CUF yamvaa Prof. Muhogo

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.

BARAZA Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF), limemvaa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kumtaka aueleze umma wa Watanzania sababu za kukatika umeme, hususan katika Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema wakati umefika kwa umma kujua ukweli kuhusu kile kinachotokea na si vinginevyo.

Alisema baraza hilo limemtaka waziri huyo kutoa ufafanuzi kutokana na kauli zake za awali za kusisitiza hakutakuwa na mgawo wa nishati hiyo muhimu, lakini taifa linashuhudia mgawo wa kimya kimya kila kukicha.

“Pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Muhongo kuwaeleza Watanzania kuwa hakutakuwa na mgawo na kwamba mgawo kwa sasa itakuwa ndoto, bado maeneo mengi ya nchi yetu ikiwemo Jiji la Dar es Salaam hali ya umeme si ya kuridhisha hata kidogo.

“CUF inamtaka Waziri wa Nishati na Madini kuwaeleza Watanzania nini tatizo la msingi juu ya suala la kuendelea kwa mgawo wa umeme kinyemela,” alisema Prof. Lipumba.

Aidha, alisema CUF inapinga mpango wa TANESCO kuongeza bei ya umeme na badala yake kuitaka serikali kuona umuhimu wa kuwa na mpango wa uhakika wa kuhakikisha tatizo la umeme linakwisha na Watanzania wengi wananufaika na huduma kulingana na gharama zinazoendana na hali za maisha yao.

Akizungumzia suala la michango kwa wanafunzi wanaoanza shule za msingi nchini, Prof. Lipumba alisema licha ya serikali kutangaza utoaji wa elimu ya msingi bure, lakini kumekuwepo na tatizo kubwa la michango na kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati suala hilo, kuhakikisha kuwa amri ya kutowachangisha wazazi michango hiyo inasimamiwa kwa vitendo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s