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano.

Mapendekezo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa BAKAZA, Prof Abdul Sheriff katika mkutano wake na vyombo vya habari.

Mapendekezo mengine ni kutaka Benki Kuu (BoT) Vyama vya siasa na uhamiaji yaondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano.

Pamoja na rasimu hiyo mpya, kuzingatia utaratibu wa Rais wa Muungano kupatikana kwa zamu kati ya washirika wa Muungano wa pande zote mbili, Zanzibar na Tanganyika.

Prof Sheriff alisema mapendekezo hayo yametokana na uchambuzi wa rasimu ya Katiba ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa Juni 3, mwaka huu.

Alisema hakuna sababu ya maana kwa Polisi na Usalama wa Taifa kuendelea kubaki katika orodha ya mambo ya Muungano katika mfumo wa serikali tatu.

Kwa mujibu wa mapendekezo hayo imeelezwa kuwa Ibara ya 217 ya rasimu ya Katiba ifutwe na kuruhusu kila mshirika wa Muungano kuwa na Benki Kuu yake itakayokuwa na mamlaka ya kusimamia sera za fedha pamoja na kuangalia mwenendo wa uchumi wa nchi husika, Tanganyika na Zanzibar:

“Ni vema Zanzibar ikawa na mfumo wa sarafu yake na Benki Kuu yake ili iweze kudhibiti na kuendesha uchumi wake bila ya kuathirika na Muungano kama ilivyo kwa Hong Kong na Macau ndani ya Jamhuri ya Watu wa China,” alisema Prof Shariff.

Hata hivyo, BAKAZA imesema kama suala la Mambo ya Nje litaendelea kubakia katika orodha ya mambo ya Muungano, basi nafasi za watendaji na mabalozi zitolewe kwa usawa kwa Zanzibar.

Mapendekezo hayo ambayo yanafungamana kwa kiwango kikubwa na msimamo wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

Ibara ya 2 ya rasimu ya Katiba, wametaka kuingizwa haki ya nchi mshirika wa Muungano kujitoa kwa kutumia utaratibu wa kura ya maoni, kama itaonekana hakuna manufaa yoyote katika muungano huo.

Prof Sheriff aliwaambia waandishi wa habari kuwa muhtasari wa mapendekezo hayo ndio utakuwa muongozo mkuu wakati wa kutoa elimu kwa wajumbe wa mabaraza ya Katiba katika visiwa vya Zanzibar, Unguja na Pemba..

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s