“Heko Baraza la Wawakilishi”

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Uenezi na Mahusiano na Umma, Salim Bimani.

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, habari,Uenezi na Mahusiano na Umma, Salim Bimani.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, lililokutana hivi karibuni na kukamilisha Mkutano wake wa Kumi na Mbili kwa umakini mkubwa, limeashiria kuwa ni chombo muhimu cha wananchi na pia moja ya mihimili mikuu imara ya dola katika kusimamia na kutekeleza majukumu yake kwa maslahi ya Nchi.

 

Heko Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, wa pande zote, kwa namna walivyosimama kuwasilisha michango yao, kujenga hoja, na hata ilipobidi kuihoji na kuibana Serikali pale ilipostahili, kwa kuzingatia maslahi ya maendeleo na ya wananchi waliowachagua.

 

Pongezi kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Naibu Spika, Wenyeviti wa Baraza, Viongozi na Wajumbe wa Kamati na Daraja mbali mbali kutokana na hikma na busara zilizoonyesha dira ya matumaini ambapo Nchi inahitaji kuelekea, umma umewashuhudia.

 

Chama cha Wananchi, CUF, kinachukulia ujasiri huo wa hali ya juu wa wahusika wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, kuwa ni ushindi wa jumla wa Wazanzibari.

 

Zanzibar ni Nchi inayohitaji mafanikio ya maendeleo katika ngazi zote, kupitia misingi muhimu ya demokrasia na utawala bora, chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo sasa imeweza kuangaza matumaini ya kweli ya ukombozi wa Wazanzibari wote.

 

Zama za ubabaishaji, ubadhirifu, ufisadi wa kupindukia, ubaguzi, vitisho na kila aina ya hujuma dhidi ya wananchi, Wawakilishi wa wananchi, watendaji waaminifu na waadilifu, na watetezi wote wa mali ya umma, zimepitwa na wakati duniani kote; huu ni wakati wa kuishi kwa kuchunga haki, demokrasia, utawala bora, sheria, umakini, na uwazi usioleta shaka.

 

Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wanayo haki, bila ya vitisho, ya kuhoji, kulaumu, kukemea na hata kukataza inavyostahiki, kila aina ya uovu na ubadhirifu hasa ule ambao Serikali inaendelea kuufumbia macho, na hayo ndiyo matarajio na maslahi ya umma.

 

Wazanzibari walishuhudia na kujenga matumaini, kupitia Mkutano huo wa Baraza la Wawakilishi, juu ya Miswada Miwili ya Sheria iliyopitishwa: Mswada wa Sheria ya Kutoza Kodi na Kubadilisha baadhi ya Sheria za Fedha na Kodi kuhusiana na Ukusanyaji na Udhibiti wa Mapato ya Serikali na Mambo mengine yanayohusiana na hayo, na pia Mswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Umma (Appripriation Bill).

Matumaini hayo yanakuja juu ya ile hima ya kudhibiti mianya ya uvujaji na ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kupitia utaratibu bora, na hilo ndilo ambalo Wawakilishi wao wenye azma njema wamekuwa wakilipigia kelele mara kwa mara.

 

La kushangaza na la kujiuliza ni mara ngapi Kamati za Baraza la Wawakilishi wamewasilisha ushahidi wa kutosha wa kitaalamu juu ya ubadhirifu na ufisadi unaotendwa na baadhi ya Watendaji wasiokuwa waaminifu na hadi sasa hazijaonekana hatua za kinidhamu? Nini watarajie wananchi juu ya mwenendo huo wa baadhi ya Watendaji wa Serikali, kama siyo kuendelea kufichua maovu, hata ambayo ni siri, ambayo mamlaka bado zinaendelea kuyakumbatia?

 

Kwa hili, Chama cha Wananchi, CUF, kinasema Wawakilishi lazima waendelee kuwa wakali bila woga, wasiogope vitisho, kwani wanaoteseka na kuteketea zaidi ni umma wa wananchi ambao ndio walipakodi.

