Lipumba amshangaa Muhongo

ImageMwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema  anashindwa kumwelewa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kutokana na kauli yake ya mwanzoni mwa wiki hii alipowatoa maanani wananchi wa mikoa ya kusini walioandamana kudai maslahi yatokanayo na gesi ianyochimbwa kwenye eneo lao.

Katika matamshi hayo, sio tu kwamba Prof. Muhongo alisema wananchi hao hawana haki ya kutoa madai hayo, bali pia alikanusha ikiwa gesi hiyo inachimbwa kutoka Mtwara.

Profesa Lipumba amesema ikiwa Prof. Muhongo hajui hali halisi ya maeneo ya Watanzania, kama hawezi kusema gesi iko maeneo gani katika mikoa ya Tanzania, basi ni profesa wa ajabu kidogo. Hayo ni kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa (4 Januari).

Alifafanua kuwa anashindwa kumwelewa kwani anapingana na sera ya serikali ambayo yeye mwenyewe ni waziri.

Alisema kuwa kama gesi ilipoanza kuchimbwa Songosongo likajengwa bomba dogo la nchi 12 kusafirisha gesi chini ya bahari toka Songosongo hadi Somanga na bomba la nchi 14 lilijengwa toka Somanga hadi Dar es Salaam.

“Uwezo wa mabomba haya ni mdogo ukilinganisha na gesi inayopatikana Songosongo na mahitaji yake kwa shughuli ya kufua umeme na kutumia viwandani,” alisema.

Alisema kuwa mpango huu ulikubaliwa na serikali na ukaingizwa katika Mpango Kabambe wa Taifa wa kufua na kusambaza umeme, kwamba mradi huo wa kufua umeme MW 300 Mtwara ulipangwa uwe umekamilika mwaka huu wa 2012.

Lipumba aliongeza kuwa wananchi wa Mtwara wanahitaji kujua kwa nini serikali haikutafuta njia mbadala ya kugharamia mpango wa kufua umeme na kuiunganisha Mtwara na gridi ya taifa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s