ADC yachanwachanwa Tanga

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa ziarani Tanga.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa ziarani Tanga.

Aliyekuawa Mkurugenzi waulinzi na Usalama wa ADC bwana Albadawi amekichana chama hicho hadharani. Bwana Albadawi alisema kwamba yeye alikua na mashaka na mwenendo wa Hamad Rashid tokea zamani angalimo katika CUF ila alikua akimchunguza kwa makini na akisubiri ajiridhishe.

Bwana Albadawi baada ya kusikia Hamad Rashid ananzisha chama cha ADC alikua wa mwanzo kuingia kundini na kushiriki kukitafutia chama hicho usajili. Anasema nia mbaya ya Hamada Rashid juu ya uanzishaji wa chama chake aliubaini mapema mno pale Hamad Rashid alipokwenda kwa Kadinali Piicarp Pengo na kumuomba amsaidie kukipatia usajili chama chake. “Hamad kanusha kama hatukwenda kwa Pengo ukamuomba atusaidie usajili wa ADC” alisema Bwana Albadawi kwa hasira.

Aliwafahamisha wananchi wa Tanga kwamba Hamad Rashid alipachikizwa na Nyerere katika kundi alilolifukuza katika chama miaka ya 1980 ili akawachunguze wanachokifanya ili apelike habari kwa CCM na watawala. Bwana Albadawi alimalizia kwa kusema wameshindwa wenye nguvu kuimaliza CUF na Maalim Seif ataweza kibwetere Hamad Rashid? Akawatoa was was wananchi wa Tanga kwamba vurugu la Hamad Rashid limeshadhibitiwa na sasa ametulia kama maji ya mtungi hajui la kufanya wala la kuacha.

Halkadhalika wanachama 50 waliohi kukihama chama cha CUF kwa kushawishiwa kujiunga ADC wamerejea CUF na kumkabidhi Maalim Seif kadi za chama hicho hadharani. Wanachama hao walisema kwamba walihadaiwa na kutapeliwa na Hamad Rashid kwamba atawapatia mikopo ya kujiendeleza badala yake wapambe wake walitoa masharti kwa kila aliyehitaji mkopo huo kutoa kiasi cha shilingi 25,000 lakini matokeo yake walitoweka na fedha hizo.

Advertisements

4 thoughts on “ADC yachanwachanwa Tanga

  1. Hivi kweli chama kikubwa kama CUF mnaingia katika malumbano na chama kidogo kama ADC? Mimi nilidhani mshindani wa CUF ni CCM. Lakini sasa naona mnapoteza nguvu nyingi kujibizana na ADC , kulikoni? Tengezeni mikakati ni vp mtaipiku CCM 2015 . Huo ni ushauri wangu wa bure . Lakini mkitaka malumbano endeleeni mtaona faida yake siku za mbele.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s