 

Kuhusiana na vikundi na hata vyama vinavyojaribu kutafuta takwimu za wananchi kwa hiari, lazima ieleweke kwamba Jumuiya, Taasisi na Asasi za Kiraia, zinawajibika Kisheria na Kikatiba kufuatilia katika jamii ili kuelewa na kujiridhisha, nani anafuatilia nini na anawakilishwa vipi katika Mamlaka za Uwakilishi na hata katika kuongoza Nchi, hivyo hakuna mantiki yoyote ya vitisho, ghilba, au maonyo kutoka kwa viongozi.

 

Lazima ikumbukwe kwamba lipo Agizo la Msajili wa Vyama vya Siasa la kuzitaka jumuiya na taasisi husika kuratibu, kuhakiki, na kukuza taarifa za Wanachama kila inapowezekana ili kujenga ufanisi; hili si ajabu kwani Masheha wote, kwa muda mrefu, wamekuwa wakiendesha zoezi hilo, na kwa kukitumikia Chama fulani, hivi sasa CUF imo katika shughuli muhimu ya kukusanya Taarifa za wanachama wake katika majimbo yote, huu ni wajibu wetu kama Chama na Taasisi halali iliyosajiliwa nchini. “CUF haifanyi sense kama ilivyofikiriwa na ni vyema vyombo vya Ulinzi na Usalama, wakuu wa Mikoana, wilaya na Masheha walitambue hili na kuacha jazba ya kutaka kuvunja zoezi hetu hili ambali kwa Chama chetu ni muhimu sana.

 

Msajili alipoziona ofisi yetu ya Makao Makuu hivi karibuni alitutaka na kutuhimiza kuwatambuwa wanachama wetu kila tawi, Jimbo na wilaya na kuweka kumbu kumbu zao vizuri. CUF haingependa kuingiliwa katika shuguli na wajibu wake na kwa mujinu wa sheria.

 

Chama cha Wananchi, CUF, kinaitaka Serikali kuonya na kuwaadhibu, kwa mujibu wa Sheria, watu wanaowafanyia hila au vurugu wananchi wenzao wasijiandikishe katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, almuradi wanafuata utaratibu halali; hilo ni kosa la jinai na ni vyema atakayebainika kufanya hivyo achukuliwe hatua za kisheria.

 

Chama cha Wananchi, CUF, kinalaani mwenendo huo na kinaitaka Serikali kuwa makini hasa wakati huu ambao wananchi wanashuhudia ubadhirifu mkubwa wa zoezi hilo, ambapo yanaonekana makundi kwa makundi ya watoto na watu wasiostahiki, wakipelekwa kwa magari, kwenda katika Ofisi za Wilaya, wakiandikishwa, kinyume na utaratibu, huku watu ambao wanastahiki, wakinyimwa haki yao hiyo.

 

Kinachosikitisha zaidi wakati huu ambao Viongozi Wakuu wa Serikali, usoni mwa malka za kutunga na kusimamia Sheria, wakisisitiza umuhimu wa amani, utulivu na mshikamano, ambayo hayapatikani pasi na kuzingatia haki, umma unashuhudia, kwa makusudi wananchi wakinyimwa nafasi yao hiyo ya kisheria.

 

HAKI SAWA KWA WOTE

  

…………………………….

Salim Bimani,

Advertisements

One thought on ““Heko Baraza la Wawakilishi”

  1. Ni taarifa nzuri na njema lakini CUF ni mshirika ktk kuendesha Serikali? hivyo haipaswi kulalamika tu lakini pia kuchukuwa nafasi yake hata ikibidi kuwafikisha wavunja sheria ktk vyombo husika hasa mukiwa mnawafahamu. Kuwaachia ccm kufanya wafanyayo hapa pale mchana kweue kama Uchaguzi mdogo wa Bububu ni udhaifu mkubwa. Waziri wa Sheria si ccm, Chukuweni nafasi yenu adhimu (play yr vital role) kutandaza utawala bora kivitendo! Tuliamini mnaenda kuweka funzo Serikalini ya namna Nchi inavyoongozwa
    https://hakinaumma.wordpress.com/2013/08/07/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari-6/

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s