CUF yaikata CCM vipande vipande Lindi

Mbunge wa Lindi (CUF), Salum Khalfan Barwany, akisalimiana na moja wa wapiga kura wa jimbo lake.

Mbunge wa Lindi (CUF), Salum Khalfan Barwany, akisalimiana na moja wa wapiga kura wa jimbo lake.

CHAMA  cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi, kimevunja kambi iliyokuwa inategemewa na Chama Cha Mapinduzi ya Kijiji Cha Mkundi, kata  ya Makata baada ya wanachama wote wa tawi hilo kujiunga CUF.

Wanachama hao wapatao 310  wa kijiji hicho ambacho kilikuwa kinafahamika kwa jina la utani la Dodoma ikiwa na maana ya makao makuu ya chama  tawala walikabidhi kadi za CCM ili wakabidhiwe za CUF na Mjumbe wa Baraza la Ushauri  Taifa la CUF ambaye pia ni Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwany.

Hayo yalitokea kwenye sherehe ya kumpongeza mgombea wa CUF, Jafari Nyimage aliyeshinda udiwani katika uchaguzi uliofanyika Novemba 28.

Akikabidhiwa  kadi ya CUF baada ya kukabidhi kadi ya CCM kwa niaba ya wanachama wengine, aliyekuwa Mwenyekiti wa tawi hilo la CCM, Jafari Masura alisema  wameamua kujiunga na CUF kutokana na matamko ya viongozi wa wilaya wa CCM ambapo alidai kuwa mbunge wa jimbo hilo alipofanya ziara kwenye kijiji hicho mara baada ya matokeo ya uchaguzi mdogo aliwafananisha wakazi wa kijiji na mbuzi aliyepotea.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

“Kauli ya mbunge wetu aliyoitoa mwezi uliopita ya kutufananisha na mbuzi aliyepotea na kudai amekuja kuwatafuta kutokana  na kumpatia udiwani mgombea wa CUF ilituudhi hivyo tumeamua kukihama chama hicho”alisema Masura huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya kata hiyo.

Akiwakaribisha wanachama hao wapya waliohamia kutoa CCM mbele ya wanachama na wapenzi wa chama hicho, Barwan aliwashukuru kwa kuamua kujiunga na chama na kuahidi kufanya kila linalowezekana kushirikiana katika harakati za maendeleo.

“Sasa hivi uelewa wa wananchi juu ya mfumo wa vyama vingi umeongezeka sana kwani miaka ya nyuma ilikuwa vigumu kukuta umati mkubwa  kama huu kwenye mikutano ya nyama vya upinzani na hii ilitokana propaganda za viongozi wa chama tawala ambao walidai upinzani ungeweza kusababisha vita,” alisema Barwany.

Chanzo: Mwananchi, Jumatatu,31 Disemba 2012

Advertisements

2 thoughts on “CUF yaikata CCM vipande vipande Lindi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s