Mkoani wafuturu na Maalim Seif

 

Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisubiri kuswali sala ya Magharibi na badae kujumuika pamoja na wananchi katika ftari alioiandaa wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa kisiwani Pemba.

Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisubiri kuswali sala ya Magharibi na badae kujumuika pamoja na wananchi katika ftari alioiandaa wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa kisiwani Pemba.

Wananchi mbali mbali wilaya ya Mkoani mkoa wa kusini Pemba wamejumuika pamoja katika ftari maalumu ilioandaliwa na makamo wa kwanza Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad iliokuwa na lengo la kupata fadhila za Allah (s.w)hususan katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Wakati akizungumza mara baada ya kumaliza kwa ftari hio iliofanyika katika skuli ya Michenzani jimbo la Mkanyagni mkoa wa kusini Pemba,Maalim Seif ametowa shukrani zake za dhati kwa wananchi mbali mbali waliohushuria katika khafla hio.

‘’Ndugu wananchi mbali mbali mlioweza kuacha kazi zenu na kuitikia wito wangu napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwenu kwa kuacha kazi zenu na kufika hapa kujumuika na mimi nasema ahsanteni”alisema Maalim Seif.

Pamoja na hayo maalim Seif ameweza kuomba dua maalumu kwa ajili ya wananchi wote yakuwa mwenyezimungu awajalie wawe wenye kukubaliwa saumu zao sambamba na kusamehewa makosa yao wanayoyajua na wasio yajua.

Aidha amemuomba tena Allah (s.w)atujaalie tuwe miongoni mwa wenye kufadika na kuwa miongoni mwa watu wenye kurehemewa katika kumi la mwanzo la mwezi huu mtukufu wa ramadhani sambamba na maghfira la kumi la pili la mwezi mtukufu wa ramadhani kisha kumi la tatu la kuachiwa huru na moto.

Licha ya hayo Maalim aliwataka waislamu wote nchini kuendeleza umoja uliopo katika nchi yetu kwa ajili ya kuepusha matatizo mbali mbali yanayoweza kuiharibu nchi yetu na alisisitiza umuhimu wa wananchi kushikama na kuwa kitu kimoja.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi waliohudhuria hapo kaadhi wa wilaya ya Mkoani Sheikh Muhaammed Adam amemshuru sana Mwnyezimungu kwa kuweza kumpa moyo wa busara Maalim Seif na hatiame kufanya jambo kubwa sana mbele ya Allah la kuftarisha waislamu waliofunga jambo ambalo nijema sana mble ya Allah kesho Akhera.

Pamoja na hayo amewaomba waislamu wote kushikamana katika kuitetea dini ya Allah (s.w)na kufanya yale yote yanayompendezesha Mwenyezimungu.

Akizungumzia kuhusu suala la utulivu wa nchi amewanasihi wazanzibar kuulinda na kuuwezi umoja wa kitaifa uliopo kwani ndio umetufikisha hapa tukawa kitu kimoja bila ya kubaguana.

Maalim Seif na ujumbe wake tayari wamemaliza rasmi ziara ya kutembelea wagonjwa na wafiwa Zanzibar nzima katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhan.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s