Kikwete, hivi ndivyo CCM yako inavyofanya siasa

Salamu maalum kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete, kuhusu viongozi wa CCM wanavyofanya siasa Zanzibar. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, anaonekana kuja na staili mpya ya kasi ya ubaguzi wa wazi na wa hadharani dhidi ya jamii za watu fulani huku Zanzibar.

Maskani kuu za CCM (KISONGE na KACHORORA) ambazo ni taasisi rasmi za CCM zinzonekana kufanya kazi ya kutumwa na chama chao kwa muda mrefu sasa kuwatukana na kuwakebehi Wazanzibari wenye asili ya Pemba akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad bila ya kukemewa.

Maskani maarufu kuu hapa Zanzibar zimekuwa kwa muda mrefu wakichapisha katika mbao zao za uchochezi maneno yanayohubiri matusi, kashfa dhidi ya viongozi wa CUF hususana Maalim Seif na kuwakejeli wazanzibari wenye asili ya Pemba.

Moja ya mabango ya kibaguzi ya maskani ya Kachochora mjini Zanzibar. CCM wameula na chuwa, Zanzibar hairudi tena nyuma.

Moja ya mabango ya kibaguzi ya maskani ya Kachochora mjini Zanzibar. CCM wameula na chuwa, Zanzibar hairudi tena nyuma.

Maskani hizo zimekwenda mabali zaidi kwa kujeli udugu wa jadi wa Unguja na Pemba kwa kuandika ujumbe unaohimiza na kutishia kuvunjwa kwa jamii ya kizanzibari na visiwa viwili vya Unguja na Pemba kutengana.

Jambo linaloshangaza wengi ni hivi jee viongozi wa CCM wa Zanzibar hawaoni uvunjifu huu wa umoja wa wazanzibari na watanzania kwa jumla? Hivi hawajui hawa wana CCM kwamba hata Rais wa Zanzibar nae anakejeliwa katika mbao za KISONGE na KACHORORA kwa kuwa ana nasabu ya Kipemba?

Badhi ya ujumbe uliokuwa unawekwa katika mbao zao hizo ni kama vile:

1. “Muungano huu ni wa watanganyika na waunguja nyinyi wengine hamumo rudini kwenu”. Kwa mjengeko wa Jamhuri ya muungano amabao hawajatajwa katika ujumbe huo ni wapemba ambao ndio waliokusudiwa kuwa wao hawamo warudi kwao.

2. “Muunganoi huu ni wa watanganyika na waunguja, hivi ndivyo vizazi halali vya nchi hii nyinyi rudini kwenu”. Halkadhalika hapa ujumbe huu unawatoa wapemba katika kizazi cha kitanzania kwa mujibu wa maskani za KISONGE na KACHORORA.

3. “Ammiii (wakimaanisha wapemba), kwanza tujadili muungano wa Unguja na Pemba halafu ndio tujadili Muungano wa Tanganyika na Zanzibar”.

4. “Msaliti wa Unguja ni Yule Yule Balahau (wakikusudia Maalim Seif na wapemba wenziwe) anapinga Mapinduzi ya 1964 na Muun gano wa Tanzania…..”

5. “Angalieni Sudan ya Kaskazini na kusini Vereje(itashindikanaje) Unguja na Pemba, Inawezekana”. Maana yake kama zilivyojitenga Sudan ya Kaskazini na Kusini na Pemba na Unguja nazo zitenganishwe.

Haya ndio mahubiri na siasa za CCM hapa Zanzibar kwa sasa wakifikiri kufanya hivi watawagawa Wazanzibari walioungana baada ya Maridhiano ya 2009. Lakini nawaambia: Yaguju, Wazanzibari wa ukweli hawataji Uuunguja wala Upemba maana Uzanzibari ni mkubwa kuliko hayo.

Ukimuona mtu anazungumzia Upemba na Unguja basi yeye si Mpemba wala si Muunguja. Wazanzibari wa kweli wameungana kudai mabadiliko ya mfumo wa Muungano kuipatia Zanzibar mamalaka yake kamili na yako njia ni yanakuja kupitia Muunganao wa MKATABA.

Iachie CCM itumie agenda ya kuwagawa Wazanzibari, lakini wajuwe kamwe hawagawiki ila CCM itajikuta ikikataliwa na sehemu kubwa zaidi ya jamii ya Kizanzibari. Wimbi hili ni kubwa na hakuna anayeweza kulizua hata kama akitaka!

Advertisements

4 thoughts on “Kikwete, hivi ndivyo CCM yako inavyofanya siasa

  1. nikweli ccm wengine hawajielewi ni aljununu fununu, wanajidai ni waz’bar lkn hawaitakii mema, je hiyo ni akili au matope? Zanzibar daima hadi kiama asietaka ahame. Cuf na uamsho ni wakombozi wa znz.

  2. Sote binadam duniani tuna pita
    acheni kuigawa zazibar wenyewe naishi kwaamani
    amna sababu ya kulazimisha jambo lisilo wezekana kwali tanzania ni yetu sote akuna nchi inabagua binadam wacheni waishi kwaamani wapemba jamani aya maishatu mschochee ugonvi ni asala kwa inchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s